Tafuta

Hata Maaskofu katolini nchini Ghana kama ilivyo Niger, Nigeria na Burkina Faso wanapinga operesheni ya Kijeshi ya ECOWAS na wanaomba njia za diplomasia zitumike. Hata Maaskofu katolini nchini Ghana kama ilivyo Niger, Nigeria na Burkina Faso wanapinga operesheni ya Kijeshi ya ECOWAS na wanaomba njia za diplomasia zitumike. 

Ghana,Tamko la Maaskofu wa Ghana:ECOWAS itumie njia ya kidiplomasia na sio ya kijeshi

Hata Maaskofu Nchini Ghana wametoa Tamko wakitaka Njia ya kidiplomasia zifuatwe wakipinga uingiliaji wa kijeshi nchini Niger.Katika Tamko lenye saini ya Rais wa Baraza la Maaskofu(GCBC)walisema:“Hapana uingiliaji kati wa kijeshi chini ya mwelekeo wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baraza la Maaskofu nchini Ghana kama ilivyo kwa maaskofu Nchini Niger, Burkina Faso, na Nigeria,  wameelezea upinzani wao kuhusu uwezekano wa kuingilia kijeshi dhidi ya utawala wa kijeshi ambao ulichukua mamlaka nchini Niger tangu tarehe 26 Julai 2023. Katika tamko lao lililotolewa siku ya Alhamisi tarehe 24 Agosti 2023 na kutiwa saini na Askofu Mathayo Kwasi Gyamfi, wa Jimbo la Sunyani na Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Ghana (GCBC), linabainisha  kuwa: “Msimamo wa Baraza hilo ni kwamba "wazo la uingiliaji wa kijeshi wa  umuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi (ECOWAS) kwa ajili ya kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger haupaswi hata kufikiriwa”.

Mkutano wa wakuu wa Uchumi wa Jumuiya za Magharibi (ECOWAS) na kamati ya Ulinzi
Mkutano wa wakuu wa Uchumi wa Jumuiya za Magharibi (ECOWAS) na kamati ya Ulinzi

Baraza la maaskofu nchini Ghana (GCBC) linaeleza kuwa: “Mali na Burkina Faso tayari zimetuma ndege za kivita nchini Niger ili kukabiliana na uwezekano wa kuingilia kijeshi kwa ECOWAS”. Nchi hizo mbili, zinazotawaliwa na wanajeshi walioanzisha mapinduzi, kwa hakika zimethibitisha kwamba hatua zozote za kijeshi dhidi ya waasi huko Niamey zitafikiriwa kama tangazo la vita dhidi yao". Aidha Maaskofu wa Ghana wanakumbusha kuwa: “Zaidi ya hayo, Burkina Faso imetishia kujiondoa kutoka ECOWAS ikiwa kambi hiyo ingeingilia kijeshi nchini Niger.” Vile vile: “Sambamba na mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo (Rej. Yohana 14:27), sisi, kama  Baraza, tunapinga uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya waliopanga mapinduzi nchini Niger, kwani hii inaweza kuzidisha hali ambayo tayari ni hatari katika nchi hiyo ambapo raia kama vile wanawake, watoto, wazee, wanyonge na walio hatarini katika jamii wanabeba mzigo mkubwa wa hali ya machafuko haya.”

Watu wa Niger katika maandamano
Watu wa Niger katika maandamano

Kwa njia hiyo katika maelezo ya Tamko lao linabainisha kuwa: “Msimamo wa Baraza la Maaskofu Ghana ni kwamba ECOWAS na viongozi wake wanapaswa kufuata njia za diplomasia katika kushughulikia hali hiyo. Hii itahitaji ushirikiano zaidi na waliopanga mapinduzi ili kujadili dira halisi ya kushughulikia hali hiyo." Na kwa hiyo: " Baraza  la Maaskofu lina imani kwamba mbinu hii itawezesha pande zote na wapatanishi kuendeleza kwa haraka masuluhisho ya kudumu ya hali ya Niger,”  taarifa hiyo inahitimisha. Katika msimamo wa Baraza la Maaskofu wa Ghana dhidi ya hatua za kijeshi nchini Niger unaongeza ule wa Baraza la Maaskofu wa Kikanda wa Afrika Magharibi, RECOWA, (taz. Fides 10/8/2023), wa Mabaraza ya Maaskofu wa Nigeria na wa Niger na Burkina Faso (taz. Fides 7/8/2023) na wa Maaskofu wa Jimbo la Ibadan nchini Nigeria (taz Fides 22/8/2023).

Maaskofu Ghana wanaonya ECOWAS watumie njia za kidiplomasia na sio za kijeshi
25 August 2023, 18:10