Tafuta

2023.04.03 Tanzania: Makanisa mbalimbali duniani Tanzania na ulimwengu wote wameadhimisha Dominika ya Matawi. 2023.04.03 Tanzania: Makanisa mbalimbali duniani Tanzania na ulimwengu wote wameadhimisha Dominika ya Matawi. 

Mwanzo wa Juma Takatifu:Ushindi wa Kristo tayari unajionesha kwa Hosana aliye Juu!

Tumeanza Juma Kuu Takatifu linalofunguliwa na Dominika ya Matawi.Katika siku hii kwa Maneno ya Hosana yanaonesha kuwa ni ushindi wa Kristo ambao tayari anaingia kifalme katika maisha ya mwanadamu.Hosana kwa aliye juu kabisa inabubujika kutoka katika mioyo ya wale ambao wameelewa kuwa Kristo pekee ndiye anayeweza kuleta wokovu wa kweli,ule ambao hauzingatii zana na mafaniko bali ule unaotajirishwa na ustawi wa kiroho.Kanisa lote la ulimwengu limesheherekea Siku ya Matawi.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Dominika tarehe 2 Aprili 2023 ilikuwa ni mwanzo wa Juma Kuu Takatifu ambalo kiutamaduni katika Liturujia linaitwa Dominika ya Matawi,ambapo ni Mwanzo wa Mateso ya Bwana, kwa sababu ni ukumbusho wa siku ya kuingia kwake Yesu Kristo jijini Yerusalemu ili kukamilisha Fumbo lake la Pasaka! Hili ni jambo ambalo linaonesha umuhimu wake ambapo, tangu nyakati za kale, Injili mbili husomwa, kabla ya kuanza maandamano na baada ya masomo ambapo husomwa historia ndefu  ya mateso ya Bwana katika misa hiyo. Ni suala ambalo pia litarudia katika Siku ya Ijumaa Kuu Takatifu. Kuhusiana na sherehe hii, Baba Mtakatifu Francisko aliwahi kueleza kwamba: “sherehe hii ina ladha mbili, tamu na chungu: ndani yake tunasherehekea Bwana, anayeingia Yerusalemu kwa sifa, na wakati huo huo, historia ya Kiinjili ya Mateso yake inatangazwa. Hii ndiyo sababu mioyo yetu inahisi utofauti huo wa kuhuzunisha na kuhisi kwa kiasi kidogo kile ambacho Yesu lazima alihisi moyoni mwake siku hiyo, siku ambayo alifurahi pamoja na marafiki zake na kulilia Yerusalemu” (Mahubiri ya Papa Francisko,Dominika ya Matawi 2017).

Askofu wa Sumbawanga nchini Tanzania akibariki matawi 2 Aprili 2023
Askofu wa Sumbawanga nchini Tanzania akibariki matawi 2 Aprili 2023

Hata  Papa  Benedikto XVI, katika kitabu chenye kichwa: “Yesu wa Nazareti; Kuingia Yerusalemu hadi ufufuko" aliandika kuwa: “Kifungu cha Kuingia kwa ushindi kina umuhimu sana wa matejeo ya ajabu. Kama  Bwana alivyoingia katika mji mtakatifu akiwa amepanda punda, vivyo hivyo Kanisa lilimwona akifika kila mara tena chini ya mwonekano wa unyenyekevu wa mkate na divai”. Kwa njia hiyo tunaweza kukazia fikira zetu kwenye vifungu mbalimbali vya Injili na maandiko mengine matakatifu ya Biblia. Kwa upande mmoja, Yesu alishuka kutoka kwenye Mlima wa Mizeituni kando ya Bethfage na Bethania, ambako Masiha alitarajiwa kuingia. Akiwa na maandalizi hususan kuhusu mwana-punda, Yesu alitumia haki ya wafalme kuomba kwa ajili ya matumizi ya kibinafsi.

