Papa,Hungaria,Padre Fabry:Kuna maelfu ya vijana wanaotaka kukutana na Papa
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Tunajitahidi kuandaa vyema ziara hii, katika roho ya urafiki na maombi. Hayo yamesemwa katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican na Padre Kornél Fábry, mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Kichungaji ya Hungaria, na katibu mkuu wa zamani wa Sekretarieti ya Kongamano la 52 la Ekaristi Takatifu lililofanyika huko Hungaria mnamo Septemba 2021. Katika mahojiano hayo kwenye fursa ya Ziara ya Kitume ya 41 ya Papa Francisko katika nchi hiyo amesisitiza kuwa Papa katika ziara hiyo sio kama ya kufunga Kongamano la Kimataifa la Ekaristi, kwa sababu hatakutana na maaskofu na viongozi wa kidini pekee, lakini pia mapadre, waseminari, na wale wanaoshirikiana katika parokia”. Na zaidi hasa, mkutano na vijana utakuwa katika uwanja wenye viti zaidi ya 10,000, kisha mabembelezo yake yatawafikia walemavu, na wakimbizi. Katika hilo amewafikiria zaidi ya Waukraine, kwa sababu zaidi ya milioni moja wamepitia Hungari mnamo mwaka 2022.
Swalijingine ni kuhusu vijana na zaidi uchungaji wa vijana katika chuo kikuu cha Hungaria na ambacho kilikuwa kimepigwa marufuku wakati wa ukomunisti. Kwa hiyo sasa vijana wanajiandaa namna gani kumpokea Papa. Tayari inaonekana idadi kubwa ya maombi ya mkutano kwenye uwanja huo, na wanaona kuwa ni kubwa kuliko viti vilivyopo, sawa na 11, 000. Vijana wengi watatoka katika parokia, lakini pia kutoka vyuo vikuu, sio tu vya Kikatoliki bali na visivyo katoliki. Papa atakuwa na mikutano miwili nao kwanza vijana katika uwanja wa michezo na siku ya mwisho, ulimwengu wa utamaduni na vyuo vikuu. Kuna vijana wengi wanaotaka kusali pamoja na Papa Francisko, na wanajiandaa kwa mkutano huu huku wakisoma waraka wa Christus vivit, wa kitume ambao Papa aliwaandikia vijana.
Katika nembo ya safari hiyo ya kitume kuna daraja, ishara ya Budapest. Daraja linaunganisha, linatengeneza mazungumzo na huu ndio mwaliko ambao Papa ametoa kwa vijana na wazee. Mazungumzo kati ya vizazi, kwa kuheshimiana, yalihimiza hasa katika mzunguko wa katekesi ambayo Papa Francisko aliiweka kwa wazee mwaka 2022. Katika uchungaji kuna umuhimu gani kuukubali mwaliko huo, pia kupinga utamaduni wa kutupa?
Padre, alijibu kuwa “Hili ni jambo muhimu sana kwetu. Huko Hungari, familia haziishi tena pamoja, vizazi tofauti viliishi pamoja. Huko mashambani kuna nyumba kubwa, ambazo waliishi wote pamoja. Leo hii ni nadra sana. Pamoja na hayo, katika makanisa yetu tunahimiza mazungumzo kati ya vijana na wazee, kwa mfano katika liturujia. Hata kwa nyimbo za kisasa zaidi, zenye kusikilizana. Huu ni wajibu wa kichungaji: kukuza umoja kati ya vijana na wazee. Katika parokia nilipokuwa hapo awali, kila sherehe ilikuwa ya familia, ikiwa ni pamoja na babu na babu. Kuwasikiliza, kuwakaribisha ni muhimu, ni watu wetu wenye busara! Katika wakati wetu, ambapo ulimwengu wa mtandao unaonekana kuwa mbali sana na wale walio wazee, mara nyingi mimi hutazama jinsi wajukuu wanavyowafundisha babu na nyanya zao jinsi ya kutumia mazungumzo, Intaneti. Hii ni nzuri, tunasonga mbele pamoja”.
Huduma ya kichungaji ya huduma ya afya pia ni muhimu kwa ushirikishwaji wa kweli. Je, ni kawaida kiasi gani huko Hungaria? Padre alisema kwamba Wengi sana, kuna mapadre wanaohusika, kwa mfano katika jimbo kuu la Budapest, kusaidia vipofu kushiriki katika liturujia. Nadhani ni muhimu sana kuandaa matukio maalum, kujumuisha. Ninafikiria Misa zilizoundwa mahsusi kwa walemavu, ni utajiri wa Kanisa. Mkutano ambao Papa atafanya na watoto hawa ni muhimu sana, itakuwa wakati wa faragha na watoto hawa, pamoja na wazazi wao. Askofu wa Roma anataka kutumia muda pamoja nao, ili kuwatia moyo.”