Askofu wa Rumbek na vijana wanafika Juba kwa miguu kumpokea Papa
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Katika fursa ya Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko huko Juba nchini Sudan Kusini, na katika kumkaribisha, vijana na Askofu Christian Carlassare watafika jijini Juba wakitembea na miguu kutoka jimbo la Rumbek. Kauli mbiu ya Hija yao ni " Saafari ya amani". Ilikuwa ni Jumatano asubuhi tarehe 25 Januari 2023 ambapo Askofu wa Jimbo la Rumbek aliamka mapema na vijana wake kuanza hija yao ya miguu ambayo inadumu kwa siku tisa kamili.
Hapo tunazungumza ni mwendo wa zaidi ya kilomita mia nne zinazowatenganisha Jimbo la Rumbek na mji mkuu wa Sudan Kusini, bila kuhesabu sehemu ya kupitia ndefu na ngumu ya savanna. Kwa sababu ya utaratibu waliojipangia wa kutembea kilomenta Ishirini, au ishirini na tano kwa siku, wakisafiri kwa saa tano au sita, Askofu alisema ni juhudi kubwa lakini ambayo inastahili furaha ya kuweza kumkumbatia Papa wakati atakapofika tarehe 3 Februari 2023 katika nchi yao ambayo ni kwa mara ya kwanza kufika Papa katika taifa changa, ambalo lilipata uhuru mnamo 2011.
Kabla ya kuanza safari hiyo, Askofu Carlassare akihojiwa na mwandishi wa habari alikiri jinsi ambavyo mwanzoni, wazo la kuweka na kuunganisha baadhi ya makundi ya vijana kujiandaa kufika Juba lilikuwa linampa shida kidogo. Na hii hasa kutokana na ukosefu wa fedha na ugumu wa kutumia vyombo vya usafiri, kwa hiyo Askofu wa Rumbek alijaribu kujinasua na kile alichofikiri kwamba kilibaki kuwa mzaha tu akisema: “basi Twende kwa miguu". Lakini vijana wake walimchukulia kwa uzito. Kwa hiyo Askofu alithibitisha kwamba hakutarajia! Lakini mwisho wake mwaliko huo ulitafsiriwa na vijana kadhaa kutoka katika parokia kumi na sita kama fursa ya kweli ya kutembea pamoja. Wengi wao, kwa sababu ya uhasama baina ya makabila, kwa kawaida hawawezi hata kukutana kufanya shughuli za kawaida za kiutamaduni pamoja, lakini kumbe katika hali hiyo wataweza kufanya hivyo", alibainisha katika mahojiano hayo.
Hija hiyo imehusisha kupitia hali halisi tisa za maparokia ambapo Askofu Carlassare na vijana wake wanapeleka maneno ya amani, upatanisho na ushirika kwa kila Mkristo wanayekutana naye njiani. Askofu vile vile alieleza kwamba wangeweza kutembea katika saa zenye baridi zaidi za siku na kuutumia mchana kuhuisha jumuiya mahalia. Kwa maana hiyo alisisizita kuwa “itakuwa wakati mzuri wa imani."
Baada ya yote, yote haya yanaweza kuchukuliwa kuwa uwakilishi wa mwepesi wa njia ya upatanisho ambayo Sudan Kusini inaitwa kufanya katika jaribio la kuweka nyuma miaka mingi ya mapigano ya kikabila na ghasia ambazo zinaendelea kumwaga damu taifa hilo. Askofu Carlassare aliweka waziwazi kwamba Kwa kujitolea kwao wanataka kupitisha ujumbe kwamba Papa hakika anafika kuwasisitizia tena kuwa lazima wote wawe kitu kimoja, kama sala ya Yesu inavyosema.
Ziara ya Baba Mtakatifu pia itakuwa ni hija ya kiekumene, ikizingatiwa kwamba, Papa Fransisko atasindikizwa na Mkuu wa Usharika wa Kianglikana, Askofu Mkuu Justin Welby, na msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland, Ian Greenshields. Kwa njia hiyo Askofu Christina alisema: "Mtazamo wa kiekumene ni muhimu sana kwa sababu huko Sudan Kusini kuna uzoefu wa kipekee: Makanisa yote yameunganishwa kweli katika uinjilishaji na hiyo imewafanya kugundua kwamba uinjilishaji wenyewe umewalazimisha kuzungumza juu ya amani, haki na upatanisho.
Askofu Carlassare pia alisisitiza kuwa mchakato huo uliwafanya wawe wamoja katika Baraza la Makanisa la Sudan Kusini na kuzungumza kwa sauti moja na Serikali na katika maeneo ambayo kulikuwa na migogoro. Hapo uekumene kwa usemi wa “kitaalimungu ukawa mwili”. Vurugu hizo, ambazo Askofu Carlassare alikumbana nazo binafsi alipojeruhiwa miguuni kwa risasi chache mnamo mwezi Aprili 2021 kabla ya kuwekwa wakfu wa askofu wa Rumbek, bado zipo juu ya yote katika eneo la Upper Nile na katika Jimbo la Umoja.
Kimsingi inabakia katika maeneo ambayo zimekuwa sababu za mzozo wa 2013, uliomalizika rasmi mnamo 2020, lakini ambao bado hazijatatuliwa, na ambapo kuna umaskini, vile vile kuna watu waliohamishwa ambao hawana tena makazi ya kuishi na ambapo rasilimali zipo zimenyonywa bila kubagua, alisisitiza Askofu wa Rumbek. Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko iliandaliwa na majimbo yote ya nchi kwa sala ya kudumu na kwa katekesi nyingi zilizolenga kuifanya sura na nafasi ya Ushirika wa Papa kujulikana zaidi ndani ya Kanisa, lakini pia nje yake. Lakini Je! Papa atapata sura gani ya Kanisa? Kwa jibu la Askofu Carlassare ambaye amekuwa karibu na idadi ya watu na ambaye ameteseka kutokana na mzozo alijibu kuwa "atakutana na watu rahisi sana.Kanisa lisilo na miundo mikubwa wala taasisi lakini karibu na watu, lililojaa furaha na matumaini".