Papa Benedikto XV alishauri maaskofu kuwa seminari ziendane na kanuni
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mnamo tarehe 30 Novemba 1921, Papa Benedikto XV aliwatumia Maaskofu wa Chekoslovakia barua yake kwa kuwapa ushauri na wito kwamba wao wanapaswa kusimamia utendaji sahihi wa seminari na kwamba lazima ziendane na maagizo ya kanuni za sheria. Kutokana na hiyo, tarehe 30 Novemba 2022 ilikuwa ni kumbu kumbu ya miaka 101 tangu kuchapishwa kwa barua hiyo ya kipapa kwa maaaskofu hao. Katika barua hiyo Papa Benedikto XV aliandika kuwa: “Tumejifunza kwamba sababu ya kwanza ya maovu tunayolalamikia ni ukweli kwambamakasisi, kwa sehemu kubwa, hawafundwi vya kutosha katika akili na kiroho, na hii inategemea na seminari za makasisi ambazo zinapaswa kuendana kikamilifu na ukamilifu wa maagizo ya kanuni takatifu, badala yake zinakutwa karibu kuwa na kasoro. Kwa hiyo barua yetu hii haikusudii kitu chochote isipokuwa kuwashauri kwa nguvu zote za kuwandaa kwa malezi sahihi makleri wenu; kwa njia hiyo mtakuwa na watu wakamilifu hata kwa afya ya watu.”
Kuhani lazima awe balozi, mhudumu wa Yesu na mweka hazina ya mafumbo
Kwa hakika hali ya seminari ilikuwa mada kuu katikaUpapa wa mbenediktini huyo ambaye alikuwa hapo awali amewaalika Maaskofu kuhusu muktadha huo. Kwa hiyo Papa aliandika tena: “Katika barua na hati za Vatican kuhusu uklero, alisisitiza tena, huku akinukuu Papa Leo XIII, kwamba ukweli unasisitizwa mara nyingi kwamba kuhani hawezi, kutokuwa kama balozi, kama mhudumu wa Kristo, kama mweka hazina wa mafumbo ya Mungu na kwa ajili ya huduma yake takatifu, ikiwa hajapata ujuzi wa kutosha wa sayansi takatifu na ya kimungu, na ikiwa hana wingi wa utauwa ambao kwa huo anakuwa mtu wa Mungu. Kwa hiyo ni lazima kuhani awe na ukweli na fadhila za wema kiasi cha kutokuwa na hitilafu au dosari yoyote.”
Kuhani afanye Mapenzi ya Mungu ya 'ili wote wawe Watakatifu'
Papa Benedikto XV katika barua hiyo anaeleza maaskofu kwamba: “Tunawaomba mjitoe ili kusiwe na jimbo katika nchi yenu ambayo haina Seminari; na mahali ambapo tayari ipo, hakikisheni inaendana kulingana na kanuni za kanoni mpya ya sheria. Na ikiwa kuna vizingiti vya upanuzi au umaskini wa baadhi ya majimbo hauruhusu uwepo wa taasisi kama hiyo, itakuwa vizuri kutumia kanuni zilizowekwa kwa seminari ya pamoja ya kimajimbo. Kwa hiyo Seminari ya Jimbo inahitaji kwa usahihi umakini na jitihada ya hali ya juu ya Askofu. Askofu, kwa maana hiyo, ili aweze kufuata na kutia moyo kwa uangalifu wa ubaba wa maendeleo ya wakleri wake katika njia ya ukweli na uaminifu, atafanya jambo bora sana kama ile asemayo Mwalimu Mtakatifu Alphonsus, kwamba: "ikiwa ataingia Seminarini mara kadhaa, ikiwa atawachochea wanafunzi, kwa mashauri yanayofaa, kwa ibada ya fadhila na barua, ikiwa pia ataingilia kati duru na mijadala ya kishule, ambapo atastaajabisha kuwachochea katika kuiga kwenye muktadha kati wa Elimu. Hivyo itatokea pia kwamba Askofu, akiisha kuwajua wapadre wake kikamilifu na kibinafsi, hatawaweka mikono yake juu yao kwa haraka, bali atawapatia ukuhani wale waishio kwa moyo wa Yesu, yaani, wale wanaoheshimu huduma yao wenyewe kwa mapenzi ya Mungu ambayo ni wote wawe watakatifu”.