Tafuta

Maandamamo ya kupinga Dikri ya Cutro katika Bunge inayohusu kuondoa ulinzi na usalama kwa wahamiaji wanaofika. Maandamamo ya kupinga Dikri ya Cutro katika Bunge inayohusu kuondoa ulinzi na usalama kwa wahamiaji wanaofika.  (ANSA)

Jumuiya Mt.Egidio/Makanisa ya Kiinjili:Okoa ulinzi maalum&kuza ufungamano

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili wamezindua wito kwa Serikali na Bunge:“kuokoa ulinzi maalum na kukuza fungamanishaji,”kufuatia na kile kiitwacho “Cutro decree”,yaani tamko la Cutro inayotaka kuondoa ulinzi maalum kwa ajili ya wahamiaji,Italia.

Na Angella Rwezaula, -Vatican.

Mbele ya kukabiliwa na hatua za kutekeleza kuhusu suala la uhamiaji, ambao sasa umekuja katika uchunguzi wa Bunge nchini Italia, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili nchini Italia, ambayo yamekuwa yakifuatilia jambo hilo kwa miaka mingi na kutoa majibu thabiti, kama vile Mikondo ya kibinadamu  iliyojaribiwa sasa, wanaeleza wasiwasi wao wote na kuzindua wito kwa Serikali na Bunge. Wito wao unaongozwa kichwa “kuokoa ulinzi maalum na kukuza fungamanisho”. Katika wito wao vyombo hivi vimeandika kwa pamoja wito wao kuwa “Kifurushi cha sheria mpya zinazokusudiwa kitaendesha hatari ya kudhoofisha mtindo ambao, ingawa kati ya taa na vivuli, imewezesha kulinda haki za msingi, kuhakikisha michakato halisi ya ujumuishaji na kuwa na matukio ya ukiukwaji na ukengeushi. Kwa namna ya pekee inahitajika kufikiria tena matokeo ambayoo kizuizi kinachojulikana kama ulinzi maalum kingekuwa nacho na  lazima kirudiwe,  sio kifungu cha Italia pekee kwa sababu kinatekelezwa, kwa njia tofauti, na nchi zingine nyingi za Umoja”.

Madhara ni makubwa kwa wanaoomba ulinzi

Jumuya ya Mtakatifu Egidio na Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili wanaandika: “Madhara makubwa yatakuwa kwanza kabisa kwa watu wanaoomba. Kiukweli, hawataweza kulindwa tena ikiwa katika hatari ya kutendewa kikatili katika nchi zao za asili, wala hawatapata utunzaji muhimu zaidi kwa ajili ya maisha yao, wala hawatakuwa na uwezekano wa kukaribishwa wanapokimbia majanga ya asili kama vile mafuriko na matetemeko ya ardhi”.  Kwa hiyo amethibisha “Inabidi kukumbuka kuwa hizi ni haki zilizohakikishwa na Katiba yetu, ambazo tume za majaji na mahakama hazitaweza kuzifumbia macho”. Hatimaye, kutobadilishwa kwa ulinzi maalum kuwa kibali cha makazi kwa sababu za kazi inaweza kupanua wasiwasi katika eneo la makosa (na kwa hiyo pia ya ukosefu wa usalama) kwa usahihi wakati ambapo nguvu zote za uzalishaji wa nchi zinaombwa kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa raia wa kigeni.

Kizuizi cha ulinzi maalum ni hatari

Huo ndio wito  ambao umejikita katika uzoefu madhubuti wa ushirikiano uliopatikana tangu 2016 kupitia 'ukanda wa kibinadamu': uzoefu unaozingatia uhalali, ambao umekuwa na utambuzi muhimu wa kitaasisi, na ambao unatumiwa kama mfano na nguvu zote za kisiasa, mwingi kama pamoja na upinzani. Hatari ya kizuizi cha ulinzi maalum ni ile ya kutoa athari kinyume na inayohitajika na kutangazwa, kwa kutopendelea au kukatiza njia hizo za ujumuishaji na 'uhamiaji mzuri' ambao nchi, pia kwa kuzingatia takwimu juu ya ajira, upungufu katika minyororo mbalimbali ya usambazaji, ambayo inahitaji sana.

