Ave Maria katika maadhimisho ya miaka 10 ya Upapa wa Francisko
Vatican News.
Ramani ambayo ina mishumaa mingi inayowashwa ili kumwonesha ari ya Papa Francisko ya msaada unaotolewa kwake wa sala za waamini kutoka ulimwenguni kote, kwa kuzingatia kumbukumbu ya miaka 10 ya upapa wake. Wazo la kuanzisha tukio la maombi ya maadhimisho hayo kwa njia ya mitandao lilikuja kutoka katika sehemu ya Sinodi ya Kidijitali ambayo ilizindua pendekezo kupitia kiunga ambacho kitakuwa hai hadi mnamo tarehe 13 Machi 2023 katika siku ya kumbukumbu hiyo ya upapa wake.
Maombi yetu kwa Papa
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa inasomeka kuwa: “huduma ya Petro ni neema kubwa ambayo Yesu alitoa kwa Kanisa lake na lazima tuishukuru kila wakati. Kwa hiyo, maombi yetu yanapaswa kuwa zawadi bora zaidi, ili Mungu amsaidie katika huduma yule ambaye amemchagua kwa ajili ya huduma hiyo, kwa sababu juu ya mwamba huu anajenga Kanisa lake kwa muda na historia”.
Mishumaa midogo
Kwa yeyote anayetaka kushirikisha mpango huo atapata kutoka katika tovuti mwaliko wa kusali Salamu Mariamu mmoja au zaidi na mwisho tutamtumia Baba Mtakatifu ramani hiyo iliyojaa 'mishumaa midogo' inawakilisha 'Salamu Maria' wanayo mwombea, huku wakimshukuru Mungu kwa huruma zake.”
Sinodi ya kidijitali
Sinodi ya Kidijitali ni mtandao wa wamisionari wa mtandaoni ambao wameitikia wito wa Papa wa kushiriki katika safari ya sinodi kwa kufanya mazungumzo na wale wanaoishi katika bara la kidijitali na kuleta uzoefu wao wa Kikristo. Huo ni mpango unaosindikizwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.