Umati wa kukumbuka“Kutembea pamoja na waathirika wa biashara mbaya wa binadamu
Vatican News
Juma la Kimataifa ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu illimalizika kwa kushiriki katika Sala ya Malaika na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro Dominika tarehe 12 Februari 2023 pakiwepo kundi la vijana wawakilishi wa kimataifa wa mtandao wa Siku ya Kusali na Kutafakari Dhidi ya Biashara Haramu Ulimwenguni ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 Februari, sambamba na Siku kuu ya Mtakatifu Josephine Bakhita, mwathirika wa biashara hiyo mbaya ya binadamu. Siku ya Ijumaa tarehe 10 Februari, walifanya tukio moja muhimu wakitembea kupitia katika njia ya Conciliazione, Roma hadi mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, vijana kumi na tano walifika Roma kutoka sehemu mbalimbali za dunia na ambao walweza kutoa uhai kwa kundi la watu dhidi ya vitisho vya biashara haramu ya binadamu na utumwa wa watu, unaoratibiwa na mtandao wa Talitha Kum.
Mtandao wa kimataifa wa kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu una simamiwa na watawa, marafiki na washirika zaidi ya 3,000, na unahamaishwa na Muungano wa Mama Wakuu na Mashirika ya kitawa , kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Mtandao wa Nia za Maombi ya Papa Kimataifa., Caritas Internationalis, CoatNet, Harakati ya Focolare Shirika la Kijesuit la Huduma ya Wakimbizi, Umoja wa Kimataifa wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki (WUCWO), Jumuiya ya Yohane XXIII, Shirikisho la Kimataifa la Matendo katoliki, Chama Katoliki cha Scouts na cha Ulinzi (Agesci), Kundi la Mtakatifu Marta na mashirika mengine mengi duniani kote. Siku hiyo inaungwa mkono na Mfuko wa Kimataifa wa Mshikamano.
Kauli mbiu ya mwaka 2023 ni “Walking for Dignity”, yaani kutembea kwa hdhi ambapo Sista Abby Avelino, mratibu wa kimataifa wa Talitha Kum, alielezea kwamba ilichaguliwa na kikundi cha vijana kutoka pande zote za dunia kwa nia ya kuwaalika watu wenye mapenzi mema kutembea pamoja na wahanga na manusura wa ajali hiyo., ya Biashara haramu ya binadamu, hasa wahamiaji, ambapo kama mahujaji wa utu na matumaini ya binadamu. Vijana, watu wazima na watoto, watu wa mila, tamaduni na vizazi mbalimbali vya kidini. Ni kwa pamoja tu, kama jumuiya, tunaweza kukomesha janga hilo la usafirishaji haramu wa binadamu. Kulinda heshima ya kila mtu kunawezekana tu ikiwa tunajua jinsi ya kulinda amani na mazingira asilia. ”