Sinodi-Afrika,Sr.Nathalie:Uhusiano wa kianthropolojia wa Afrika ni muhimu!
Sr. Jecinter Antoinette Okoth, FSSA, AMECEA
Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu ameeleza upekee wa mkutano wa bara uliomalizika hivi karibuni mjini Addis Ababa, Ethiopia, huku akibainisha kwamba anthropolojia ya Kiafrika ilionekana wakati wa mkutano huo wa Juma moja. Katika mahojiano na AMECEA Mtandaoni Dominika tarehe 5 Machi 2023, Sr. Nathalie Becquart mwanamke wa kwanza kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi alisema, “Hapa Afrika kuna hisia kwamba watu wanaishi imani na kukutana na wengine si tu na ubongo na akili lakini kwa hisia zote. Hiki ni kitu cha kipekee sana kutoka Afrika ambacho nadhani pia kinatokana na anthropolojia ya uhusiano: hisia kwamba siwezi kuishi bila ‘sisi’ na niko kwa sababu wewe uko.”(falasafa ya Ubuntu)
Wwakati wakitoa wito kwa Waafrika wote kushiriki roho moja na watu wa Mungu kutoka sehemu nyingi za dunia hasa ambako kuna mbinu hiyo ya kibinafsi, Mtawa wa Wamisionari Yesu Kristo wa Xaveri (XMCJ) alisimulia kwamba hisia ya ushiriki iliyojitokeza wakati wa mkutano wa sinodi ya bara ni zawadi maalum kutoka Afrika. Sr. Nathalie alifichua kwamba baada ya kuhudhuria mikutano tofauti ya sinodi ya bara ndani ya bara la Australia na visiw vyake na ile ya Mashariki ya Kati, amejioneana jinis ambavyo watu wana vipawa vya pekee kwani wengine wana maana ya ukimya. Wakati wa mahojiano hayo mtawa huyo wa kifaransa ambaye ndiye mwanamke wa kwanza kuwa na haki ya kupiga kura katika mkutano wowote ujao wa maaskofu, alithamini kwamba katika bara la Afrika, watu wa Mungu wana roho ya sahuku ya kuendelea na mchakato wa safari ya sinodi.
Kwa mujibu wake alisema “Kinachonishangaza ni kwamba kwa Afrika ninapozungumza kuhusu sinodi karibu kila mtu anaungana na dhana ya Kanisa kama familia ya Mungu ambayo ilikuwa matokeo ya sinodi barani Afrika, ambapo kama mkurugenzi wa zamani wa Huduma ya Kitaifa katoliki ya Ufaransa kwa ajili ya Uinjilishaji waw a watu na miito kwa Vijana” na kuongeza kuwa “Inapendeza kusikia zaidi kuhusu uhusiano kati ya sinodi na maadili ya kiutamaduni ya Afrika: Mshikamano, hali ya familia, mazungumzo ikiwa ni pamoja na palaver, Ubuntu na Ujamaa.”
Baada ya mazungumzo na zaidi ya wajumbe 200 kutoka bara na wajumbe wengine waloalikwa kutoka Vatican, Sr. Becquart Sr. aliona kwamba ingawa mada ya sinodi ni ya kawaida katika mabara yote, kwa upande wa Afrika inaelezwa kutoka na ndani ya uhalisia wa utamaduni wa Kiafrika. Hata kama mbegu za sinodi tayari zipo katika bara hili, Sr. Becquart alisema “Bado kuna magugu na vikwazo katika mchakato wa sinodi hivyo wito wa kuendelea na safari ya sinodi na muda wa kujifunza jinsi ya kuwa sinodi ambayo inapaswa kuwa njia ya mazungumzo ya kibinafsi na ya jumuiya euendelee.” Katika Mkutano huo uliojumuisha vijana, walei, wajumbe kutoka dini nyingine, wanaume na wanawake, mapadre maaskofu na Makardinali, Sr. huyo alisema, ni mchanganyiko mzuri ambao ulitoa nafasi kwa wamini wote wa Kanisa na watu wa Mungu kusikiliza na pia ishara ya utofauti katika Kanisa.
wakati wa mkutano wa sinodi ya bara la Afrika akilinganisha mchakato wa sinodi barani Afrika na mabara mengine ambayo tayari alitembelea, mtawa huto ambaye alihudumu kwa miaka 10 katika Baraza la Maaskofu wa Ufaransa alisema, “Katika Afrika tumepitia hali ya mazungumzo ya kiroho kwa namna fulani ya kusikilizana kwa njia ya majadiliano na mazungumzo katika vikundi vidogo kwa roho ya sala na utambuzi, zaidi ya hayo, kulikuwa na ibada ya Kilatini na ibada ya kiethiopia ambayo ni ishara nzuri ya sinodi kwamba hatuna Kanisa la Kilatini tu bali pia na Makanisa ya Mashariki”. Katika Afrika watu hawakuzungumza tu kuhusu Kanisa bali pia masuala mengine ya bara hili ikiwa ni pamoja na umaskini, haki, utunzaji wa kazi ya uumbaji, utawala bora ambayo ni halisi katika maisha ya watu.
Mtawa huyo alifichua zaidi katika Amerika ya Kusini, sinodi ilipangwa na kujadiliwa katika makusanyiko ya eneo kabla ya kusanyiko la mwisho la bara,” (Wakati) “Katika Mashariki ya Kati kulikuwa na Makanisa kutoka kwa taratibu saba zinazoonesha tofauti za Kanisa.” akihitimisha, Sr. Becquart alishukuru sana fursa ya kutembelea Afrika na kuwa sehemu ya safari ya bara akisema, “Ninashukuru kwa uzoefu huu. Tulikuja wajumbe kutoka Vatican kusikiliza na kuwa pamoja na watu na kujifunza katika mchakato huo.” “Nimefurahishwa sana na kuguswa na mazungumzo niliyoyasikia kutoka kwa vijana, walei, watawa, mapadre, maaskofu na Makadinali. Nimejisikia udugu mkubwa na ilikuwa baraka kusafiri na Afrika kwani hii inanipatia hamu ya kurudi na kugundua zaidi kuhusu Afrika.”