Awamu II ya sinodi kibara kwa Ulaya inaendelea huko Praga!
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Akiwa katika Ziara yake ya Kitume Barani Afrika, kuanzia tarehe 31 Januari hadi 5 Februari 2023, Papa Francisko kati ya mengi aliyofanya na kushauri, alikumbuka mojawapo ya vipengele muhimu vya utendaji wa kisinodi, kwamba: “Jukumu la Maaskofu si kuwa maafisa wa watakatifu, wasimamizi au viongozi wa makabila, bali ni kuwa wachungaji wanaochafua mikono katika Kanisa, katikati ya watu", kwa hiyo hata huko Praga viongozi wa Kanisa Barani Ulaya wameingia katika uendeshaji wa hatua ya kibara wa mchakato wa sinodi, ambao kimsingi ni kuthibitisha dhana hiyo muhimu sana kwa Kanisa na waamini wake.
Mikutano Saba ya kibara
Mchakato wa Kanisa la Sinodi unaongozwa na kauli mbiu: “Ushirika, ushiriki, na utume (2021-2024) ambao unaendelea kuingia katika moyo wa awamu tofauti ambayo ilidhamiliwa. Baada ya mashauriano katika makanisa mahalia yaliyomalizika hivi karibuni katika majira ya kiangazi kwa sasa ni 'hatua' ya pili, ile ya Mashirikisho ya mabaraza ya maaskofu kwa ajili ya Sinodi ya kibara. Katika wakati huu, huko Australia ulianza Dominika tarehe 5 Februari huko Suva (Visiwa vya Fiji hadi 10 Februari).
Hivyo hivyo hata huko Mashariki ya Kati, kuanzia tarehe 12 hadi 18 Februari ijayo itakayofanyika huko Beirut (Lebanon); kwa Bara la Amerika ya Kaskazini kuanzisia tarehe 13 hadi 17 Februari, itakayofanyika huko Orlando (Florida); kwa upande wa Bara la Asia kuanzia tarehe 23 hadi 27 Februari, itakayo fanyika huko Bangkok (Thailand); kwa upande wa Bara la Afrika ni kuanzia tarehe 1 hadi 6 Machi 2023 huko mjini Addis Ababa (Ethiopia); kwa Upande wa Amerika ya Kusini kuanzia tarehe 17 hadi 23 Machi itakayofanyika huko Bogota (Colombia).
Wajumbe mia mbili kutoka Ulaya
Pamoja na maadhimisho ya Misa, iliyoongozwa na Askofu Mkuu Jan Graubner, wa Praga katika Kanisa la Premonstratensian huko Strahov, Mkutano wa Bara la Ulaya kwa ajili ya Sinodi ulifunguliwa usiku wa tarehe 5 Februari katika mji mkuu wa Czech. Mkutano huo, unaoendelea hadi tarehe 12 Februari 2023 na ambao zaidi ya hayo unaadhimishwa katika kumbukumbu ya miaka ishirini ya Waraka wa kitume baada ya Sinodi wa Mtakatifu Yohane Paulo II uitwao ‘Ecclesia in Europa’ yaani Kanisa barani Ulaya, mkutano uliogawanyika sehemu mbili : wa moja kwa moja wenye wajumbe wapatao 200 (156 kutoka katika mabaraza ya Maaskofu 39 wa Ulaya.
Mabaraza mengine 44 yaliyoalikwa binafsi na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya CCEE) wakikutana ili kuelezea changamoto na uwezekano wa Sinodi; na ya pili, kuanzia tarehe 11 hadi 12 Februari, ambapo marais 39 pekee yao ndio watakutana kutathmini yale yatakayojiri katika mijadala hiyo na kuanza kufafanua muhtasari utakaotumwa, ifikapo mwezi Machi, kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, pamoja na yatokanayo kutoka mabata mengine. Kutokana na uchunguzi wa Hati hizi saba za Mwisho, Instrumentum Laborius yaani Hati ya kitendea kazi itatayarishwa na kukamilika ifikapo mwezi Juni 2023.
Kukusanya matunda ya utambuzi katika ngazi mahalia
Chombo cha uendeshaji cha kufikia awamu hii ya majadiliano kati ya Makanisa mahalia, kilichotumiwa ili kuelewa jinsi kutembea pamoja inaendelea hasa katika hati ya kitendea kazi kwa hatua ya kibara ambayo inakusanya na kurejesha katika ngazi ya mahalia kile ambacho Watu wa Mungu wa dunia nzima walisema katika mwaka wa kwanza wa mchakato wa Sinodi.
Mwongozo sahihi wa kuwawezesha kuimarisha utambuzi wao, kwa kuzingatia maswali matatu: ambayo mwelelekeo unasikika sana; kwa hiyo nimasuala gani yanapaswa kushughulikiwa katika hatua zinazofuata; ambayo vipaumbele, mada zinazorudiwa na wito wa kuchukua hatua vitaweza kujadiliwa katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Sinodi mnamo Oktoba 2023.
Wajumbe wawakilishi wa aina mbalimbali za Watu wa Mungu
Matokeo ya kuhusika kwa kila Askofu wa jimbo na timu yake ya sinodi yanahitajika katika hatua ya bara. Uwakilishi wa aina mbalimbali za Watu wa Mungu umehakikishwa kuanzia Maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake watawa, walei wanaume na wanawake, kwa kuzingatia hasa wanawake na vijana. Kwa hiyo orodha ya washiriki wengine takriban wajumbe 390 kupita mtandaoni.