Tafuta

Papa Mstaafu  Benedikto XVI: Akiwa na umri wa miaka 95 ameaga dunia akiwa katika Nyumba ya monasteri jijini Vatican Jumamosi 31 Desemba 2022. Papa Mstaafu Benedikto XVI: Akiwa na umri wa miaka 95 ameaga dunia akiwa katika Nyumba ya monasteri jijini Vatican Jumamosi 31 Desemba 2022. 

Tanzania-TEC:Tunamshukuru Mungu kwa maisha ya Mja wake

Katika telegramu za salamu za rambi rambi zilizofika kutoka ulimwenguni kote,Askofu Mkuu Nyaisonga,Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) anatoa pole za dhati kwa Baba Mtakatifu Francisko na Kanisa zima ulimwenguni kufuatia na kifo cha Papa Mstaafu Benedikto XVI kilichotokea tarehe 31 Desemba 2022.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Ulimwengu mzima umepokea kwa masikitiko makubwa habari za kifo cha Papa Mstaafu Benedikto XVI kilichotokea alfajiri saa 3.34,  Jumamosi tarehe 31 Desemba 2022. Kufuatia na kifo hicho,viongozi wengi wa Kanisa na hata kijamii, wametuma salamu zao za rambi rambi. Miongoni mwa salamu hizo ni Askofu Mkuu Gervaz J. Nyaisonga, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Tanzania (TEC) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki Mbeya, Tanzania ambaye amebainisha kwamba: "ninatoa salamu za rambi rambi za dhati kwa Baba Mtakatifu Francisko na Kanisa zima na tunamshukuru Mungu kwa maisha mazuri ya mja wake. Mungu amjalie pumzo la Milele Mbinguni".

Wengine ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Munich na Frisinger alikokuwa anatoka Papa Mstaafu, na  wanamwombea Papa Mstaafu pumziko la milele; Rais wa Baraza la maaskofu Austalia ametuma salamu za rambi rambi, kwa niaba ya Kanisa zima; Baraza la Maaskofu Italia(CEI); Baraza la maaskofu Hungaria; Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya; na Baraza la maaskofu Ujerumani. Aidha ujumbe kutoka kwa Askofu Mkuu Justin Welby wa Kanisa la Kianglikani Canterbury, Uingereza na  Baraza la Maaskofu katoliki wa  Uingereza na Walles.

Umoja wa Wabudha Italia pia wametuma ujumbe wao wakionesha uchungu na kuungana na Kanisa Katoliki la Italia na ulimwengu kwa ajili ya kifo cha Papa Msfaafu Benedikto XVI. Wanamkumbuka alivyo kuwa na wazo la kina na utafiti wa kitaalimungu na umakini wa majadiliano ya kidini. Aidha, "Kimo chake kama msomi mzuri kililingana na upole wake. Kujiuzulu kwake katika kiti cha upapa ilikuwa ni ishara iliyoshangaza ulimwengu mzima na jumuiya ya waamini katika imani yoyote ile”, wamebainisha.  Na ujumbe mwingi sana kutoka katika jamii mbali mbali duniani, viongozi wa vyama na kisiasa wameelezea masikitiko na shukrani kwa Papa mstaafu kwa yote aliyotendea Kanisa lote, dini zote bila ubaguzi na kwa jamii nzima.

SALAMU ZA RAMBI RAMBI
31 December 2022, 15:18