Tafuta

Viongozi wa Kikristo kushirikiana na wa kijamii ili kuleta sulihisho la matatizo ya nchi. Viongozi wa Kikristo kushirikiana na wa kijamii ili kuleta sulihisho la matatizo ya nchi.  (AFP or licensors)

Guinea:Viongozi wa Kikristo na Kiislamu wakubaliana kushughulikia matatizo ya nchi

Hatimaye nchi ya Guinea baada ya migororo mingi kwa miongo kadhaa,Askofu Raphaël Balla, wa Jimbo katoliki la N'zèrèkore anakiri kuwa sasa nchi hiyo mojawapo ya nchi zenye maendeleo duni zaidi barani Afrika,baadhi ya mambo yanaendelea vizuri: “Jeshi linafanya kazi na wanafanya kazi kwa kutazama matokeo ya ujenzi wa barabara na miundombinu kitaifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Guinea Conakry ni nchi ya Afrika Magharibi ambayo tangu uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mnamo  Oktoba 1958,inapakana na Mali, Sierra Leone na Bahari ya Atlantiki, na sehemu ya kaskazini inapakana na kona ya Guinea Bissau na moja ya nchi ya Senegal. Nchi hiyo imepata mapinduzi matatu:  ya kwanza mnamo mwaka 1984, pili mnamo  mwaka 2008, ya mwisho mnamo Septemba 2021. Mapinduzi ya mwisho bila kumwaga damu, ni sehemu kamili ya wimbi jipya la mapinduzi ambayo yamezikumba nchi mbalimbali za Afrika, hasa katika eneo la Sahel-Magharibi ambayo mara nyingi yalifanyika bila umwagaji damu na kwa msaada fulani maarufu. Mapinduzi nchini Guinea mwezi Septemba miaka miwili iliyopita yalikomesha serikali ya Rais Alpha Condè, aliyechaguliwa tena hivi karibuni kwa muhula wa tatu uliokuwa na ushindani mkubwa, na kumuingiza Mamady Doumbouya madarakani. Mwaka mmoja na nusu baada ya mabadiliko haya ya ghafla katika siasa za Guinea, machafuko yanajirudia nchini humo kutokana na maandamano yaliyoandaliwa na upinzani, kuchoshwa na kusubiri uchaguzi na maendeleo katika kipindi cha mpito kilichoahidiwa na utawala wa kijeshi ambao ungechelewa kufika.

Wakristo ni wachache nchini Guinea lakini wanaoshirikiana na waislamu
Wakristo ni wachache nchini Guinea lakini wanaoshirikiana na waislamu

Katika hali hiyo, Askofu Raphaël Balla, wa Jimbo katoliki la N'zèrèkore kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari za Kimisionari Fides  anakiri kwamba sasa nchini humo, mojawapo ya nchi zilizo na maendeleo duni zaidi barani Afrika, baadhi ya mambo yanaendelea vizuri: kwa sababu “Jeshi linafanya kazi, na wanafanya kazi kwa kutazama matokeo ya barabara, miundombinu inaanza kufanya kazi. Kuhusu siasa, wale wa upinzani wanataka mpito uwe mfupi na mchakato uharakishwe. Pia wanalalamika sana kwa sababu kuna viongozi wamefungwa, hata kama, shukrani pia kwa upatanishi wa askofu mkuu wa Conakry Vincent Coulibaly, kumekuwa na matokeo mbalimbali hivi karibuni. Kulingana na Askofu Balla, ni muhimu pia kutambua kwamba wakati mwingine maandamano ya upinzani yanazuia nchi, watu hawawezi kufanya kazi, watoto wana shida ya kuhudhuria shule. “ Lakini katika maeneo ya bara, kwa mfano ninapoishi, karibu kilomita 1000 kutoka mji mkuu, kutoka eneo hilo  kwa mtazamo hakuna matatizo”.

Nchini Guinea ni moja ya nchi maskini barani Afrika kutokana na mizozo ya ndani na mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara
Nchini Guinea ni moja ya nchi maskini barani Afrika kutokana na mizozo ya ndani na mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara

Askofu aidha anakiri kwamba hata katika nchi yake, kama ilivyotokea katika nchi nyingine katika eneo hilo, jeshi la mapinduzi linaungwa mkono fulani na wananchi: “wananchi wanaendana na utawala huu. Hata kunapokuwa na maandamano dhidi ya jeshi, kadhaa yanaibuka.” Zaidi ya hayo, “inavyoonekana, ni viongozi wa kisiasa nje ya nchi ambao wanadanganya idadi ya watu na kuna ripoti kwamba vijana wanapokea pesa za kuingia mitaani kuandamana, na hii sio nzuri”. Miongoni mwa dalili chanya za mabadiliko, Askofu Balla anaorodhesha uboreshaji wa jumla wa hali katika mji mkuu Conakry, na maendeleo ya miundombinu: “mtandao wa barabara umeboreshwa, na hata tatizo la zamani la umeme sasa linakaribia kutatuliwa katika miji mbalimbali. Ninapoishi, umeme hufanya kazi kikamilifu, na pia katika mji mkuu na miji mingine. Hadi miaka michache iliyopita, ilikuwa ni huduma duni sana na hivyo sasa wanajenga nyumba mpya zenye viwango vya kisasa, na uchumi unaimarika.

“Zaidi ya hayo, naweza kukuhakikishia kwamba miundombinu mingi imejengwa kwa rasilimali za nchi, si kwa msaada  kutoka nje. Vijana wote wanakwenda shuleni, ambayo inachukuliwa kuwa ya msingi na wote. Pia kwa sababu hiyo, idadi ya watu hutazama maandamano hayo kwa kutokuwa na imani, kwa sababu yanazuia mwendo wa kawaida wa masomo”. Jumuiya ya Kikatoliki inawakilisha sehemu ya wachache katika idadi ya watu (85% Waislamu, 10% Wakristo, ambapo 8% Wakatoliki, na wengine wanawakilishwa na madhehebu na imani za kimila, lakini ni sehemu inayosikilizwa nchini, pia ngazi ya kijamii na kisiasa. “Wawakilishi wa jumuiya ya Kikatoliki kwa muijibu wa Askofu Balla “huingilia kati masuala ya umma, na daima hufanya hivyo pamoja na Waislamu. Kunapokuwa na matatizo, wanasiasa au wananchi wanamgeukia Askofu Mkuu Vincent Coulibaly na Imamu Mkuu El Hadj Mamadou Saliou Camara.

Mamlaka hizi mbili mara nyingi huitwa wakati upatanisho unahitajika. Na haya yote hayafanyiki tu sasa, lakini pia yalitokea chini ya Alpha Condè. Watu huwasikiliza. Viongozi wa Jumuiya ya Kikatoliki daima wamekuwa na tabia hii ya uwazi kwa mazungumzo jumuishi, ambapo kila mmoja anaweza kuingilia kati kusaidia ukuaji wa nchi. Hii pia ndiyo sababu Askofu Mkuu na Imam waliingilia kati kwa ajili ya kuachiliwa kwa viongozi wa upinzani waliokuwa wamefungwa. Nchi inahitaji katiba mpya ambayo bunge la mpito italazimika kuunda, na kila mtu anahitajika. Jumuiya ya Kikatoliki pia inawakilishwa katika Bunge hilo hilo”. Mamlaka zilizoanzisha vigezo vya uteuzi wa Bunge la mpito kiukweli pia zimetaka jumuiya za Kikatoliki na Kiislamu kueleza mwakilishi wao wenyewe, amefafanua.

Viongozi wa kidini huko Guinea Conakri

 

03 June 2023, 11:20