Ameyu,Sudan Kusini:Ziara ya Papa itagusa mioyo ya wengi!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Katika mahojiano na Vatican News na Askofu Mkuu Stephen Ameyu Mulla wa Jimbo Kuu katoliki la Juba nchini Sudan Kusini katika fursa ya kumsubiri Papa Francisko atakayefika huko tarehe 3 Februari 2023 ameabainisha kwamba waamsubiri kwa upendo wa Kikristo na wana uhakika kwamba hija yake nchini Sudan Kusini itagusa mioyo ya watu wote, wakiwemo wanasiasa. Kuna matarajio makubwa, kama vile unapotarajia mgeni muhimu na mwanafamilia. Wanayo imani kwamba, hija ya kiekumene ya Baba Mtakatifu Francisko itaponda kichwa cha shetani anayechelewesha amani kamili nchini Sudan Kusini, kwani imani ya watoto wa Mungu ina nguvu kuliko uovu. Pia ni fursa kwa viongozi kujumuika, kuunganisha akili pamoja na kuwaongoza watu wa Sudan Kusini kuelekea amani, upatanisho na upendo.
Wanafahamu kwamba Baba Mtakatifu anafanya ziara hiyo kukutana nao na kugusa mioyo yao kwa maombi yake, ili Roho wa Mungu awepo katika mapatano yao ya amani. Kwa Wakatoliki Askofu Mkuu amesisitiza kuwa ni wakati wa furaha kubwa na udadisi, hasa kwa wale wasiomjua Papa. Wanapongojea ziara ya kitume, ya Papa wao kama Maaskofu wanataka kuweka nuru ya mwelekeo wa kiroho na kusaidia watu kuelewa maana yake, na kwa kufanya hivyo katika kila misa wanayo sala ya maandalizi ya ziara ya Baba Mtakatifu.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Juba amesisitiza aidha kwamba utekelezaji wa makubaliano yaliyorekebishwa haupaswi kujadiliwa kwa maneno au kwa miezi, lakini kutekelezwa kwa barua na katika roho. Ni matumaini yao kwamba ziara ya Baba Mtakatifu itawafanya waelewe kwamba hakuna muda tena, kwamba njia pekee ya kusonga mbele ni ile ya amani. Watu hata wasio wakatoliki wanatarajia mengi kutoka kwa Papa. Parokia zimeandaa mikesha ya maombi ili kujiandaa na ziara yake. Wana uhakika kwamba waaambukizwa na furaha na matumaini ya Papa Francisko. “Watu wetu wanahisi kuheshimiwa, roho ziko tayari, na pia mioyo. Vipengele vya vitendo vinakamilishwa”. Na kwa upand ewa “Hali ya hewa nchini humo inatia moyo sana.
Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Ameyu alibainisha kuwa wanazishukuru kamati mbalimbali za waamini kwa ukakamavu na ujasiri wao wa kujiandaa na ujio wa Baba Mtakatifu, na wana imani kwamba ziara yake itawatajirisha wao kama Kanisa, lakini pia kama taifa. Ulimwengu hauwezi kuangalia upande mwingine: kuna majukumu ya kawaida. Nchi changa ambayo inatamani sana amani inahitaji maono ya kimataifa ya Papa Francisko. Na kwa kuhitimisha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Juba mahali ambapo Papa anakwenda amesema“Karibu, Baba Mtakatifu. Sudan Kusini ina furaha kuwa na mrithi wa Petro katika ardhi yake”, amehitimisha.