Maaskofu Marekani na Canada:hakuna ukoloni tena ni kutembea njia ya amani!
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Jumuiya ya Kikristo haitaweza tena kujiruhusu kuambukizwa na wazo kwamba tamaduni moja ni bora kuliko zingine. Maaskofu wa Marekani na Canada wanatoa shukrani zao kwa tamko la “Fundisho la Ugunduzi” kuwa ni , hatua ya mbele katika kuonesha wasiwasi na umakini wa kichungaji kwa watu wa asilia na wa kiasili ambao wamepata mateso makubwa kutokana na urithi wa mawazo ya ukoloni.Katika maelezo, Askofu Mkuu Paul S. Coakley, wa Jimbo la Mji wa Oklahoma na katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, wanaungana na kulaani ukatili na dhuluma inayotendwa na wenyeji na watu wa kiasili, na wanaunga mkono uungwaji mkono uliooneshwa na Kanisa kwa ajili ya hadhi yao na haki zao za kibinadamu na huonesha majuto na uchungu kwa nyakati zote ambazo Wakristo, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kikanisa, hawakupinga kikamilifu vitendo vya uharibifu na ukosefu wa maadili vya mamlaka ya kikoloni ya kushindana.
Maaskofu wanaunga mkono sera za maskini na wasiojiweza
Kwa miaka mingi hata hivyo, imebainishwa, nchini Marekani, mazungumzo kati ya maaskofu wa Kikatoliki na viongozi wa makabila ambapo walitazama vipengele zaidi vya historia hii chungu. Maaskofu wanaahidi kuunga mkono sera zinazowapendelea maskini na wasiojiweza na zinazoleta ahueni kwa familia asilia na wazawa walio katika matatizo. “Kama Kanisa ni muhimu kuelewa kikamilifu jinsi maneno yetu yametumiwa na kutumiwa vibaya ili kuhalalisha matendo ambayo yangechukiwa na Yesu Kristo”. Matumaini ni yale ya mazungumzo zaidi ya kukuza uelewa zaidi wa historia hii ngumu, kwa sababu hiyo pamoja na Mabaraza ya Maaskofu wa Canada na Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Historia, Maaskofu wa Marekani wanatafakari juu ya uwezekano wa kuandaa “Kongamano la kitaaluma na wasomi wazawa na wasio asilia ili kuongeza uelewa wa kihistoria wa 'Mafundisho ya Ugunduzi'.
Mchakato wa uponyaji kwa msaada wa Mungu
Katika barua yao, inasomeka kuwa Wazo, limepokelewa kutiwa moyo na Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Maendeleo Fungamani ya Kibinadamu na Baraza la kipapa la Utamaduni na Elimu. Ni Matumaini kwamba, kwa msaada wa Mungu, pamoja na kuwaponya wale ambao bado wanateseka kutokana na urithi wa ukoloni, wao hawa wezi kamwe kurudi katika njia ya ukoloni, bali watembee pamoja kwenye njia ya amani”.
Kamwe zisitumiwe zana za ukandamizaji
Kama ilivyo kwa maaskofu wa Marekani, hata kwa maaskofu wa Canada pia walionesha kwamba kwa karne nyingi kauli nyingi na za mara kwa mara za Kanisa na Papa zimeunga mkono haki na uhuru wa watu wa kiasili na jinsi Papa katika siku za hivi karibuni alivyoomba msamaha katika matukio kadhaa kwa ajili ya matendo maovu yanayofanywa na Wakristo dhidi ya watu wa kiasilia. Andiko hilo linakumbusha kwamba “Mafundisho ya Ugunduzi” si sehemu ya fundisho la Kanisa Katoliki, kwamba, hasa, Hati ya karne ya XV “hawakuwahi kuchukuliwa kama kielelezo cha maneno ya imani ya Kikatoliki” na kwamba “hayajawahi kungazia vya kutosha na kuakisi hadhi sawa na haki za watu wa kiasilia. Kwa hiyo “Kamwe hazitatumika zana zinazotumiwa kuwalazimisha wengine”, wamehitimisha Maaskofu wa Canada.