Msamaha wa Celestine:Agosti 28,Kard.Semeraro atafungua Mlango Mtakatifu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ibada ya ufunguzi wa Mlango Mtakatifu, itakayoongozwa na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyikiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu, itaadhimishwa mnamo tarehe 28 Agosti saa 12.30 Jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Maria wa Collemaggio, “Santa Maria in Collemaggio, Jimbo kuu la Aquila, nchini Italia. katika ufunguzi wa Toleo la Maadhimisho ya Mwaka wa 729 wa Huruma ya Papa Celestine V. Siku hiyo saa 4.00 usiku kutafuatia tukio Msamaha wa vijana, skauti, vyama vya walei, na wahudumu wa kichungaji kwa misa takatifu itakayoongozwa na Askofu Michele Fusco, askofu wa Jimbo la Sulmona-Valva Italia . Baadaye, ni mkesha wa usiku wa Msamaha kuanzia saa 7 hadi za 12 alfajiri na Huduma ya Kichungaji ya Vijana wa Jimbo, kuanzia saa moja hadi saa 6 asubuhi, kwa kuabudu kimya kimya mbele ya Sakramenti Takatifu.
Jumanne tarehe 29 Agosti 2023, katika siku kuu ya kifo cha shahidi Mtakatifu Yohane Mbatizaji, saa 12 asubuhi Msamaha wa Wafanyakazi na misa iltaongozwa na Padre Sergio Nuccitelli, mkurugenzi wa ofisi ya Jimbo kwa ajili ya huduma ya kichungaji ya kazi; saa 1:30 Rozari itatangazwa mbashara kwenye Radio Maria. Saa 2.00 Msamaha wa watawa wa kike na kiume pia kutangazwa mbashara na Radio Maria na Misa itaongozwa na Askofu Gianfranco De Luca, askofu wa Termoli-Larino. Saa 4.00 Msamaha wa Vikosi vya Wanajeshi na Vikosi vya Polisi pamoja na Misa itakayoongozwa na Askifu Claudio Palumbo, wa jimbo la Trivento. Saa 5:30 asubuhi Msamaha wa makatekista na watoto, wanafunzi na walimu. Misa hiyo itaongozwa na Askofu Mkuu Orlando Antonini, balozi wa Vatican.
Msamaha wa familia utafanyika saa 6:30 machana huku Misa ikiongozwa na Askofu Mkuu Emidio Cipollone, wa Jimbo Kuu la Lanciano-Ortona. Alasiri, saa 10.00 jioni kutakuwa misa Misa ya Msamaha kwa ajili ya wagonjwa na ya ndugu na misa itaongozwa na Askofu Giovanni Massaro, wa Jimbo la Avezzano. Saa kumi na mbili jioni kutakuwa na masifu yatakayoongozwa na shemasi mkuu wa Jimbo kuu Sergio Maggioni. Na hatimaye, saa 12:30 misa ya kufunga Mlango Mtakatifu itakayoongozwa na Kardinali Giuseppe Petrocchi, Askofu mkuu wa mji mkuu wa Aquila, Italia. Tangu tarehe 28 Agosti saa 12.30 hadi -29 Agosti, saa 12.30 kutakuwa na sakramenti ya kitubio katika Kanisa Kuu hilo.
Jina Msamaha linatokana na Fahali wa Msamaha ambao Papa Celestine V alitoa huko Aquila, Italia mwishoni mwa mwezi Septemba 1294 na ambapo alitoa msamaha wa jumla kwa mtu yeyote ambaye angungama na kutubu dhambi zao kwa kuingia kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Collemaggio kuanzia tarehe 28 Agosti hadi tarehe 29 Agosti katika siku kuu ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji wangepokea wakati huo huo ondoleo la dhambi na kupata rehema kamili.