Tafuta

Askofu Almachius Rweyongeza wa Jimbo Katoliki la Kayanga Tanzania Askofu Almachius Rweyongeza wa Jimbo Katoliki la Kayanga Tanzania 

Tanzania.Askofu Rweyongeza:Mlee mtoto kabla hajazaliwa,mtunze katika lishe na mifano bora

Mchungaji mwema ni mwalimu anayefundisha maadili bora,anamlinda mwanafunzi wake asipotee katika maovu ikiwemo ushoga na usagaji,ulevi,uzurulaji,magomvi,fitina,ufisadi na udanganyifu.Ni kwa mujibu wa Askofu Rweyongeza, Jimbo la Kayanga,katika Siku ya Kuombea Miito sanjari na maadhimisho ya Siku ya Mchungaji Mwema.

Na Patrick Tibanga, -Bukoba, Tanzania & Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, katika Ujumbe wake kwa Siku ya 60 ya Kuombea Miito Duniani, iliyoandhimishwa Dominika tarehe 30 Aprili 2023 anasisitiza kwa uthabiti huu  wa mabadiliko ya kukutana kati ya Mungu na mwanadamu, ambayo ndiyo kiini cha kile tunachomaanisha kwa neno “wito. Na anatusihi tugundue tena ukuu wa Mungu, kwa sababu ni  pale tu tunapotoa nafasi kwa ajili yake na wito wake, ndipo maisha yetu yanastawi na uhuru wetu unatambulika katika wema na ukweli. Baba Mtakatifu anafanya uchaguzi sahihi wa  kuanza kutoka kwa Mungu, kutoka katika neema yake, kutoka kwa baba na maombi yake yanayotuelekea sisi, kuja na kututafuta na kuzungumza nasi kama na marafiki" (Dei verbum, 2). Ni kutokana na  zawadi tu ya bure na ya ukarimu ya urafiki ambayo Bwana huja kukutana nasi ndipo kuna uwezekano wa kutekeleza utume katika maisha yetu, katika Kanisa, katika jamii na katika historia. Kwa ufupi, utume wetu hapa duniani unazaliwa kutokana na neema ya Mungu!

Miito hata kupitia mikutano ya vijana kimataifa
Miito hata kupitia mikutano ya vijana kimataifa

Baba Mtakatifu Francisko anakazia katika ujumbe wake kuwa wito ni zawadi na kazi, chanzo cha maisha mapya na furaha ya kweli. Sala na mipango ya uhuishaji inayohusishwa na Siku hii iimarishe usikivu wa kikazi katika familia zetu, katika jumuiya za parokia na zile za maisha ya wakfu, katika vyama na harakati za kikanisa. Roho wa Bwana mfufuka atusaidie kutoka katika  kutojali na atupatie  huruma na upole , tuishi kila siku tukiwa tumezaliwa upya kama watoto wa Upendo wa Mungu (rej. 1 Yoh 4:16) na kwa upande wetu tuwe wenye kuzaa katika upendo: wenye uwezo wa kuleta uzima, kila mahali hasa ambapo kuna kutengwa na unyonyaji, umaskini na kifo. Ili nafasi za upendo zipanuke na Mungu atawale zaidi na zaidi katika ulimwengu huu.

