Tanzania,Abate Pambo:Miaka 134 tangu kuuawa wamisionari 3 Wabenediktini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ndugu msikilizaji na msomaji wa Vatican News leo hii kama kama ilivyo hapo zamani bado kuna haja ya kuhamasisha maoni ya umma kuhusu janga la wakristo wengi wanaoteseka na wanaouawa; Wanaonyimwa haki zao, wanaokanyagwa hadhi zao kwa sababu ya kutetea imani yao,na zaidi kuna hata baadhi ya nchi ambazo wanaruhusu dini moja tu, kwahiyo kutokuwa na uhuru wa dini na mahali pengine inaonesha jinsi gani ya kuwatesa kwa nguvu zote au kudharau kwa mantiki ya utamaduni, mbele ya wafuasi wa Yesu. Lakini pia hata kiurahisi wengine kujiamulia kukandamiza wengine kwa sababu wanaozijua wenyewe. Katika muktadha huo wamisionari wengi na watu wengi waamini wa kujitolea, zamani hata leo hii wanaendelea kukumbukwa na kuwaenzi.
Kutokana na hilo, hata Kanisa nchini Tanzania mnamo tarehe 13 Januari 2023 limeadhimishwa misa Takatifu katika kituo cha Hija huko Pugu kidogo ya mji wa Dar es Salaamu nchini Tanzania kwa kuwakumbuka wafiadini, hata kama hawajatangazwa rasimi na Kanisa kwani mchakato wao unaendelea, wamisionari 3, Wabenediktini (Mabruda wawili na Sr. mmoja). wakiwa katika utume wao wa kimisionari; lakini sio hao tu bali hata waamini wengine waliuawa wakiwemo baadhi ya watoto kati ya 40 waliokuwapo tayari katika kituo hicho cha Pugu, na ambao walikatwakatwa kikatili mnamo Dominika tarehe 13 Januari 1889, nchini Tanzania, kwa hiyo ni miaka 134 iliyopita.
Misa hiyo iliudhuliwa na viongozi wakuu wa dini Katoliki na wasio kwa namna ya pekee, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar Es Salaam, Kardinali Policarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar Es Salaamu, Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi (OFM.cap); Maaskofu wasaidizi Henry Mchamungu Kyara na Askofu Stephano Lameck Musomba, OSA., Maabati wabenediktini, wakuu wa mashirika ya kitawa ya kike na kiume, watawa na waamini walei watu wa Mungu. Katika mahubiri yake, Abate Pambo Martini Mkorwe (OSB) wa Abasia ya kibedikiti Mvimwa, alitoa historia kamili ya wamisionari hao waliomwaga damu wakitetea imani yao kwa Yesu Kristo katika watu wake wa Mungu.
Katika mahubiri hayo Abate Pambo aalisema kuwa, damu iliyomwagika ni mbegu ya uinjilishaji na hivyo kuna haja ya kuwa na wajibu wa kweli wa kiamadili thabiti ya wakatoliki, kwa misingi ya kujitokeza mawimbi ya siku hizi wakidai miujiza na waamini wakatoliki wanakuwa kama bendera fuata upepo. Abate Pambo alifafanua kuwa: “Mkatoliki mwenzangu tulia katika imani, hacha kulandalanda” kwa maana hiyo alionya dhidi ya ulaghai mwingi uliopo wa siku hizi. Aidha alisisitiza kuwa: “Wakatoliki tuna urithi mkubwa wa Sakramenti, na unakwenda kulandalanda kutafuta mafuta ya upako, miujiza ya nini? Mfano mwingine alioutoa ni kwamba kuna watu wanaokwenda kubariki hata mafuta ya nguruwe ya kupikia kwa hiyo akibainisha kuwa “ utamaduni huu wa kuiba iba kanisani ni kucheza na matakatifu”.
Abate Pambo vile vile alitoa mifano kadhaa ya wamisionari ambao alimlkumbuka na kumwekeza wa kuigwa mfano imani thabiti ya Bruda mmoja alipoona wale ‘waliojiita wanajeshi’, alikimbilia taberkulo na kula hostia ili wasije kukufuru. Ni ushuhuda mzuri wa dhati wa kuheshimu na kuabudu Bwana. Abate Pambo alifafanua zaidi kuhusu Sakramenti na visakramenti na kuwaomba waamini waheshimu kila wakati matakatifu. “Leo hii kuna ugizaji. Ugizaji wa Mafuata ya upako lakini je! Mafuta ya upako wanapaka wapi? Amekutuma nani na wakati anakupaka Anasema nini? Katika Kanisa letu limeweka vizuri kabisa namna ya kuadhimisha Sakramenti, kwa maana hiyo ni muhimu kuheshimu matakatifu.
Na wakati wa kupewa nafasi ya kutoa neno na kutambulisha wanashirika, alisema nchini Tanzania kuna Abasia za kibenedikiti 4 na kuwatambulisha maabati na Priori. Lakini pia ilikuwa ni fursa kwake, kufafanua juu ya utofauti kati yaa Abate na Askofu, wakfu na kubarikiwa na vile vile mavazi wakati wa Misa na wakati usio wa misa. Hii ni muhimu sana kwani watu waamini wengi hawajuhi. Ndugu msikilizaji na msomaji wa Vatican News, kwa mahubiri na maelekezo yote Idhaa ya Kiswahili inakuletea Mahubiri yake yote:
Mara baada ya Ibada ya Misa, Abate Pambo alipewa nafasi ya kutambulisha na kutoa neno lake. Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na Shirika hili la Kibenediktini nchini Tanzania: