Tafuta

Sherehe za Noeli huko Nchi Takatifu Sherehe za Noeli huko Nchi Takatifu 

Tumaini jipya huko Bethlehemu kwa kupokea mahujaji wengi!

Nchi ya Israeli imewezesha kipindi cha Noeli kuwapatia ruhusa wakristo elfu 10 kati ya Ukanda wa Yordan na Gaza,ili waweze kusali katika maeneo matakatifu na kuwaona ndugu zao.Patriaki Pizzaballa amesema vurugu zinaongezeka.Padre Rami Asakrieh(OMF) Paroko wa madhabahu ya Kuzaliwa kwa Bwana: Uviko ulikuwa mbaya sana,Kanisa limejitahidi kuongeza nguvu ya uhuru wa ndani kwa waamini.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kuadhimisha Sherehe za kuzaliwa kwa Bwana bila vizingiti na kuwa na wanahija wengi sana, ndilo limekuwa tukio ambalo linafanywa uzoefu huko Nchi Takatifu, Dominika tarehe 25 Desemba 2022 na kurudia hali halisi ya kawaida, kama ile iliyokuwapo kabla ya janga la uviko- 19. Ndivyo ilivyoelezwa  na Patriaki wa Kilatino, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, na hata Padre Ibrahim Faltas, Makamu Msimimizi wa Nchi Takatifu, ambaye alitaarifu kuwa katika siku kuu ya Noeli, Mamlaka ya Israeli, iliwezesha kutoa ruhusu kwa Wakristo wa kati ya Jordan na ukanda wa Gaza yenye muda hadi tarehe 20 Januari 2023 ili wanahija hao waweze kwenda Bethlehemu na maeneo mengine matakatifu kusali na kuwaona ndugu zao.

Maadhimisho ya Usiku wa Noeli Nchi Takatifu

Katika Pango la Kuzaliwa kwa Yesu wakati wa usiku wa Noeli, maadhimisho yaliongozwa na Padre Francesco Patton. Kwa maana hiyo katika mji idadi ya wahahija imerudi kuwa kubwa kama ilivyokuwa  mwaka 2017 na mamlaka inatarajia kuendeleza kukua  kwa haraka hadi kufikia hali kama ilivyokuwa 2019. Na katika kusheherekea misa ya usiku  huko Bethlehemu, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Pierbattista Pizzaballa amesema vurugu zinazidi kuongezeka. Vurugu utafikiri zinageuka kuwa lugha yao msingi. Katika misa hiyo iliudhuriwa hata Rais na Waziri Mkuu wa Palestina, Mahmoud Abbas na Mohammad Ibrahim Shtayyeh.

Patriaki Pizzaballa: Siasa iwe huduma ya Nchi

Patriaki Pizzaballa alielezea kwa mara nyingine kuhusu wasiwasi kwa ajili ya serikali mpya ya Israeli, mahali ambapo kuna hatari ya kuvunja kile ambacho tayari ni kidhaifu, yaani kuhusu msimamo  kati ya jumuiya tofauti za kidini na kikabila ambazo zinaunda jamii. Kwa mujibu wake alibaninisha kuwa Sera ya kisiasa zina jukumu la  kuhudumia Nchi na wakazi wake, kufanya kazi kwa ajili ya maelewano kati ya jumuiya tofauti za kijamii na kidini za nchi, na kutafsiri katika matendo ya dhati na chanya katika eneo, lakini sio kuchochea migawanyiko, au mbaya zaidi chuki na ubaguzi. Patriaki Pizzaballa akiendelea alisema kuwa mwaka huu hasa wameona kukua kwa ghasia katika barabara, mitaa na viwanja vya wapalestina na kuwa na idadi kubwa ya vifo ambavyo viliwahi kuonekana miaka kumi  ya nyuma iliyopita. Hiyo ni ishara ya wasiwasi ambao unaongeza mivutano kisiasa na kukua kwa matatizo hasa ya vijana wao kwa kutafuta  suluhisho ambalo linaonekana kuwa mbali sana kutokana na migogoro inayoendelea.

Wakati ujao wa matarajio makubwa

Aliyezungumzia matumaini makubwa ya wakati ujao pia ni Padre Rami Asakrieh, Makamu msimamizi wa wafransiskani huko Nchi Takatifu na Paroko wa Bethlehemu katika Kanisa la Mtakatifu Katarina, mahali palipo na madhabahu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Akizungumza katika Radio Vatican, alisema kuwa, baada ya kumalizika Uviko, kwa sasa wanayo matarajio. Katika wakati huu, wanaona makundi mengi ya wanahija hivyo ni Noeli iliyojaa watu kama zamani. Matashi yake mema  ya Padre ni kwamba inawezekana kusimamisha kweli hata vita katika wakati huu kama vile ya Ukraine, mbali na mambo ambayo wao wanaishi katika  Nchi, na ambayo yamewakuta kwa uzito hata wakristo wa Nchi Takatifu, ambao tayari wamejaribiwa. Na mbaya zaidi ilisababishwa na Janga la Uviko.

Katika maelezo ya  Padre Assakrieh na Vatican News amebainisha kwamba anafikiria nyakati zilizopita kuwa  zilikuwa mbaya sana za vita na mbaya zaidi kwa kila mzozo kwa sababu zamani angalau walikuwa na wafadhili, walipokea msaada na watu wengi walikuwa na uwezo wa kusaidiwa hasa Wakristo wa Nchi za Ulaya. Kutokana na mgogoro wa dunia wa Janga la Uviko, kwa aliyekuwa anatoa ameanza kufanya hivyo lakini kidogo, kwani virusi vilishambulia uchumi wote, ambapo umesababisha ugumu wa maeneo ya Ulinzi wa Nchi Takatifu. Utalii ndio rasilimali msingi huko Bethlehemu, kwa maana wengi wanafanya kazi kuanzia maduka, hadi sokoni, saloon, njia za usafiri, hoteli, wanaongoza watalii, kwa wastani  yote  hayo yanahusisha utalii. Janga lilisababisha wote kuishi kipindi kigumu zaidi ya hata ya vita.

Jitihada za Kanisa

Kanisa kwa muda huu amesema  linaitwa kutoa nje ile nguvu yake ili kukaa karibu na watu, katika kutafuta kuongeza nguvu ndani za kibinadamu, kwa sababu iunde watu wa imani, watu wenye nguvu ndani, watu wanyenyekevu ambao wanakubali kile ambacho kinakuja, na ambao wanashukuru Mungu, ambao wanaheshimu Bwana katika maisha yao  na wanaoamini Mungu mpaji,  ambaye anasaidia kuwa angalu kidogo na uhuru wa ndani, kwa sababu ule wa nje amesema una vikwazo na kwa njia hiyo waongeza nguvu kwa watu hao kwa njia ya Neno la Mungu,  kwa sakramenti na shughuli za kichungaji.  Shughuli za huko Bethlehemu ni nyingi sana, ambazo zimekabidhiwa kwa makundi ya vijana, makundi ya skout, ambao hujikita kuandaa sherehe mbali mbali kama vile Noeli na kama makundi mengine ya sala. Kwa maana hiyo wanatafuta kufanya kila liwezekanalo, kwa kuwapa wakirsto maisha ya hadhi ili waweze kuishi kwa utulivu na familia na kuvumilia hali hiyo ya hofu na ukosefu wa msimamo, amehitimisha Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Catarina Nchi Takatifu.

27 December 2022, 12:03