Papa ameteua Jimbo jipya Wote nchini Kenya na Askofu wake wa kwanza!
Vatican News.
Jumamosi tarehe 22 Julai 2023, Baba Mtakatifu Francisko ameteua Jimbo Jipya Katoliki liitwalo Wote, nchini Kenya kwa kuligaliwa Jimbo la Machakos na kulifanya kuwa sehemu ya Jimbo kuu la Nairobi, Kenya. Na wakati huo huo akamteua Askofu wake wa Kwanza wa Jimbo katoliki la Wote, ambaye ni Askofu Paul Kariuki Njiru, hadi uteuzi huo alikuwa ni Askofu wa Jimbo katoliki la Embu.
Jimbo jipya la Wote nchini Kenya liko katika Kaunti ya Makueni. Limegawanywa kutoka katika Jimbo Kuu la Nairobi. Makao ya jimbo hilo ni mji wa Wote. Kanisa Kuu katika Mkutadha wa Jimbo Jipya kikanisa kwa sasa ni Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi. Idadi ya watu kwa mujibu takwimu za mwaka 2022 Machako, kuwa kabla ya mgawanyiko, machakos ilikuwa na 14.135, (km²) na Jimbo jipya la Wote kwa sasa ni 8.009, (km), baada ya kugawanya Machakos inabaki na 6.126 km.
Kuhusu idadi ya watu na idadi ya wakatoliki
Kabla ya Mgawanyiko Machakos ilikuwa na watu 2.409.585, jimbo jipya la Wote sasa ni 987.653 na baada ya mgawanyiko Machakos inabaki na watu 1.421.932. Wakatoliki kabla ya mgawanyiko Machakos walikuwa ni 999.096, jimbo Jipya la Wote sasa ni 388.946 na baada ya mgawanyiko machakos wakatoliki wanabaki 610.150.
Parokia na mapadre
Parokia za Machakos zilikuwa jumla 80, na Jimbo Jipya la Wote sasa ni 31 na Machako inabaki na parokia 49. Mapadre wa jimbo la Machakos walikuwa 202 kabla ya mgawanyiko kwa hiyo jimbo jipya ka Wote linakuwa na 90, na Jimbo la Machakos libaki na mapadre 112.
Mapadre wamisionari na mashemasi
Wakati Mapadre wamisionari machako walikuwa ni 31 Jimbo jipya wanakuwa 9 na Jimbo linabaki na mapadre wamisionari 22. Mashemasi wa Jimbo la Machakos walikuwa ni 9, Jimbo jipya Wote ni 3, na libaki na mashemasi 6. Waseminaristi wa Mchakos walikuwa 69, jimbo jipya wote 36, na kubali na mashemasi 33.
Makatekista
Makatekista, wa Machakos walikuwa ni 1.660, Jimbo Jipya Wote wanakuwa 732, na Machakoc libaki na makatekista 928. Mashirika ya kitawa wanaume 9, na ya Kike ni 39 ya Jimbo la Machakos.
Mashirika ya kitawa Machakos na Taasisi za Elimu
Mashirika ya kitawa wa kike 56 Machakos. Watawa wa kike ni 249 Jimbo la Machakos. Taasisi za Elimu Machakos zilikuwa 544, sasa Jimbo la Wote ni 200 na kubaki taasisi 344 Jimbo Kuu la Machakos.