Tafuta

Picha ya Bikira Maria, Malkia wa Mashahidi wa Los Angeles nachini Marekani. Picha ya Bikira Maria, Malkia wa Mashahidi wa Los Angeles nachini Marekani. 

Mshukiwa wa mauaji ya Askofu David G.O’Connell amekamatwa

Ni mshangao mkubwa wa kukutwa mwili wa Askofu wa Msaidizi wa Los Angelis,Marekani aliyejitolea maisha yake kwa wengine kupigwa risasi kikatili mnamo tarehe 18 Februari 2023.Uchunguzi umemweka mbaloni mshukiwa ambaye ni mume wa mlinzi wa nyumba ya Askofu.Wamekataa pia dhamana ya dola milioni 2.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Huko Los Angeles, nchini Marekani, mamlaka imemkamata mshukiwa mume wa mwanamke ambaye alifanya kazi kama mlinzi wa nyumba ya Askofu Msaidizi David G. O’Connell kuhusiana na mauaji ya Askofu huyo msaidizi mpendwa wa Jimbo katoliki la  Los Angeles nchini Marekani. Hayo yamesemwa na  maafisa Jumatatu tarehe 20 Februari 2023. Sherifu wa Kaunti ya Los Angeles Bwana Robert Luna alimtambua Carlos Medina kama mshukiwa wa mauaji hayo. Hakutaja ni kwa nia gani lakini alisema mdokezi aliwaambia mamlaka kuwa Madina alikuwa akifanya mambo ya ajabu mara baada ya mauaji hayo na kudai kwamba Askofu huyo alikuwa na deni lake la pesa. Sherifu alisema Madina ana miaka 65; hata kama, rekodi za jela zinaonesha mshukiwa kuwa na umri wa miaka 61.

Sherifu alisema wapelelezi waliunganisha Madina na uhalifu kwa  njia ya video ya uchunguzi ambayo ilionesha gari  lake katika nyumba ya  Askofu O'Connell kuhusu wakati wa mauaji. Silaha zilipatikana katika nyumba ya huyo Madina huko Torrance, na sherifu alisema uchunguzi zaidi unaendelea. Ufichuzi kuhusu ufyatuaji risasi ulikuja wakati wa mkutano wa habari na waandishi  mchana wenye hisia kali ambapo maafisa na Askofu Mkuu José H. Gómez wa Los Angeles akimsufy  Askofu  O’Connell msaidizi wake kwa urafiki wake, wa kutokuwa na ubinafsi na umakini wake kwa jamii aliyokuwa akiipenda na kuitumikia kwa miongo kadhaa. "Askofu huyo alikuwa msaada wa wanyonge na tumaini la wasio na tumaini”, halisema pia Msimamizi wa Kaunti ya Los Angeles Janice Hahn, ambaye alielezea kuwa Askofu O'Connell alikuwa kama rafiki wa muda mrefu. “Alijua kwamba kumtumikia Mungu kulimaanisha kuwatumikia wanadamu.”

Askofu  O'Connell, mwenye umri wa miaka 69, aliuawa Jumamosi alasiri  tarehe 18 Februari 2023, katika nyumba inayomilikiwa na Jimbo  katoliki huko Hacienda Heights ambako aliishi peke yake. Luna alisema askofu huyo alipatikana chumbani kwake akiwa na jeraha moja la risasi sehemu ya juu ya mwili. Lakini hapakuwapo na bunduki iliyopatikana katika eneo la tukio, na hakukuwa na dalili ya kuingia  ndani kwa nguvu.  Na Wahudumu wa afya walimtangaza kuwa amefariki katika eneo la tukio. Wanandoa wanaoishi kwenye barabara tulivu, yenye mstari wa miti walisema hawakusikia mlio wa risasi au kelele nyingine isiyo ya kawaida kabla ya kuwasili kwa wazima moto na wafanyakazi wa gari la wagonjwa. Alipoulizwa kuhusu ni nani aliyepiga simu 911 kuripoti kisa hicho, Mpelelezi huyo alisema anaamini shemasi wa Kanisa alikuwa amekwenda nyumbani kwa Askofu O’Connell kumchunguza baada ya Askofu mwenyewe kuchelewa katika mkutano. Sheriff pia aliulizwa ikiwa viongozi walizungumza na mfanyakazi wa nyumbani. Kwa Sheri alisema wapelelezi walimhoji kabisa, ma kusema kuwa: “Kama tunavyojua kwa wakati huu amekuwa na ushirikiano kamili.”  Wapelelezi wa mauaji na uhalifu mkubwa walifanya kazi usiku kucha katika saa 48 tangu kuuawa kwa askofu huyo ili kumpata mshukiwa. “Tulimkamata kwa kazi ya ajabu ya upelelezi, aliongeza  “Kipaumbele chetu kinachofuata ni kumfanya ashtakiwe.

Naye Askofu Mkuu Gómez alitokwa  na machozi alipokuwa akiongea kuhusu Askofu O'Connell, ambaye alimkumbuka sana kwa lugha yake ya Kihispania iliyozungumza kwa lafudhi ya Kia Irland. Kwa hiyo Askofu mkuu alimwita O’Connell  kuwa “rafiki mzuri wa Los Angeles” na akasema kwamba “kila siku alitaka kuwahurumia maskini, wasio na makao, wahamiaji na wale wote wanaoishi kando ya jamii. Alikuwa kasisi mzuri, askofu mwema na mtu wa amani.” Sauti ya Askofu mkuu ilianza kutetemeka alipokuwa akizungumzia juu ya kifo cha rafiki yake kilivyo hasara kubwa na jinsi anavyoshukuru kwa Luna na timu ya wapelelezi “kwa kazi yao kubwa ya kumtia mshukiwa kizuizini.”  Baadaye Askofu Mkuu alishikwa  na mhemko wa huzuni sana na sheriff akamfariji. “Samahani, Bobby,” Askofu Mkuu  Gómez alisema,  huu akibainisha kwamba “ni wakati wa huzuni na uchungu kwetu sote. ... Tafadhali tuendelea kumuombea Askofu David na familia yake. Pia tuwaombee maofisa wa sheria wanapoendelea na uchunguzi.”

