2023.02.25  Nathalie Becquart_Katibu wa Sinodi ya Maaskofu akihutubia katika Mkutano wa Kibara huko Asia 2023.02.25 Nathalie Becquart_Katibu wa Sinodi ya Maaskofu akihutubia katika Mkutano wa Kibara huko Asia 

Sr. Becquart:Sinodi iwe shughuli ya kichungaji ya Kanisa

Katibu Msaidizi wa Sinodi amezungumza 25 Februari katika Mkutano wa Baraza la Sinodi la Makanisa ya Asia,mjini Bangkok.Kanisa la kisinodi ni njia pekee ya kusambaza imani leo hii.Katika siku ya pili ya kazi,washiriki vijana walitafakari juu ya vipaumbele vitano kwa ajili ya bara la Asia.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Sinodi ni zawadi na katika kusikiliza wito wa Mungu ni lazima tuwe na tabia ya kushukuru. Hayo yalisemwa na Sr. Nathalie Becquart, Katibu Msaidizi  wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Baraza la Sinodi la Makanisa ya Asia, ambayo kazi yake ilianza mnamo Ijumaa tarehe 24 Februari 2023. Mtawa huyo kwanza kabisa aliwashukuru vijana waliokuwepo kwamba kwa hakika ni baraka kuwasikiliza, kujifunza kutoka kwao na kuwa sehemu ya mkutano huo wa kibara. Sr.  Becquart wakati wa hotuba hiyo alitafakari mambo matatu pamoja na vijana wa Bara la Asia. Kipengele cha kwanza kilikuwa ni kuona sinodi kama mwito kutoka kwa Bwana. Sio suala la kusema kama tunaipenda, hatupendi, iwe tunasajili shauku nyingi au la, lakini ni kujibu mapenzi ya Mungu kwa  ajili ya Kanisa la milenia ya tatu, alisisitiza. Katika kueleza dhana hiyo alimnukuu mtaalimungu  wa Australia, Herman Rush, ambaye aliandika jinsi ambavyo sinodi ilivyo kwa ufupi, kuwa ni Mtaguso wa Pili wa Vatican.

Kwa hiyo, mtawa huyo alisema wanachofanya sasa ni kuendeleza mapokezi ya Mtaguso ho na  kuutekeleza. Mawazo ya Katibu huyo yalikwenda ndani ya Sinodi juu ya vijana na kwamba walielewa kama Kanisa kama njia pekee ya kueneza imani leo hii katika ulimwengu huu, katika jamii inayobadilika na changamoto zote wanazozijua ni kuwa Kanisa la kisinodi. Mafundisho yametoka kwa vijana kwa Wakristo wote, kwa sababu sio huduma ya vijana pekee yake ambayo lazima iwe sinodi, lakini  ni kila aina ya kazi ya kichungaji Baada ya kufafanua sinodi  kama mchakato  wa kina  ambapo ni muhimu kutoa nafasi kwa nyingine, kumfuata Kristo kwenye njia ya uongofu wa kweli na mabadiliko, Sr Nathalie  aliwaalika wale waliohudhuria  mkutano huo wote kutambua, kwa sababu utambuzi unajumuisha kwa usahihi kusikiliza. Roho ndani yetu na katika wengine walioko kwenye kundi. Jambo la pili aliongeza  linajumuisha kuishi sinodi kama zawadi.

Kwa njia hiyo Sr alifafanua likichopelekea kuzidisha usikivu kwa wote  na utambuzi na kutambua mwitikio wa wito huo kutoka kwa Mungu kwamba  ni mtazamo wa shukrani. Kadiri tunavyoweza kupambanua zawadi ya sinodi ambayo tayari tumeipokea, ndivyo zaidi tutajifunza kutoka ya zamani kuyaelekeza katika siku zijazo, kwa sababu sinodi ni njia ya ubunifu. Baada ya kusikia mwito wa Mungu na kuonesha shukrani kwa karama ya sinodi, wakati unafika wa kuchagua. Jambo la tatu ni chaguo hilo, matunda ya utambuzi. Hatua ya tatu ya safari ni kupambanua na kuchagua, kuwa na uwezo wa kuelewa ni hali zipi za haraka sana za kukabiliana nazo. Kwa mujibu wa Sr. Nathalie Becquart  kwa vijana alisema “Leo tumeitwa kuchagua vipaumbele, kuangalia mapungufu mbalimbali. Katika kukubali kwamba kamwe si rahisi kuchagua vipaumbele, mtu anaelewa umuhimu wa kuwa na mbinu kisha kufikia uamuzi, daima kwa kumsikiliza Roho”.

Vikundi mbalimbali vya wahusika wakuu wa vijana huko  Bangkok vilifanya kazi pamoja, kuwasilisha masuala ya dharura ya bara la Asia, kuelewa matatizo na mapungufu, na kisha kuendelea na uteuzi wa vipaumbele vitano. Mwisho utawasilishwa wakati wa vuli katika awamu inayofuata ya Sinodi. Kila kipindi cha kazi kimehitimisha  kwa sala kabla ya Sakramenti Takatifu. Kusimamia na kuratibu vikundi hivyo aalikuwa ni Askofu Mkuu Anil Joseph Thomas Couto, wa Jimbo Kuu katoliki la  Delhi; Christina Kheng, mjumbe wa Tume ya Mbinu  ya Sinodi na Momoko Nishimura, Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Sinodi ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia (FABC).

Katika siku hizi wajumbe wa nchi 29 zinazounda Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Asia (FABC), waliokusanyika katika Baan Phu Waan, kituo cha mafunzo ya kichungaji cha jimbo kuu la Bangkok, na walishirikisha uzoefu wao na kuzingatia mada na mivutano mbalimbali inayoikumba Asia  na ili sinodi, iweze kufanya  maamuzi, kipadre. miito, vijana, maskini, migogoro ya kidini na mapadre kwa matumaini ya kuweza kutembea pamoja katika bara kubwa na mseto la Asia katika siku zijazo. Kazi zote za vikundi na uingiliaji kati zitaingiza katika hati ya mwisho ambayo itawasilishwa kwenye mkutano na itawakilisha mchango wa Makanisa katika bara la Asia kwa ajili ya kuandaa rasimu Hati ya Kitendea Kazi ya Sinodi ya Oktoba 2023.

27 February 2023, 12:02