Waamini katika maadhimisho ya Dominika ya Matawi nchini Tanzania
Waamini katika maadhimisho ya Dominika ya Matawi nchini Tanzania

Daudi aliamuru kwamba mwanawe Sulemani apandishwe juu ya nyumbu wake na kuchukuliwa kuwa mfalme aliyetiwa mafuta (1 Wafalme 1:33). Punda alikuwa amefungwa, kama Yakobo alivyosema kuwa Yuda angefanya kuwa wake mwenyewe (Mwanzo 49:11). Kwa upande mwingine, watu walitandaza nguo zao katika njia ya Yesu, kama wakazi wa Yerusalemu walivyokuwa wakifanya nyakati za kale kwa heshima ya wafalme (2 Wafalme 9, 13). Na umati, ukiwa umejawa na furaha na shangwe, walianza kumwimbia Yesu (Zaburi 118: “Abarikiwe Mfalme, ajaye kwa jina la Bwana!”. Pia walisema: “amani na utukufu juu mbinguni,” maneno ambayo yanatukumbusha hata  wimbo wa Malaika, wakati Yesu alipozaliwa  huko Bethlehemu ( Lk 2:14), katika mji wa Mfalme Daudi na  wa Masiha.

Hosana Juu mbinguni 2 prili 2023 Dominika ya Matawi
Hosana Juu mbinguni 2 prili 2023 Dominika ya Matawi

Mantiki hii ya  kimasiha ya kile ambacho kilikuwa kinaanza kutokea hakikuepuka kuonekana kwa Mafarisayo, ambao, kwa kashfa, walimwomba Yesu awakemee wanafunzi wake walichokuwa wakiimba na kutukuza. Lakini kwa bahati nzuri Bwana alisisitiza ugumu wa mioyo yao.  Hizi zilikuwa ni ishara za Masiha zilizokuwa  wazi kabisa na kwa hiyo  hata mawe yangepiga kelele kwa heshima yake ikiwa angefaulu kuwanyamazisha wanafunzi, kama alivyothibitisha Bwana mwenyewe. Na vile vile kama mmoja wa mababa wa Kanisa anavyoeleza vema kwamba: “Baada ya kusulubishwa kwa Bwana, walipoona wale waliomjua hawakufungua vinywa vyao kwa sababu walikuwa wamejawa na woga, mawe yalimsifu, kwa sababu, alipokwisha kufa nchi ikatikisika, mawe kati yao yakapasuka na makaburi yakafunguka”(Rej. Mtakatifu Beda). Kwa hivyo tukio la Dominika ya Matawi  inarudiwa kwa namna fulani katika maisha yetu wenyewe. Yesu anaukaribia mji wa roho zetu akiendesha mambo ye tu ya kila siku, kupitia unyofu wa sakramenti au kwa mapendekezo muhimu, kama yale ambai tunapaswa kuishi utimilifu wa wajibu wetu kwa usahihi; kutabasamu kwa ajili ya wanaohitaji, kwa kuwsaidia chochote hata ikiwa roho yetu inateseka.

Maandamano ya kuingia Kanisani katika Siku ya Matawi
Maandamano ya kuingia Kanisani katika Siku ya Matawi

Kwa hiyo tunapaswa kutoa wakati unaofaa kila wakati na hasa kwa siku hizi kwa ajili ya maombi, bila kukata  na kwenda kukutana na wale wanaotafuta msaada wetu. Ni jambo la muhimu kutena haki kwa ajili ya kujitajirishwa neema ya upendo. Ni kwa kadiri tunavyowafikia wenye kuhitaji, ndipo upendo wa Mungu ulipo, na ambao wameutuhimiza. Juma hili Tkatifu kwa maana hiyo tutatafaka ni nani anaweza kuwa punda, maana kuna mamia elfu na mamilioni ya wanyama ambao ni wazuri zaidi, wenye akili zaidi lakini pia hata wakatili zaidi. Yesu hakuchagua wale ambao ni wazuri sana na wenye sifa bali wale wanyenyekevu, ina ndiye punda. Bwana anathamini furaha ya moyo punda mchanga, hatua rahisi, sauti isiyo na adabu, macho safi, sikio la uangalifu kwa neno lake la upendo. Hivyo hutawala katika nafsi. Yeyote anayempokea Yesu kwa unyenyekevu na urahisi basi anaweza kumpeleka popote. Mpango wa mahubiri ya Yesu uko mbali na kiwango cha ufahamu wa mwanadamu, kwa sababu umewekwa katika mantiki tofauti kabisa, inayofungua kwa wokovu, kwa uzima wa milele, kwa uhakika wa furaha katika hali yoyote ya maisha ambayo mtu anajikuta. Sio utajiri na mafanikio ambayo hutoa amani ya moyo, lakini upendo wa Mungu, kukumbatia kwa Baba, faraja katika uchovu, utulivu wa ndani.

