Tafuta

2023.01.21 Askofu Jean Bertin Nadonye (katikati )akifuatia André Atoko(kushoto)na Romain Awolombi (kulia),wote wawili ni Makatekista katika kituo cha Mafunzo ya Makatekista kichungaji na kiikolojia,Mobokoli,jimbo la Lolo(Congo DR). 2023.01.21 Askofu Jean Bertin Nadonye (katikati )akifuatia André Atoko(kushoto)na Romain Awolombi (kulia),wote wawili ni Makatekista katika kituo cha Mafunzo ya Makatekista kichungaji na kiikolojia,Mobokoli,jimbo la Lolo(Congo DR). 

Congo-DRC,Biblia,sala na kazi ya makatekista,katika jimbo la Lolo

Kwa mujibu wa Askofu Ndongo akizungumza kabla ya tukio hilo Jumamosi tarehe 21 Januari 2023 alielezea jinsi alivyopata mwaliko kwa jimbo lake kushiriki katika Misa ya Dominika ya Neno la Mungu akiwa na makatekista wawili kutoka katika Chuo cha Mafunzo ya Makatekista kichungaji na kiikolojia,Mobokoli,Jimbo la Lolo(DRC).Makatekista walikuwa miongoni mwa wengine katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Neno ambalo ni jepesi, kitulizo cha moyo uliochoka, zawadi inayochipuka yenyewe, upanga unaopenya maishani ukituweka katika shida na hivyo kuelekeza na kubadilisha. Neno ambalo haliwezi kunyamazishwa bali lazima lishuhudiwe, likiumba mwili kwa ajili ya  kubembeleza wale wanaoteseka. Katika Kanisa Kuu la Vatican, Papa Francisko alitoa tafakari ya kina juu ya Dominika ya Nne ya Neno la Mungu ambayo yeye mwenyewe aliianzisha mnamo mwezi Septemba 2019 na kwa barua yake binafsi ya Motu Proprio Aperuit illis. Picha alizotumia Baba Mtakatifu Francisko zilikuwa wazi na zenye kuamsha hisia ili kutukumbusha kwamba utangazaji wa Injili bado ni wa dharura hadi leo hi ina , kwamba Neno halijaangaziwa katika mtindo wa kufikirika na tulivu, lakini linajua historia yenye nguvu na kwamba zaidi ya yote ni kwa kila mtu, kwa sababu wokovu ni kwa wote. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo katika mahubiri yake alitoa onyo kuwa “tusije kumkiri Mungu mwenye moyo mpana na kuwa Kanisa lenye mioyo finyu; hii ingeweza  kuwa laana,ya kukiri Mungu kwa moyo mpana na kuwa Kanisa lenye moyo mfinyu. Na isitokee tunahubiri wokovu kwa wote na kufanya njia ya kuikaribisha isiwezekane; isitokee kwamba tunajua tumeitwa kupeleka tangazo la Ufalme na kupuuza Neno, tukijitawanya wenyewe katika shughuli nyingi za ziada, au mijadala mingi.

Mmoja wa makatekista akipokea kutoka kituo cha mafunzo huko  Mobokoli jimbo la Lolo DRC
Mmoja wa makatekista akipokea kutoka kituo cha mafunzo huko Mobokoli jimbo la Lolo DRC

Katika muktadha wa maadhimisho hayo ya Dominika ya Neno la Mungu, Askofu Jean-Bertin Nadonye Ndongo, wa jimbo la Lolo nchini DRC ambaye yuko Roma aliyeshiriki  Misa Takatifu  Dominika tarehe 22 Januari 2023 katika Misa Takatifu  ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro akihojiwa  Waandishi wa habari wa Radio Vatican na Shirika la Habari za kimisionari Fides, kuhusiana na suala la ziara ya Papa Francisko ambayo inakaribia katika nchi yao alisema:  “Tunatazamia kwa hamu kubwa ziara ya Papa Francisko kwetu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika makanisa yote sala ilitungwa kwa ajili ya kusali kwa tukio hilo”. Wakati wa maadhimisho hayo  waamini wanawake na wanawaume walei wamepewa huduma ya Usomaji wa Neno la Mungu na ya Makatekista, kwa njia hiyo watu watatu walipokea huduma ya Usomaji na waamini 7 wakapokea ile ya ukatekista. Hawa ni waamini walei ambao wanawakilishi Watu wa Mungu waliolifika Italia kutoka Jamhuri ya Kidemokraisia Congo (DRC), Ufillipini, Mexico na Wales.

Askofu Jean Bertin Nadonye wa jimbo la Lolo DRC akizungumza katika studio za Radio Vatican
Askofu Jean Bertin Nadonye wa jimbo la Lolo DRC akizungumza katika studio za Radio Vatican

Kwa mujibu wa Askofu Ndongo akizungumza kabla ya tukio hilo Jumamosi tarehe 21 Januari 2023 alifafanua jinsi alivyopata  mwaliko kwa jimbo lake. Na akieleza sababu yake alisema kwamba  Baraza la Kipapa la Uinjilishaji waliona makala ambayo wao walikuwa wameandika wakielezea juu ya shule yao ya mafunzo kwa ajili ya makekista na ndipo walimtumia mwaliko ili kuwakilisha mpango huo katika Kongamamo la Kimataifa la Makatekista jijini Roma. Vile vile ilikuwa ni Baraza hilo la Kipapa la Uinjilishaji lililomjulisha kwamba Papa Francisko alikuwa anamwalika yeye na makatekista wawili ili kushiriki maadhimisho ya Neno la Mungu. Kituo cha Mafunzo cha Makatekista, cha Kichungaji na Ekolojia “Mobokoli” cha Jimbo la Lolo kilianza huduma yake ya mafunzo mnamo 2018-2019.

