Tafuta

Kutawazwa kwa Mfalme Charles III. Kutawazwa kwa Mfalme Charles III. 

Uingereza wanaye Mfalme mpya Charles III ambaye ametawazwa!

Tarehe 6 Mei 2023 ametawazwa Mfalme Charles III nchini Uingereza,katika Kanisa Kuu la Kianglikani la Westminster kwa kuudhuriwa na viongozi wa mataifa mbali mbali na wa kidini.Misa iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury,Justin Welby.Baada ya mahubiri umeimbwa wimbo wa Uje Roho Mtakatifu na nyingine.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Kanisa Kuu la la Kianglikani la Westmister, nchini Uingreza, lilijaa ishara mbali mbali za kiutamaduni na mpya katika afla kuu ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III. Kwa mfano katika tukio hili ilionekana jinsi ya kuingia  katika Kanisa Kuu, kabla ya kiapo, sala, mahubiri, hatimaye kivalishwa nguo za kifalme adharani na taji…. Wakati huo huo, kwaya iliimba vizuri sana….. sala za kumbariki baada ya kuvikwa taji na wawakilishi kutoka makanisa mbali mbali  kumtakia baraka, na kuhitimisha na  Askofu Mkuu Justin Werby. Miongoni mwa waliomtakia baraka alikuwa ni Askofu mkuu Katoliki Kardinali Nicols wa Uingereza na Wales. Baada ya  wimbo ilifuatiwa hatua ya Malkia  Camila kuvalisha kofia ya kimalkia na pete. Wote wawili walikwenda kutoa mavazi hayo na kuendelea na ibada iliyoja alama nyingi. Baadaye kulikuwa na kupokea Ekaristi na damu ya Kristo.

Kabla ya kutawazwa
Kabla ya kutawazwa

Na katika katika gazeti la Osservatore Romano, Askofu mkuu wa Westminster na mkuu wa Kanisa la Uingereza na Wales Kardinali Nicols katika maoni yake siku moja kabla ya tukio alisisitiza  vipengele vikuu  vya sherehe kuwa ni maonesho ya kina na ya uaminifu ya imani ya Kikristo na matumaini. Maneno ya ufunguzi ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III, ambayo yamefanyika Jumamosi kwa hiyo tarehe 6 Mei  2023 huko Kanisa Kuu la iangalikan la Westminster ni muhimu sana. Aliyekuwa wa kwanza kuongea ni mwimbaji wa kwaya, ambaye alisema: “Ee mfalme, kama watoto wa Ufalme wa Mungu tunakukaribisha kwa jina la Mfalme wa Wafalme”, ​​na Mfalme Charles alijibu: “Kwa jina lako, na kwa mfano wako; sikuja kutumikiwa, bali kutumikia.”

Malkia Camilla
Malkia Camilla

Kwa hiyo sherehe iliyofuata ni ya Kikristo sana katika kila hisia na vitendo, ikichanganya historia na uvumbuzi, kitendo na neno, muziki na sala ya kimya.  Kardinalia alisema alivyoambiwa kuwa katika kumbukumbu za Jumba la Lambeth  kuna kumbukumbu za kutawazwa kwa wafalme na malkia wa karne ya 11. Katika kutawazwa huko kuna vipengele vinne vya kudumu: upako wa mfalme, kutawazwa, utoaji wa upanga wa haki na upokeaji wa komunio. Ishara zote hizo ambazo zilionekana wazi wakati wa kutawazwa.

Mfalme Charels wakati anakwenda Kanisa Kuu
Mfalme Charels wakati anakwenda Kanisa Kuu

Mambo hayo yote yaliyokuwapo katika  kutawazwa huko, yameimarishwa na ishara nyingine nyingi za jadi, ikiwa ni pamoja na kupewa baadhi ya vitu, kutia ndani orbi ya kifalme, ambayo inawakilisha mamlaka ya kidini na kiadili, fimbo ya enzi, inayowakilisha mamlaka, na fimbo ya enzi ya enzi kuu, fimbo ya dhahabu iliyoinuliwa na njiwa mweupe, ishara ya haki. Kwa hiyo ni sherehe iliyoonesha utajiri wa mila, na kwa hiyo kuendelea na utulivu. Muziki wa kwaya uliotungwa hivi karibuni ulisikika, ukiimbwa katika lugha tofauti za visiwa mbali mbali. Watu wa mataifa mbalimbali walialikwa, pamoja na viongozi wa mataifa mbalimbali au utoaji wa zawadi.

Mfalme Charles III
Mfalme Charles III

Wigo kamili wa madhehebu ya Kikristo  pia ulilikuwapo, na baadhi walikuwa na sehemu hai ya kutekeleza. Mwishoni mwa sherehe, kabla ya kuondoka Kanisa Kuu la Kianglikani la Westminster, Mfalme alisalimiwa na viongozi wa kidini wa madhehebu mengine, ambao walimtaja kuwa karibu na imani. Kwa njia hiyo pia Askofu Mkuu Nocols alipokea mwaliko akawa mmojawapo wa kumtakia baraka  ya kutambuliwa kutoka kwake. Historia ya nchi hizi inamulikwa sana na historia yao ya kidini. Hadi karne ya 16 kutawazwa kulikuwa kwa Kikatoliki tu. Imekuwa huduma ya Kanisa la Kianglikani kwa miaka mia nne iliyopita na inaendelea kuwa hivyo. Lakini wakati huu mambo mengi ya tukio yanaakisi na kuimarisha mahusiano yaliyobadilika sana kati ya Makanisa mawili ya kianglikani na Kikatoliki.