Askofu akibariki Matawi kabla ya kuanza maandamano
Askofu akibariki Matawi kabla ya kuanza maandamano

Katika siku hii  na mwanzo huu wa Juma takatifu tuone kwamba huu ni ushindi wa Kristo,na huku ndiko kuingia kwa kifalme katika maisha ya mwanadamu, Hosana katika mbingu ya juu kabisa inayobubujika kutoka katika mioyo ya wale ambao wameelewa kuwa Kristo pekee ndiye anayeweza kuleta wokovu wa kweli, ule ambao hauzingatii zana, hali njema, lakini ambayo inatajirishwa na ustawi wa kiroho. Si wakati huo tu, wakati wa Yesu, lakini pia leo hii ni vigumu sana kukubali ujumbe huuo, ili kuufanya maisha yetu, yawe sababu ya  utajiri unaonekana kwa mungu pekee wa kweli badala ya  kuabudu sanamu, au picha ya kujifafanua mafanikio tu. Haijalishi malengo haya yanasababisha mateso kiasi gani katika maisha ya mwanadamu, haijalishi kwamba ili kupata utajiri na mafanikio mwanadamu analazimishwa katika ishara na tabia zisizokubalika! Kilicho muhimu ni kufikia lengo, ambalo kwa bahati mbaya ni lengo la kifo, ambalo huleta huzuni na uchungu.

Shangilio la Bwana anayeingia mji wa Yerusalemu siku sita kabla ya mateso ya Bwana
Shangilio la Bwana anayeingia mji wa Yerusalemu siku sita kabla ya mateso ya Bwana

Katika siku hii ya kuadhimisha, mafumbo hayao ambayo liturujia inatuonesha kuingia kwa Yesu Yerusalemu kwa ushindi,ni muhimu sisi sote tufurahi na kumsifu Bwana kwa sababu saa ya wokovu imekaribia, saa ambayo tutakuwa na uhakika kwamba hakuna tena kitakachoweza kutuangusha, ambapo uovu hautaweza kuchukua uwepo wetu. Hata hivyo, tunapaswa kujihakikishia kwamba ustawi ambao Baba anatupatia si wa kimwili, bali ni furaha moyoni, uhakika wa upendo hata katikati ya matatizo ya kila siku na kushindwa duniani kwetu. Kwa ufahamu tutaweza kuishi Pasaka kwa shukrani na hisia kwa sababu tutaweza kupata ujasiri wa kuachana na mashaka yote katika Mungu Baba na kujua jinsi ya kukumbatia maisha na wepesi wa upendo wa Aliyefufuka. Kwani "Ni mtamu kiasi gani kusimama mbele ya msalaba, au kupiga magoti mbele ya Sakramenti Takatifu, na kuwa tu mbele ya macho yake”, alisema Papa Francisko katika Waraka wake wa Evangelii gaudium, n. 264). Ndugu msomaji tujiandae vema katika Juma Kuu Takatifu.

Tafakari ya Kard. Cantalamessa
Tafakari ya Kard. Cantalamessa ya mwisho ya kipinid cha kwaresima
03 April 2023, 13:54