Katekista kutoka jimbo la Lolo alipokea msalaba kutoka mikononi mwa Papa
Katekista kutoka jimbo la Lolo alipokea msalaba kutoka mikononi mwa Papa

Ili kuelewa umuhimu wake, inabidi kuzingatia kwamba  Jimbo la Lolo linapatikana katika msitu wa Ikweta kaskazini magharibu mwa DRC  mahali ambapo alisisitiza asilimia 93 ya watu wanaishi kwa umaskini mkubwa. Karibia wakazi 200,000 waliotanyika katika vijiji 293, wametengwa kati yao kwa karibia eneo lenye kilomita 10,000 za mraba. Kuna makatekista 317 ambao wanahudumia maparokia 10.  Inabidi pia kuzingatia kwamba kila parokia inaweza kuwa na vijiji 30 ambavyo vimetengana kati yao kwa umbali mkubwa. Na inawezekana kupita hata mwaka mmoja kabla Paroko hajamaliza kutembelea vijiji vyote na hivyo makatekista wanafanya kazi hiyo ya kuongoza jumuiya ya waamini katika  ibada ya Neno la Mungu kila Dominika. Kwa mujibu wa Askofu huyo alisisitiza kuwa alipochaguliwa kuwa Askofu wa jimbo la Lolo aliona wakati wa mikutano yake ya kichungaji, umuhimu wa kuimarisha mafunzo ya makatekista na hasa  kwa kuzingatia  uhusiano wa uwepo wa makanisa mengine mengi ya kikristo yanayoibuka kama uyoga. Na pia alisema kwamba kila wakati wanaulizwa maswali kwa mfano, kwanini wakatoliki wanabatizwa wakiwa wadogo na sio wakiwa watu wazima? Kutokana na swali hilo la kila mara lilikuwa ni msukumo wa uamuzi wa kuunda shule ambayo iweze kuhakikisha mafunzo ya dhati na thabiti kwa ajili ya makatekista wao.

Kituo cha mafunzo ya Makatekista huko Mobokoli ,jimbo la Lolo DRC
Kituo cha mafunzo ya Makatekista huko Mobokoli ,jimbo la Lolo DRC

Kwa njia hiyo walianza kujenga Kituo hicho mnamo 2017, wakianzia na ujenzi wa nyumba 10 na vifaa vilivyopatikana katika maeneo na moja kwa kila parokia alikumbusha Askofu Ndongo. Wakati marafiki kutoka Shirika la ufadhili ‘Missio Aachen’ walipokwenda kuwatambela waliwasaidia kujenga upya majengo kwa nyenzo bora zaidi. Ndani ya miaka 3 wameweza kupata nyumba 10 za kukaa wanafunzi. Aidha, nyumba ya mkurugenzi na shule iliyogawanywa katika madarasa matatu, mawili ya wanawake na ya wanaume yalijengwa. Askofu Ndongo alisisitiza umuhimu wa malezi yanayotolewa kwa wanawake, ambao mara nyingi hawajui kusoma na kuandika kwamba “Wanawake, walioolewa na Katekista ambao nao kwa kupitia malezi, hayo wanapokea majiundo mawili tofauti.

Kituo cha Mafunzo ya Makatekista :hao ni wenzi baada ya kuhitimu masomo huko Bokpli Jimbo la Lolo
Kituo cha Mafunzo ya Makatekista :hao ni wenzi baada ya kuhitimu masomo huko Bokpli Jimbo la Lolo

Mbali na ile ya katekesi, pia kuna moja ya maendeleo ya binadamu yanayolenga kusoma, kushona na kozi za usimamizi wa familia. Kwa hiyo wanaporudi kijijini, wanandoa wa katekista, mume na mke, wanakuwa sio tu kituo cha kumbukumbu kwa Wakatoliki bali pia mawakala wa maendeleo ya binadamu kwa wakazi wote, hasa kwa wanawake. Malezi ya wanaume, pamoja na sehemu ya kitaalimungu na kimaadili, yanajumuisha kile kinachoitwa sehemu ya kiraia (kwa mfano juu ya haki za binadamu na kiraia), sehemu ya vitendo juu ya jinsi, kwa mfano, kutoa mafundisho ya Kikristo kwa wale ambao wanaomba kujiunga na Kanisa katoliki. Hatimaye, sehemu nyingine inajikita  kwa ajili ya maendeleo ya binadamu, ambayo inalenga katika kilimo na ufugaji. Si kwa bahati kwamba alama ya shule ni Biblia iliyofunguliwa iliyo na panga karibu nayo, chombo cha kazi cha kuvuna matunda ya dunia. Kwa ufupi, wanarejea kanuni iliyoanzishwa na  Mtakatifu Benedikto Mmnonaki  ya 'Ora et Labora” yaani 'sala na kazi' .

MAKATEKISTA JIMBO LOLO DRC
23 January 2023, 15:56