2023.04.23 Ziara ya Askofu Stephen Chow Sau-yan wa Hong Kong huko Beijin. 2023.04.23 Ziara ya Askofu Stephen Chow Sau-yan wa Hong Kong huko Beijin. 

Askofu wa Hong Kong:Safari ya Beijingi katika ishara ya umoja

Askofu Stephen Chow Sau-yan alihitimisha ziara ya siku tano mjini Beijing kwa mwaliko wa Askofu Mkuu Li Shan.Katika ziara hiyo alikutana na jumuiya ya Kikatoliki ya mji mkuu wa China.Madhumuni ya ziara hiyo ilikuwa kukuza ushirika kati ya Majimbo hayo mawili.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Askofu Stephen Chow Sau-yan wa Hong Kong, alihitimisha safari ya siku tano ya kwenda Beijing Ijumaa tarehe 21 Aprili 2023. Askofu huyo aliandamana na askofu msaidizi, Joseph Ha, na Padre Peter Choy, na katibu wake wa kibinafsi, mlei Wong Ka-chun. Ziara hiyo imefanyika kwa mwaliko wa Askofu Mkuu Joseph Li Shan wa Beijing. Siku ya kwanza, Jumatatu tarehe 17 Aprili, kulikukuwa na muda wa maombi ya pamoja uliofanyika katika Kanisa Kuu la Mwokozi Mtakatifu Zaidi (Beitang), pamoja na waamini kadhaa waliohudhuria. Picha ya Padre Mjesuit Matteo Ricci, mmisionari nchini China kati ya karne ya 16 na 17, ilikuwa imewekwa mbele ya Altare. Yeye aliyetangazwa kuwa mwenyeHeri mnamo Desemba 2022, alipendwa sana na Wakatoliki wa China. Papa Francisko alimfafanua kama mtu wa utamaduni wa kukutana, miongoni mwa watu wa kwanza kuanzisha daraja la urafiki kati ya China na Magharibi, kutekeleza mfano halali wa kueneza ujumbe wa Kikristo katika ulimwengu wa Kichina" (Hotuba ya 9 Mei  2022).

Ziara ya Askofu wa Hong Kongo huko Beijing China
Ziara ya Askofu wa Hong Kongo huko Beijing China

Siku ya Jumanne tarehe 18 Aprili 2023, Askofu  Chow alitembelea Seminari ya Kitaifa ya Kikatoliki, akaadhimisha Misa katika Kanisa la Mama Msafi wa Moyo  (Nantang) kisha akakutana na baadhi ya wawakilishi wa serikali. Na siku ya Alhamisi tarehe 20 Aprili aliadhimisha Misa na Askofu mkuu wa Beijing katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Mwokozi na Askofu Mkuu Li Shan aliongoza maadhimisho hayo. Na wakati huo huo , Askofu Chow alitoa mahubiri mafupi, ambapo alithibitisha kwamba Bwana Mfufuka alishinda kila kitu, hata kifo, akituweka huru kutoka katika hofu. Aliyefufuka aliwapa wanafunzi wake Roho Mtakatifu, ambayo ni zawadi ya Baba na Mwana katika ushirika wa upendo. Baba Mtakatifu Francisko – anahamaisha njia ya sinodi katika Kanisa, akiwaalika washiriki wote wa Kanisa kusikiliza kila mmoja na zaidi, kujifunza kumsikiliza Roho Mtakatifu anayetuongoza katika safari yetu. Roho Mtakatifu ni Mungu wa umoja si wa mgawanyiko. Kwa hiyo Askofu katika mahubiri hayo alihitimisha  kwamba ni matumaini kuwa majimbo ya Hong Kong, ya Beijing na jumuiya zote za Kikatoliki za bara zinaweza kudumisha ushirikiano wa kina zaidi na kubadilishana katika ushirika wa upendo na kuwaalika wamini wa Beijing kuwaombea.

Askofu wa Hong Kong pamoja na wa Beijing wakati wa misa ya pamoja
Askofu wa Hong Kong pamoja na wa Beijing wakati wa misa ya pamoja

Baada ya Misa hiyo Askofu huyo alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari nje ya Kanisa Kuu. Kama ilivyoripotiwa na magazeti mbalimbali, Askofu  Chow alisisitiza umuhimu wa kupenda nchi na Kanisa. “Sote tunataka nchi yetu iende vizuri, kuwa wazalendo ni jukumu.” Kisha alisisitiza utume wa Jimbo la Hong Kong kama daraja na kuongeza kuwa amemwalika Askofu Mkuu Li Shan kutembelea Hong Kong. Na siku ya  Ijumaa tarehe 21 Aprili 2023 , Askofu  aliongoza Misa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph (Dongtang) nakuhitimisha akiwasalimu waamini walioshiriki katika adhimisho hilo. Askofu alindokea  Beijing akirudi kwao  huko Hong Kong.

 

22 April 2023, 14:32