Askofu Savino, Makamu Rais ( CEI)

Nina mashaka, kama raia na askofu, ninaposikia mazungumzo ya hali ya hatari na kuondolewa kwa ulinzi maalum. Nafikiri kwamba makabiliano ni muhimu kujaribu kutafuta suluhisho kwa masuala ya sera ya uhamiaji, kuweka kando chuki na mbinu za kiitikadi”, amesema hayo Askofu  Francesco Savino, wa Jimbo Katoliki la  Cassano Jonio na makamu rais wa Baraza la Maaskofu Italia ( CEI) katika siku ambayo  imepangwa kupigiwa  kura kwa kile  kinachojulikana kama “Cutro decree” kuhusu  wahamiaji. Askofu Savino alizungumza na Shirika la Habari za kidini la Baraza la Maaskofu Italia, (SIR), kando ya Kongamano la 43 la Caritas Kitaifa linaloendelea mjini Salerno kusini mwa Italia.  

Askofu Francesco Savino, wa Jimbo la Cassano ya Ionio huko Calabria na makamu wa CEI
Askofu Francesco Savino, wa Jimbo la Cassano ya Ionio huko Calabria na makamu wa CEI

Katika mkutano huo, alikuwa amerudia hata hivyo muda mfupi kabla kuwa “Caritas au Kanisa la Italia haliwezi kuwa kama jani la mtini kwa kuzingatia sera fulani zisizofaa. Tunataka kuaminisha michakato ya mabadiliko”. Katika marejeo ya masuala ya umaskini na uhamiaji kwamba: “Caritas daima imeshuhudia kanuni ya kampuni ndogo ambayo huongeza uhusiano kati ya makampuni, mashirika, vyama na taasisi za kisiasa alibainisha na hivyo alisisitiza kwamba anaamini Caritas lazima ifanye mazungumzo na taasisi za kisiasa kwa matumaini kwamba wasikilize sauti ya wale wanaoelewa mahitaji halisi na ya kweli katika vituo vya ushauri, na kuheshimu majukumu. Kamwe kama katika wakati huu mgumu na mgumu zaidi kwa kutembea pamoja, tunaweza kufikia matokeo makubwa zaidi kwa manufaa ya wote.

Wekeni kando chuki na kauli fulani

Askofu Savino alisema kuwa na uhakika kwamba wanaweza kugeuza uhamiaji kutoka katika shida kuwa rasilimali  na  zaidi ya yote aliposoma kwamba idadi kubwa ya wahamiaji wanaweza kupunguza deni la umma na anaposikia kwamba Confindustria na wajasiriamali, wana takwimu mikononi mwao kuomba rasilimali zaidi. Kwa hivyo, Askofu amethibitisha kwamba waweke kando chuki na kauli mbiu fulani na waepuke kuwa kwenye kampeni za uchaguzi kila mara kwa kufuata mitazamo ya watu wengi au kuwashwa matumbo.  Hata hivyo wabaoaswa kujua kwamba suala la uhamiaji sio rahisi kulisuluhisha.

Wito kutofikiria misingi ya upendeleo

Katika siku za mkasa wa Cutro, uliotokea hivi karibuni Pwani kusini mwa Italia, Askofu Savino alikuwa na la kusema kwa  niaba ya CEI na katika muktadha wa kifurushi cha sheria ya Bunge amesasisha mwaliko wake wa kutofikiria kwa msingi wa upendeleo, kauli mbiu au uelewa wa awali wa kiitikadi au kwa sababu tunapaswa kujibu matamanio fulani ya watu, tukiwaheshimu wale wanaofikiria tofauti kutoka kwetu”. Nadhani katika takwimu kubwa la majadiliano juu ya umaskini na uhamiaji tunaweza kusababisha chaguzi za kisiasa na kitaasisi zenye heshima zaidi. Pia kwa sababu, akimnukuu Mwansiasa maarufu aliyeuwawa Aldo Moro, kwamba "demokrasia inakua kwa kiwango ambacho kuna uhusiano wa usawa kati ya haki na wajibu wakati mara nyingi nina hisia kwamba haki fulani zinatengwa kila siku, kama kwa mfanohaki ya kuhama.” Katika Shule tulijifunza kwamba watu ni mchanganyiko wa watu tofauti. Suala si rahisi kutatua, kwa hakika hatuwezi kusema 'wahamiaji wote waje kwetu'. Kwa hiyo "Hii ndiyo sababu, ikiwa Ulaya ipo, lazima ipige pigo katika masuala haya. Nina hakika kwamba fursa kubwa ya kidemokrasia ni kuwafanya ndugu wahamiaji kuwa rasilimali badala ya kuwa shida. Kuhusu suala la uhamiaji tuko hatarini kwa ustaarabu wa upendo na demokrasia iliyokomaa zaidi.”

19 April 2023, 14:12