Taasisi ya Kipapa ya Maria kuanzisha kituo cha uchunguzi wa mafumbo ya Maria
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ilianzishwa katika Taasisi ya Kipapa Kimataifa ya mafunzo ya (PAMI) Uchunguzi wa matukio na majabu ya mfumbo yanayohusiana na sura ya Bikira Maria ulimwenguni kwa lengo la kuchambua na kutafsiri matukio mbalimbali ya Mama Maria (Mariophanies) yaani kutokea, machozi, lakini pia maeneo ya ndani, kama vile unyanyapaa na matukio mengine ya fumbo ambayo yanaendelea au tayari yalitokea, lakini ambayo bado yanasubiriwa kutolewa tangazo kutoka kwa mamlaka ya kikanisa kuhusu uhalisi.
Msaada kwa masomo na usambazaji
Padre Stefano Cecchin(Ofm),rais wa Taasisi hiyo PAMI ameeleza kwamba lengo walilojiwekea ni kutoa msaada kamili kwa ajili ya utafiti, uthibitishaji na ufichuaji sahihi wa matukio hayo, ambayo siku zote huendana na mafundisho ya kikanisa, mamlaka husika na kanuni kwa unaglizi wa Vatican juu ya mafundisho hayo. Mwangalizi atafanya kazi kwa utaratibu, kimkakati, taaluma mbalimbali na namna iliyohitimu, pia kwa ushirikiano na wataalam na watafiti, watu wa juu katika uwanja wa sayansi na mamlaka ya kikanisa. Ni muhimu kufafanua, kwa sababu ujumbe unaodaiwa mara nyingi huleta mkanganyiko, hueneza matukio ya siku ya mwisho yenye wasiwasi au hata shutuma dhidi ya Papa na Kanisa. Je, ni jinsi gani Mama Maria, Mama wa Kanisa, angeweza kudhoofisha uadilifu wake au kupanda hofu na upinzani, yeye ambaye ni Mama wa Huruma na Malkia wa Amani? Vivyo hivyo, ni muhimu kutoa msaada wa mafunzo kwa sababu kushughulikia kesi fulani kunahitaji maandalizi ya kutosha, alifafanua zaidi.
Tume za kitaifa na kimataifa
Kamati za kisayansi mahalia pia zitaundwa hivi karibuni, katika mantiki ya mtandao wa uendeshaji wenye uwezo wa kupanua wigo wa hatua. Mwangalizi ambaye anaanza rasmi shughuli zake katika kikao cha kwanza ambacho kitafanyika Jumamosi tarehe 15 Aprili 2023 katika makao makuu ya Tasisi hiyo PAMI Roma , mahali ambapo atafanyia kazi kwa kawaida, pia ataweza kukutana na kufanya kazi katika kambi hiyo kulingana na mahitaji au maombi ya usaidizi.
Kukuza upyaisho na kujifunza matukio ya ajabu
Madhumuni ya uangalizi kwa mujibu wa maelezo ya rais ni kutenda kwa ufanisi na kwa njia nzuri ya kuamsha tume za kitaifa na kimataifa za kutathmini na kujifunza matukio ya ajabu na matukio yaliyoripotiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia, ili kukuza upyaisho na mafunzo katika shughuli za aina hiyo ya matukio na maana zake nyingi za kiroho na kiutamaduni, ambazo zinakuza shughuli za kiwango cha juu za usambazaji na ushauri, hasa katika huduma ya Makanisa na Maaskofu wa mahali hapo, lakini pia shughuli za utafiti wa kinidhamu kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma, za walei na za kikanisa na uchapishaji wa matokeo ya tafiti zilizofanywa.