Mtoto wake Mkubwa na Familia yake
Mtoto wake Mkubwa na Familia yake

Ikumbukwe hivi karibuni  Papa Francisko alimpatia Mfalme Charles III masalio ya msalaba wa kweli wa Kristo. Masalio yaliwekwa kwenye msalaba wa fedha, ambao umebebwa wakati wa maandamano ya kwanza katika siku ya kutawazwa kwa Mfalme  Charles III. Baba Mtakatifu Francisko amewakilishwa katika kutawazwa na Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican akifuatana na Balozi mpya wa Vatican nchini humo Askofu Mkuu Maury Buendia. Sherehe yenyewe imekuwa na matokeo mengi ya asili yake ya Kikatoliki kwa mfano: kulikuwa na  wimbo wa Kyrie (utuhutumie), Veni Sancte Spiritus,(Uje Roho Mtakatifu) Te Deum, ambao ni  wimbo wa shukrani na Gloria yaani utukufu, ambao ni  mpango ulioandikwa katika karne ya 16 na William Byrd kwa ajili ya wapinzani wa Kikatoliki. Kama Kardinali Askofu Mkuu wa Westminster  alialikwa kushiriki katika baraka ya mfalme mpya aliyetawazwa, jambo jipya ambalo linawakilisha hatua nyingine mbele katika uponyaji wa majeraha yao ya kizamani. Historia yao, kiukweli, ni historia ya mgawanyiko, na hii pia inaonekana katika kutawazwa kwa sasa. Umuhimu wa utamaduni ni kiapo kilichotolewa na mfalme kabla ya kutiwa mafuta na kutawazwa.

Mtoto wake wa pili Harris akiwa anakwenda Kanisa Kuu
Mtoto wake wa pili Harris akiwa anakwenda Kanisa Kuu

Tukio la kutawazwa likiendelea kulikuwa na sehemu ya Mfalme kujibu maswali haya: “Je, utafanya yote uwezayo kuweka Uingereza katika Dini ya Marekebisho ya Kiprotestanti, kama ilivyoanzishwa na sheria? Je, utaiweka na kuhifadhi taasisi ya Kanisa la Kianglikani isiyoweza kukiukwa, na mafundisho, ibada, nidhamu na serikali yake, kama ilivyoanzishwa na sheria nchini Uingereza?” Kisha mfalme alikuwa Kiapo cha Azimio la Kuafiki (Accession Declaration Oath).

Afla ya Kusisimua kwa kutawazwa kwa Mfalme Charles III
Afla ya Kusisimua kwa kutawazwa kwa Mfalme Charles III

Mfalme Charles III hivi karibuni alikuwa ametangaza kwamba atakula kiapo hicho kama mshiriki aliyejitolea na aliyejitolea kikamilifu wa Kanisa la Kianglikani. Pia alisema kwamba wakati wajibu huu adhimu ni wajibu wake wa kikatiba, ana majukumu mengine pia, ambayo hayajaoneshwa kwa makini lakini yanafanywa kwa uaminifu sawa. Alieleza kuwa ni wajibu kudumisha utumiaji wa uhuru wa dini nchini Uingereza na kukubalika kwa watu wa imani nyingine za kidini na imani zote. Mojawapo ya mambo mapya muhimu ya kutawazwa huku ni kwamba mfalme amesali hadharani, ili kila mtu amsikie. Sala hiyo ilifanywa  mara baada ya kiapo. Mfalme alisali  hivi: “Nijalie niwe baraka kwa watoto wako wote, wa imani na imani zote, ili kwa pamoja tugundue njia za wema na kuongozwa katika njia za amani, kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu. Amina”. Ulifuata wimbo wa kwaya.

Watotot waliosindikiza Mfalme nyuma yake
Watotot waliosindikiza Mfalme nyuma yake

Kwa mujibu wa Kardinali Nocols alielezea kuwa katika kutawazwa huko, kwa hivyo, ugumu wa maisha ya Waingereza utapata usemi ulio wazi, katika historia yake, mila yake, mabadiliko yake ya kisasa na mabadiliko yake. Lakini ni usemi wa kina na mwaminifu wa imani na tumaini la Kikristo. Katikati yake ilikuwa ni sala, kutoka kwa mfalme aliye kimya mbele ya altare  ya juu kwenye ufunguzi, iliyowekwa hapo ili kutoa maelezo ya shauku  ya Mfalme Charles III  ya kuweka wazi kwamba uaminifu wake wa kwanza ni kwa Mungu, kwa maombi ya hadhara na alisoma na kisha upako wa Mafuta matakatifu na maadhimisho ya Ushirika Mtakatifu.  Kwa yyote aliyeudhuria kwa hakika hakuwa na shaka kwamba imani na tumaini la Kikristo ndio msingi wa maisha yetu. Kardinali Nicols alisema kwamba walimwambia kuwa ukiondoa mji wa Vatican, kuna nchi nyingine moja tu ulimwenguni ambayo kuapishwa kwa mkuu wa nchi hiyo hufanyika kwa sherehe ya kidini. Kwa upande wao utamaduni wa kizamani ambao unachangia kwa uthabiti hisia ya utambulisho na mwendelezo wa jamii hii ngumu ya kisasa na kwa yote tunayoleta ulimwenguni kwa jumla. Kwa kuhitmisha alisema Mungu mfalme Mfalme Charles.

 

06 May 2023, 12:39