Ask.Mkuu Perego,Mauaji ya wahamiaji baharini:ubinadamu unahitajika zaidi
Na Angella Rwezaula; - Vatican
Idadi ya wahamiaji waliotua nchini Italia mnamo 2023 imezidi 100,000 na, kwa bahati mbaya, idadi ya vifo baharini pia inazidi kuongezeka. Rais wa Tume ya Maaskofu ya uhamiaji na wa Mfuko wa Wahamiaji ametoa wito mpya kuhusu bahari yetu na kukemea hali ya kushangaza ambayo itakua zaidi na zaidi, na kukosekana kwa utulivu wa nchi mbalimbali za Afrika kutasababisha mzunguko zaidi". Kutua kwa wahamiaji nchini Italia kumeongezeka zaidi ya mara mbili katika miezi saba ya kwanza ya 2023. Idadi ya mauaji baharini inaongezeka na Papa Francisko alikuwa ameelezea wasiwasi wake mkubwa katika Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 13 Agosti 2023 alipozungumzia juu ya "ugonjwa wa ubinafsi ulio wazi katika ubinadamu wetu huku", akiomba "juhudi za siasa, diplomasia, za wale wote wanaofanya kazi ya kuzuia ajali za meli na kuokoa mabaharia. Tangu mwanzoni mwa mwaka, tayari wanaume, wanawake na watoto 2,000 wamekufa katika bahari hiyo wakijaribu kufika Ulaya," alisema Papa.
Kwa Watu 2060 walioachwa kufa baharini, wakiwemo watoto, wanawake na wazee, ni janga ambalo linazidi kuwa mauaji amesema hayo Askofu Mkuu Gian Carlo Perego, wa Jimbo kuu Ferrara-Comacchio, na Rais wa Tume ya Uhamiaji ya Baraza la Maaskofu Italia pamoja na Mfuko wa Wahamiaji. Kwa mujibu wake amesema Ni hali ya kushangaza ambayo itakua zaidi na zaidi, kwa sababu kukosekana kwa utulivu kwa nchi mbalimbali za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambayo kwa mfano Niger pia inajiunga nayo, kutaunda mzunguko na njia zaidi.” Waathirika wengi wanaweza kulinganishwa na watu ambao wameachwa kufa, askofu mkuu alisisitiza na hili lazima lihoji dhamiri yetu na wajibu wetu. Kwa upande wake Askofu Mkuu Perego, kwa hiyo, si wakati wa maneno tu, bali ni wakati wa kutafakari upya operesheni ya uokoaji katika Mediterania ambayo ina changamoto kwa Ulaya yote. Aliita operesheni mpya ya Bahari yetu (Mare Nostrum), ambayo ina uwezo wa kuwazuia na kuwaokoa watu. Wakati huo huo, marekebisho ya mfumo wa hifadhi ya Ulaya na mpango wa ushirikiano wa kimataifa na nchi zote zinazohusika katika mapokezi ni muhimu. Hii, hata hivyo inachukua muda mrefu, wakati huo huo kuna haja kamili ya watu kutoachwa wafe.
Hali ni ya wasiwasi sio tu baharini, lakini pia baadaye, baada ya kutua. Kulingana na rais wa Wahamiaji, kuna haja ya kuwa na mfumo ambao unaweza kusaidia kweli watu kujumuika katika nchi ya kuwasili. Vibali vya ulinzi wa kibinadamu ni muhimu, shukrani ambayo watu wanaweza kwenda kufanya kazi mara moja na hivyo kujenga uhuru fulani. Kwa bahati mbaya, mfumo wa mapokezi unatatizika katika saa hizi kwa sababu watu wengi wanalazimika kuondoka kwenye vituo ili kutoa nafasi kwa wahamiaji wapya wanaowasili. Kila mtu anahitaji kulindwa katika utu wake na hii ni ahadi ambayo tunatekeleza, kufungua nyumba na vituo vipya, alisisitzza Askofu Mkuu Kulingana na rais wa Wahamiaji, kuna dhana mbili za kimsingi ambazo zingesaidia hali: ushirikiano wa maendeleo na upokonyaji silaha. “Tunahitaji kuwapa watu fursa zaidi za kuweza kuishi katika ardhi yao wenyewe kwa amani na kuweza kuwa na njia hizo zinazoweza kuwajengea maisha katika eneo hilo”, anafafanua. Hata suala la deni la nje, ndio hitimisho lake ambalo bado ni janga na ambalo mara nyingi haliruhusu nchi masikini kuwa na uwezo wa kujitolea rasilimali nyingi katika miradi ya elimu, afya na maendeleo.”