Tafuta

Burkina Faso: Wanawake mara nyingi ni waathirika katika njia za uhamaji. Burkina Faso: Wanawake mara nyingi ni waathirika katika njia za uhamaji. 

Kongamano Ouagadougou:Daima wanawake wanazidi kuwa katika wimbi la uhamaji

Limefanyika kongamano nchini Burkina Faso kuhusu mada ya wimbi la uhamaji ambao unazidi kuwaona wanawake.Zaidi na zaidi wanahama bila kutegemea familia zao,wakivutiwa na mahitaji makubwa ya kazi katika sekta zinazotawaliwa na wanawake,kama vile kazi za nyumbani na huduma za afya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wanawake zaidi na zaidi ni sehemu ya mtiririko wa wahamaji kutoka Afrika. Haya ndiyo yameibuka kutokana katika Kongamani lenye kuongozwa na mada ya “Wanawake, jinsia na uhamiaji” huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika Katoliki kwa ajili ya Maendeleo na Mshikamano(OCADES, Caritas Burkina Faso) na Shirika Welthungerhilfe, lisilo la Kiserikali (NGO) huko Ujeruman, katika mfumo wa utekelezaji wa Mradi wa Appui kwa ajili ya Ulinzi wa wahamiaji walio katika hali ngumu kwenye barabara za uhamaji wa Sahel(PROMISA). PROMISA inahamasishwa na Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya Afrika (EUTF) na unasimamiwa na Caritas Uswiss (CaCH), pamoja na Shirika la Huduma Katoliki (CRS), OCADES, Caritas Mali na Welthungerhilfe (WHH).

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti na Mafunzo kuhusu Maendeleo ya Kibinadamu, Sista Jeannine Sawadogo, katika hotuba yake ya utangulizi alibainisha kwamba kwa muda mrefu,na ingawa wanawake hawakuwakilishwa kidogo sana kuliko leo hii katika mtiririko wa watu wanaohama duniani, jinsia ilipuuzwa. Kwa mfano Nchini Burkina Faso wanashuhudia bila msaada, uhamaji wa binadamu wenye sifa mpya za wahamiaji, yaani wanawake. Kwa maana hiyo inafaa wazingatie hali ya wanawake wahamiaji na hasa afya zao.

Katika Kongamano hilo naye Dieudonné Guiguemdé, mkuu wa OCADES, alisisitiza ambavyo wanatambua kwa sasa uhamiaji zaidi na zaidi una sura ya kike. Hivyo akauliza swali je, katika sera za ngazi ya kitaifa, mikakati ya uhamiaji, rafiki kwa wanawake, jinsia inazingatiwaje? Hili ndilo linalohalalisha jopo hilo kujaribu kutafakari suala la jinsia na uhamiaji; kwa kuzingatia kuwa wanawake mara nyingi ni waathirika katika barabara za uhamaji. Kwa hiyo ni lazima wafanye kazi ili kuwasaidia kupata ulinzi bora zaidi; si kwa sababu wao ni wanawake kwamba ndiyo maana lazima wachukuliwe kuwa ni watu wa kudanganywa, watu wenye lengo la kukidhi matakwa yoyote, bali wana hadhi ya kuhifadhi na kulindwa.

Wanawake zaidi na zaidi wanahama bila kutegemea familia zao, wakivutiwa na mahitaji makubwa ya kazi katika sekta zinazotawaliwa na wanawake, kama vile kazi za nyumbani na huduma za afya. Sera ya uhamiaji haijabadilika kulingana na mwelekeo huo wa kimataifa. Hakuna uelewa mpana wa utaratibu wa jinsi ya kutathmini athari za sera za uhamiaji kwa wanaume na wanawake. Mbali na hayo, wanawake na wasichana mara nyingi hubakia kuwa wahanga wa dhuluma na unyanyasaji wa kila aina katika mchakato wa njia ya wahamaji na baadaye  katika nchi wanakokwenda.

Waandaaji wa mkutano huko  Ouagadougou pia kandoni  waliandaa mkutano wa siku mbili, tarehe 28 -29 Novemba 2022, na vikosi vya usalama vya nchi hiyo(Forces de défense et de sécurité FDS), yaani Kikosi kazi cha kulinda na usalama) ili kuimarisha uelewa na uwezo wa kiutendaji wa SDF juu ya usafirishaji haramu wa binadamu, ambao ni biashara haramu ya binadamu, na kuelewa uhusiano kati ya jinsia na uhamiaji. Alifafanua hayo Katibu Mkuu wa OCADES,Padre  Constantin Séré, alibainishwa kwamba suala la ulinzi wa wahamiaji linabaki kuwa la sasa,  licha ya shida ambayo nchi yao inapitia (...). Na wahamiaji wanapofika salama katika nchi wanakokwenda, majaribu wanayopitia njiani yanaweza kuathiri uadilifu wao wa kimwili au afya yao ya akili.

Wanawake Burkina Faso
02 December 2022, 13:04