Miito ya kitawa na kikuhani
Miito ya kitawa na kikuhani

Ni katika muktadha huo wa Siku ya Kuombea miito, ambapo wazazi na walezi wametakiwa walee watoto katika maadili mema ya kumpendeza Mungu, na kupokea Sakramenti mbali mbali za Kanisa. Wito huo ulitolewa  Askofu Almachius Vincent Rweyongeza, wa Jimbo Katoliki la Kayanga Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Siku  hiyo  hiyo 60 ya  Kuombea miito duniani,  sambamba na Siku ya Mchungaji mwema misa iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Peter Claver Bugene Jimbo la Kayanga Tanzania. Askofu Almachius katika mahubiri yake alliwataka wazazi kuonesha njia kwa watoto kwa "kupokea Sakramenti katika Kanisa, kumpenda mtoto kabla hajazaliwa, kumtunza na kumpatia maadili na lishe bora, jambo litakalomfanya kuwa mchungaji mwema kwa mtoto na familia yake na kuwahasa wazazi wawasaidie watoto kujongea miito Mitakatifu: “Mlee mtoto kabla hajazaliwa, mtunze katika lishe na mifano bora, na mchungaji mwema ni mwalimu anayefundisha maadili bora na anamlinda mwanafunzi wake asipotee katika maovu ikiwemo ushoga na usagaji, ulevi, uzurulaji, magomvi, fitina, ufisadi na udanganyifu .

Vijana wanaalikwa kuudhuria siku ya vijana huko Lisbon Ureno
Vijana wanaalikwa kuudhuria siku ya vijana huko Lisbon Ureno

Askofu Rweyongeza alitoa angalisho kwamba “Wazazi muwaruhusu watoto kuchagua wito wao na kamwe msiwazuie, na wazazi ambao hamjafunga ndoa mfunge ndoa ili mtoto aweze kunuka harufu yako,  na unapokwenda kupokea Sakramenti aweze kuona. Na wakati huo huo  ujiulize je wewe ni mchungaji mwema yaani ni kiongozi na dira au ni kiongozi mbaya? Kwa hiyo Askofu pia alisema kuwa: “Tuwaombee viongozi wabaya waliopo katika dini, siasa, jamii, Kanisa na jamii wanaotetea uovu.” Alisema Askofu Almachius. Akiendelea aidha alieleza masikitiko yake  na  "wachungaji wanaoibuka na kutoa ahadi za uongo kwa waamini na kuwashauri hasa  waamini kuisikiliza vyema sauti ya mchungaji mwema na kwamba Mchungaji mwema ni mlango huru kwa kondoo anayelindwa dhidi ya wevi na mafundisho ya uongo na kamwe wasipotee katika magomvi, ufisadi, ulevi, fitina na ushoga.

Miito mbali mbali
Miito mbali mbali

“Sifa ya Kondoo ni kuisikia sauti ya mchungaji wake, kutambua na kuijua sauti ya mchungaji wake  na ili kuwepo na ufanisi kunahitajika mawasiliano kati ya mchungaji na kondoo na kwamba kondoo ana jukumu la kuisikia sauti, kujifunza na kuitikia sauti ya mchungaji iliyochangamana na mwangwi, hivyo konoddo wanatakiwa kuisikia na kuitofautisha sauti nyingine pamoja  na kuitikia sauti hiyo ambayo inasikika kwa neno Pendaneni sio wachungaji tuu wanaoibuka na kuua watu na kuwachapa viboko, alisisitiza  Askofu Rweyongeza.

Vijana wanaitwa na Bwana
Vijana wanaitwa na Bwana

Mchungaji mwema ni mlango huru kwa kondoo na kondoo huyo anatakiwa kulindwa dhidi ya wevi na mafundisho ya uongo", alsema Askofu Rweyongeza na kuwataka wote wanaoishi uchumba sugu kubariki ndoa zao na kutamatisha. "Mtoto wa nyoka ni nyoka, kama wewe mzazi haupokei Sakramenti, haukomuniki, hauungami mtoto unamnyonyesha sumu, hapo hujawa Mchungaji mwema, kwa sababu hapo unadhani mtoto atakuwa bora kiimani hata kama amebatizwa?”  aliuliza, na hivyo   aliongeza: “Ninaomba wazazi mzingatie hilo funga ndoa ili mtoto aone unayaishi maisha ya Sakramenti naye ananukia harufu yako ya matendo mema," alihimisha Askofu Rweyongeza mahubiri yake.

Kuitikia wito mtakatifu
Kuitikia wito mtakatifu
Askofu Rweyongeza:wazazi msiwazuie vijana kuchagua wito wao
04 May 2023, 17:00