Patriaki Sako ametangaza kuhamia Kurdistan
Vatican News
Kadinali Louis Raphaël Sako, Patriaki wa Babilonia ya Wakaldayo, alitangaza hadharani uamuzi wake wa “kujiondoa kutoka Makao makuu ya Upatriaki wa Baghdad na kwenda kwenye kanisa, kwenye utume wa kimisionari katika moja ya monasteri za Kurdistan ya Iraq”.
Tangazo hilo, lililochapishwa kwa Kiarabu kwenye tovuti rasmi ya Upatriaki wa Wakaldayo Jumamosi tarehe 15 Julai, linafuatia na uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Iraq, Abdul Latif Rashid, wa kufuta amri iliyoanzishwa mnamo mwaka 2013 na mkuu wa zamani wa nchi, Jalal Talabani, ambapo Kardinali Sako alitambuliwa kuwa Patriaki wa Kanisa la Wakaldayo. Kutenguliwa huko “hakuna mfano katika historia ya Iraq”, amesisitiza kardinali, akimulika “ukimya wa serikali” juu ya kile kilichotokea na mateso ya jumuiya ya Kikristo.