DRC:Vijana wa Congo wameomba Papa kuwatangaza kuwa watakatifu Anuarite na Bakanja
Na Stanislas Kambashi, SJ - Kinshasa,DRC.
Wakiungana na utamaduni ambao wakati mwingine huonekana katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, waamini wa Congo walituma fursa ya ujumbe huo kwa Papa Francisko kuhusu WenyeHeri wawili wapendwa zaidi barani Afrika ambao bado wako kwenye mchakato wa kutangazwa watakatifu kuwa kweli watakatifu wa Kanisa katika bara la Afrika. Uwanja wa Mashahidi, katikati ya mji wa Kinshasa, ulijaa watu hadi Alhamisi, tarehe 2 Februari, kwa ajili ya mkutano wa Papa Francisko na vijana na Makatekista. Makundi haya mawili ya waamini wakatoliki walimiminika kutoka kila pembe na parokia za Congo kumsikiliza Baba Mtakatifu katika tukio hilo ambalo lilikuwa maalum kwa ajili yao. Waziri Mkuu wa Congo Jean Michel Sama Lukonde na mamlaka nyingine kadhaa pia walikuwepo, pamoja na wajumbe kutoka nchi nyingine. Katika uwanja huo, bendera yenye maandishi ya lugha ya Kiitaliano “Santi Subito” yaani "Watakatifu mara moja," iliyoambatana na picha za Mwenyeheri Anuarite na Bakanja izlioneshwa mara kadhaa. Katika pande mbili za jukwaa ambalo Papa Francisko alizungumza kulikuwa na picha za mashahidi hao wawili wa Congo. Hata hivyo uhuishaji wa umati wa watu kabla ya kuwasili kwa Papa Francisko ulishuhudia imani hai na uhai wa ajabu wa Kanisa la DRC.
Anuarite na Bakanja, ni mifano ya imani na msamaha
Mwenyeheri Anuarite na Mwenyeheri Bakanja walitangazwa kuwa wenyeheri na JMtakatifu Yohane Paulo II: Wa kwanza ikiwa mnamo mwaka 1985 huko Kinshasa, wakati wa ziara ya pili ya Papa nchini Congo (wakati huo ikijulikana kama Zaire) na ya wa Pili ilikuwa ni Jijini Roma mwaka 1995. Tangu wakati huo, Wakongo wengi na Waamini Wakatoliki Barani Afrika wamezidi kukuza kwa kina ibada kubwa kwa Wenyeheri hao wawili wa Congo, waliokufa kama wafiadini kwa ajili ya uaminifu wao kwa Kristo. Katika hotuba yake siku ya Alhamisi, Baba Mtakatifu Francisko aliwataja kuwa ni mifano ya imani, ujasiri, uvumilivu na msamaha. Akijihutubia kwa vijana, Papa pia alimtaja Mtakatifu Kizito, ambaye alikuwa ni kijana wa Uganda.
Aliyeuawa shahidi mwaka 1964 kaskazini mashariki mwa DRC kwa kuulinda usafi wake hadi kifo chake, Mwenyeheri Anuarite alikuwa Mtawa wa Shirika la Masista wa Familia Takatifu, Bafwabaka. Kwa hiyo Anuarite ni kielelezo cha uaminifu katika kumfuata Kristo kama mtu aliyewekwa wakfu. Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Desemba. Wakati huo huo Mwenyeheri Bakanja ambaye ni mlezi wa walei na vijana wa Congo, alikufa mnamo tarehe 15 Agosti 1909 kutokana na majeraha aliyopata kama adhabu kwa ajili ya imani yake, ambayo alivumilia kwa uvumilivu mkali wakati akimsamehe hata mchokozi wake. Bakanja alitangazwa kuwa mwenyeheri na Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 24 Aprili 1994. Sikukuu yake imewekwa na Mama Kanisa kila mwaka tarehe 15 Agosti, katika kalenda ya kiliturujia.
Baba Mtakatifu Francisko amemtaja Mwenyeheri Bakanja kuwa ni kielelezo cha imani kwa vijana katika Waraka wake wa Kitume wa Christus Vivit. Kwa hiyo Bakanja alijulikana kama Katekista kijana ambaye alitumia muda wake wa bure kuwafundisha majirani na marafiki zake rozari na sala nyingine. Askofu Timothée Bodika Mansiyai, Rais wa Tume ya Maaskofu wa Congo kwa ajili ya Walei, alikumbusha fadhila za Mwenyeheri Bakanja katika hotuba yake ya utangulizi mbele ya Baba Mtakatifu Francisko. Kwa hiyo waamini wa DRC wanaendelea kutoa maombi yao kwa ajili ya kutangazwa watakatifu hao wafia dini wawili wenyeheri. Siku ya Alhamisi, tarehe 2 Februari kwa hiyo waamini na vina walipata furs ana njia ya kufikisha shauku yao kwa Papa Francis. Kanisa la DRC pia linasubiri kutangazwa kuwa Mwenyeheri Mtumishi wa Mungu, Christophe Munzihirwa Mwene Ngabo, ambaye alikuwa ni Askofu Mkuu wa Kijesuit wa Jimbo Bukavu aliyeuawa mnamo mwaka 1996.