Mwenyekiti wa Jumuiya ya Yohane XXIII atoa shukrani kwa Rais Mattarella kwa zawadi ya Tuzo
Na Angella Rwezauka, - Vatican.
Tarehe 29 Mei 2023 Papa Francisko alitoa Tuzo ya Paulo VI kwa Rais wa Jamhuri ya Italia na kukumbuka mwaliko wa Papa Montini wa kuwajibika kwa manufaa ya wote kwamba "tunahitaji kwenda kinyume na mawimbi ya ulimwengu kuhusiana na hali ya kushindwa na malalamiko, kuhisi mahitaji ya wengine kama vile ya kwetu". Na wakatii huo huo Mkuu wa nchi ya Italia alipenda kuchangia jumla hiyo ya Tuzo yake kwa Jumuiya ya Yohane XXIII, iliyoanzishwa na Padre Oreste Benzi na ambayo huko Emilia Romagna ina makazi yaliyoathiriwa sana na mafuriko ya siku za hivi karibuni. Kutokana na fursa hiyo, Rais mpya wa Jumuiya ya Papa Yohane wa XXIII, Matteo Fadda ameandika barua ta kuelezea hisia zao za heshima na shukrani kwa Rais Mattarella kwa kuamua kutoa Tuzo la Paulo VI kwa nyumba zao zilizoathiriwa na mafuriko huko Emilia Romagna, ardhi ambayo Jumuiya yao ipo na ambapo wanayo mamia ya vifaa vya mapokezi.
Utoaji wa Zawadi ya ajabu
Rais Mpya wa Jumuiya ya Yohane XXIII kwa hiyo alisema: tunamshukuru kwa utoaji wa zawadi ya ajabu kwa watu wengi maskini na walemavu sana tunaowakaribisha na ambao sasa wamehamishwa. Tunakumbuka ziara yake ya Rimini kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya chama chetu, alipotembelea nyumba moja ya familia yetu, aliona makazi duni ya mwanzilishi wetu Padre Oreste Benzi na kukutana na watu wengi tuliowakaribisha, wakiwemo wasichana walioachiliwa kutoka katika utumwa wa biashara haramu ya binadamu.” Kwa hiyo rais mpya wa Jumuiya ya Papa Yohane XXIII, aliyechaguliwa hivi karibuni tarehe 28 Mei 2023 huko Rimini, alitangaza kuhusu uamuzi wa Rais Mattarella wa kuchangia jumla ya tuzo ya Paul VI ambayo alipokea mjini Vatican kutoka kwa mikononi mwa Papa Francisko "kama upendo kwa Kanisa kwa Jumuiya ya Papa Yohane XXIII, ambaye miundo yake iliathiriwa na mafuriko huko Mkoa wa Emilia-Romagna Italia ambao umesababisha hata vifo, licha ya uharibifu wa mashamba na nyumba nyingi.