Seneta wa Jimbo, Bob Archuleta, ambaye ni meya wa zamani wa Pico Rivera ambaye alihudumu katika jeshi la polisi la Montebello, alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba, Askofu  O’Connell aliwagusa wote kwa  kumwita “askofu wetu, askofu wako. Alisema O’Connell “alikuwa na uwezo wa kutembea barabarani, kila mahali alipokwenda akiwaleta watu pamoja na makasisi, akiwaleta mapadri wengine pamoja, akileta familia pamoja, washiriki wa sehemu pamoja. Alileta kila mtu pamoja. Hakika alikuwa mtu wa karibu sana.” Msimamizi Hilda Solis alisema kuwa: “moyo wake umevunjika.” Kifo cha O'Connell “kinawakumba baadhi yetu, kwa sababu alikuwa rafiki wa kibinafsi na mtu ambaye alikuwa shujaa sana na mtu ambaye alijali jamii yetu, haswa jamii ya wahamiaji. Nilimfahamu kwa sababu ya shauku yake katika kusaidia kupitisha mageuzi ya uhamiaji.” O’Connell aliwahi kuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Uhamiaji cha SoCal cha kati ya Jimbo, akiwasaidia watoto wengi walioingia Marekani bila kuwa na msindikizaji wa watu wazima”.

Akiendelea alisema: “Kwangu mimi, kiukweli ni kazi ya upendo katika makala ya 2019. Hii ni, ninadhani, ni nini maana ya shule zetu na parokia. Sio tu kwa watoto wasio na wazazi bali kwa watoto wetu wote. Kuna janga la kuumiza watoto, hata wale ambao wana mengi sana. Wanahisi tumewaachwa. Na vijana wahamiaji wamekuwa kielelezo cha jamii yetu nzima.” Katika miaka ya 1990, AskofuO'Connell alipata sifa ya kutaka kuunganisha uhusiano kati ya wakaazi wa vitongoji vilivyokumbwa na ghasia na watekelezaji sheria wa eneo hilo baada ya mapigano ya Polisi wa  Rodney King. Naye Peter Dreier, profesa wa siasa za mijini katika Chuo cha Mashariki na mwandishi wa “The Next Los Angeles: The Struggle for a Livable City”, alimkumbuka Askofu O'Connell kama mratibu wa jamii anayeendelea,  ambaye aliweka haiba yake ya kibinafsi kufanya kazi kwa masikini na walionyimwa haki. "Siku zote nilivutiwa na werevu wa Baba Dave, huruma, na nia ya kuwapa changamoto watu walio madarakani kuhusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na haki za wahamiaji, haki ya makazi, ubaguzi wa rangi na usalama wa umma,Dreier aliandika katika chapisho la Facebook.  Na kwamba aliona kanisa kama chombo cha haki ya kijamii.”

Mwana parokia ya Kanisa la Mtakatifu Frances Xavier Cabrini huko Los Angeles Kusini, ambako Askofu O'Connell alihudumu kwa zaidi ya muongo mmoja, walimkumbuka mtu aliyekuwa mcheshi, kujitolea kwa kina kwa haki ya kijamii na kujitolea kutumikia jumuiya za Weusi na Amerika ya Kusini. Walipigwa na butwaa na kuhangaika kuelewa vurugu zilizogharimu maisha ya mtu ambaye wito wake ulijikita katika amani na upendo. Jarlath Cunnane, mchungaji katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Cornelius huko Long Beach, alikutana na  Askofu O’Connell zaidi ya miaka 50 iliyopita katika Chuo cha All Hallows huko Dublin, ambako walisomea pamoja  upadri. Walishirikiana kwa mambo yanayoshirikishwa na wote wawili ambao walisoma Kiingereza wakiwa katika chuo kikuu na Cunnane akaja kuthamini haraka uwezo wa O'Connell wa kutoa mzaha mzuri au maoni ya haraka katika karibu hali yoyote.

Wanaume wote wawili walihamia California, na urafiki wao uliongezeka zaidi na miaka. Mnamo 2020, wakati Cunnane alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa na maambukizi ya damu, Askofu O'Connell alimtembelea karibu kila siku. Cunnane alikuwa kwenye mashine ya oksijeni wakati huo na alikuwa na ladha ya kutisha kinywani mwake, alikumbuka, hivyo Askofu O'Connell alivyokuwa karibu kila mara akimletea kinywaji cha kombucha alipomtembelea.  “Alikuwa na uwezo mkubwa wa urafiki,” alisema. Marafiki hao wawili walikutana kwa chakula cha jioni Alhamisi kwa kukutana tu na , Cunnane alisema, na walijadili mipango ya Cunnane  ya kutembelea baadhi ya parokia katika eneo la  Askofu O'Connell katika siku za usoni. Rafiki yake wa muda mrefu hakuwa ameelezea wasiwasi wake kuhusu usalama wake, alisema Cunnane kwa hivyo alipigwa na butwaa alipojua kwamba alikuwa amepigwa risasi hadi kufa. “Nani Duniani angependa kufanya hivi?” Aliuliza. Mwandishi wa wafanyakazi wa Times Michael Finnegan alichangia ripoti hiyo.

21 February 2023, 12:11