Tafuta

Taasisi ya Kimataifa ya Uchunguzi wa matukio na matukio ya mafumbo maalumu  kama ya Maria imezaliwa rasmi siku chache zilizopita. Taasisi ya Kimataifa ya Uchunguzi wa matukio na matukio ya mafumbo maalumu kama ya Maria imezaliwa rasmi siku chache zilizopita. 

Uchunguzi juu ya maonesho ya Maria,malengo&kazi za kudhibiti maono ya uwongo

Nidhamu nyingi,ulinzi wa wadhaifu zaidi na mafunzo,ndiyo yalikuwa katika miongozo ya chombo kipya kilichoundwa na Chuo cha Kipapa cha Maria na kilichowasilishwa tarehe 3 Mei 2023 mjini Roma.Kusudi kuu ni kukusanya data kutoka ulimwenguni na kushirikisha mafunzo hayo.Sr.Daniela:wenye maono ya kweli ni watu rahisi na hawataki pesa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kutoa usaidizi wa kitaaluma wa taaluma mbalimbali unaohusisha taalimungu, elimu ya Maria, mawasiliano, dawa na sheria, kufunda wahudumu wa kichungaji na ulimwengu wa vyombo vya habari na zaidi ya  yote, kujiweka katika huduma ya watu dhaifu zaidi ambao wanaweza kudanganywa kwa urahisi zaidi. Haya ndiyo malengo ya Taasisi ya Kimataifa ya Uchunguzi wa matukio na matukio ya mafumbo maalumu  iliyozaliwa rasmi siku chache zilizopita ndani ya Taasisi ya Kipapa la Elimu ya Maria Kimataifa ambayo ofisi yake iko Roma  na kuwasilishwa rasmi tarehe 3 Mei 2023. Chuo cha Kipapa cha Maria kwa hiyo kimeunda  kituo kipya cha uchunguzi wa matukio ya mafumbo yanayohusiana na Bikira Maria ili kuweza kusaidia kwa hakika kuunda maarifa muhimu juu yake, kwa kuondoa dhana potofu ambazo zinazidi kuibuka kila kuchao.


Nchini Italia pekee, kiukweli, katika miongo ya hivi karibuni kumekuwa na maelfu ya watu ambao wameripoti kuwa na ufunuo wa kibinafsi kutoka kwa mama  Maria, lakini ni wachache tu kati ya hao ambao wametambuliwa na Kanisa. Kwa maana hiyo  engo la kuu ni kusaidia kuunda ujuzi muhimu  alieleza  Sr. Daniela Del Gaudio, mkurugenzi wa Kamati ya Uongozi wa Uchunguzi.  Kwa mujibu wake alisema “wakati Mama Yetu  anapoonekana, anaboresha maisha yetu ya Kikristo, lakini pia kuna ibada maarufu ambayo zimezaliwa kwa msingi usio sahihi, ambazo wapo wengi wanaokwenda  nyuma ya imani hizo za uwongo na sio za msingi wa kibiblia na kikanisa”.

Kulinda na kutetea walio wadhaifu

Sr. Del Gaudio  kwa hiyo alisisitiza kwamba: “Watu lazima walindwe dhidi ya udanganyifu, ulaghai na hata jaribio la wizi kwa sababu wakati mwingine anayejifanya kuona yaani  mwongo kwa kisingizio cha kutoa ujumbe kutoka kwa Mama yetu au kutoka kwa Mungu anaweza kuwadanganya watu na kuwashawishi”, kwa hiyo tunataka kujenga ufahamu huu muhimu, pia kwa waamini walei, sio tu kwa wachungaji na mapadre ili kila mtu aweze kuwa na uhuru wa kweli katika kujua jinsi ya kupambanua ukweli kutoka katika maonesho hayo ya uongo”. Kwa kufafanua zaidi alisema kwa “kawaida wenye maono ni watu rahisi, wanyenyekevu kwa sababu hiyo lazima kuwa na mawasiliano ya ujumbe vizuri zaidi. Mtu mzima au mtu mwenye utamaduni hufafanua zaidi kama mtoto mdogo ambaye anakuwa hajuhi chochote(tabula rasa)”.

Na zaidi “unachomwambia, anarudia na hii ni hakikisho la ukweli, alilisisitiza tena, akikumbusha mfano wa Mtakatifu Bernadette huko Lourdes.  Sr alisisitiza, akikumbuka pia kwamba: “Hata kama kuna faida, mtu anaweza kushuku ukweli wake, Watakatifu walipokuwa wakizidisha chakula, walifanya hivyo wakati wa njaa la  hitaji kubwa na zaidi ya yote walifanya hivyo kwa unyenyekevu mkubwa, wakistaajabia wema wa Mungu aliyeingilia kati kwa njia hiyo isiyo ya kawaida”. Katika muktadha huo, mchango wa mchunguzi kwa mujibu wa  mkurugenzi wa Kamati ya Kisayansi, “ni kwa ajili ya utafiti na uchambuzi wa kiutamaduni na mafunzo na haukusudii kwa njia yoyote kuchukua nafasi ya Tume ya Jimbo  na Askofu, ambao wana jukumu la uchapishaji wa hitimisho la mwisho. Ukweli unakuja  haraka na mara nyingi sio sahihi kuongeza matukio haya sana kwenye vyombo vya habari, lakini utafutaji lazima ufanyike kwa utulivu na usalama.

Mipango ya siku zijazo

Wajumbe wa Uchunguzi, chini ya uenyekiti wa Mfranciskani Padre Stefano Cecchin(Ofm), na rais wa Taasisi ya Kipapa Kimataifa ya mafunzo ya Maria(PAMI na ambapo wanashiriki Mafunzo ya Maria na Wataalamu wa mambo ya Maria watakusanya data na tafiti juu ya maonesho duniani kote, bila kupuuza matokeo ya kijamii, vyombo vya habari na kisayansi. Lengo kuu kwa huyo ni kuunda hifadhidata ya kimataifa na kuiweka katika vituo vya uchunguzi kwa ngazi ya kitaifa ili kuenea zaidi katika utafiti. Uchunguzi hautawasiliana na wanaodaiwa kuwa na maono moja kwa moja mradi tu uchunguzi wa tume ya jimbo unaendelea na watapokea nyenzo kutoka kwa jimbo hilo hilo kwa uchambuzi wao wa kina, ambaoo itawezekana kushauriana kwa njia ya mtandaoni. https://nemo.vaticannews.va/editor.html/content/vaticannews/sw/church/news/2023-04/taasisi-ya-kipapa-ya-maria-kuanzisha-kituo-cha-uchunguzi.html

Taaasisi mpya ya kudhibiti maono na matukio ya uongo kwa upande wa Mama Maria
05 May 2023, 15:13