Kardinali Ambongo Rais wa Secam ameandika ujumbe wa heri kwa niaba ya Kanisa Barani Afrika kumpongeza Papa kutimiza miaka 10 ya upapa. Kardinali Ambongo Rais wa Secam ameandika ujumbe wa heri kwa niaba ya Kanisa Barani Afrika kumpongeza Papa kutimiza miaka 10 ya upapa.  (AFP or licensors)

Miaka 10 ya Upapa,Kard.Ambongo-Secam:chaguo lako ni la kimisionari

Miaka kumi ya upapa imeadhimishwa na umakini wake wa kipekee kwa wale waliopendelewa na Bwana Yesu:maskini,wahamiaji,wakimbizi na wale wote wanaoishi katika pembezoni mwa maisha.Na hapo umewagusa kwa mkono na moyo wakazi 1,340 598147 wa Afrika wanaoishi katika changamoto.Ni maneno ya Kardinali Ambongo,Rais wa Secam.

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Kwa niaba ya Kanisa Barani Afrika na Visiwani, ninakupa pongezi na ninakutakia kila la kheri kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 10 ya utume wako wa mtume Petro. Katika kipindi cha kuanzia tarehe 11 Machi 2023 hadi 19 Machi 2023, sherehe mbalimbali za kiliturujia zinafanyika katika pembe zote za Bara la Afrika na Visiwa vyake kwa ajili ya shukrani kwa Mungu kwa zawadi ya Upapa wako na pia kama njia ya kufanya upya ufuasi wetu, wa mafundisho ya Askofu wa Roma na mapenzi yetu kwa Papa Francisko. Ndivyo ameanza kuandika Kardinali Fridolin Ambongo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar (SECAM) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kinshasa DRC.

Umewagusa watu 1,340 598 147 wakazi wa Afrika wanaoishi na changamoto

Kwa hiyo akiendelea na matashi mema hayo, Kardinali Ambongo anaandika kuwa: "Baba Mtakatifu, miaka kumi ya upapa wako imeadhimishwa na umakini wako wa kipekee kwa wale walio pendelewa na Bwana Yesu kama vile maskini, wahamiaji, wakimbizi na wale wote wanaoishi katika pembezoni mwa maisha na huwepo. Na hapa umewagusa kwa mkono na moyo wakazi 1, 340 598 147 wa Afrika wanaoishi katika hali hizi zenye changamoto. Ukijidhihirisha kuwa mtume wa huruma ya Mungu, ulitangaza Jubilei ya Ajabu, kwa ajili ya matumaini ya kuona uso wa Kanisa linalovumbua tena matumbo ya huruma na kwenda kukutana na majeruhi wengi wanaohitaji kusikilizwa, kueleweka na kupendwa. Katika miaka hii kumi tumeona maendeleo ya chaguo la kimisionari ambalo, kwa kubadilisha kila kitu, hufanya desturi, lugha na muundo wote wa kikanisa kuwa njia ya uinjilishaji wa ulimwengu wa sasa badala ya njia ya kujilinda" (EG, 27), amefafanua Kardinali Ambongo.

Miaka kumi ya uongozi wa kinabii na utumishi unaovuka mipaka

Kardinali Ambongo amefafanua kuwa: "Hii ni miaka kumi ya uongozi wa kinabii na utumishi unaovuka mipaka ya Kanisa Katoliki na majadiliano na dunia nzima: “Ikiwa tunataka dunia yenye udugu zaidi ni lazima tuelimishe vizazi vipya ili kutambua, kuwathamini na kuwapenda watu wote bila kujali ukaribu wao wa kimwili, bila kujali mahali walipo duniani ambapo kila mmoja alizaliwa au anaishi (Ft, 1)." Kwa hiyo “Ikolojia ya binadamu haiwezi kutenganishwa na dhana ya manufaa ya wote, kanuni ambayo ina jukumu kuu na la kuunganisha katika maadili ya kijamii” (FT, 1). LS, n.156). Kwa kuongezea Kardinali Ambongo ameandika kuwa " Baba Mtakatifu, katika miaka hii 10, Afrika imekuwa na furaha ya kukukaribisha mara nne. Bara linakushukuru sana kwa kuja kwetu kama mwanahija wa matumaini, na kuomba pamoja nasi kwa ajili ya amani, haki na upatanisho na kutusaidia kupaza sauti zetu kwa ajili ya uhuru wetu wa kiuchumi". Na kwa kuhitimisha anaandika: "Baba Mtakatifu Kanisa barani Afrika linakuombea afya yako na huduma yako”.  Tunakupongeza Baba Mtakatifu!

Kardinali Ambongo Kwa niaba ya SECAM
12 March 2023, 19:26