Tafuta

2022.12.28 Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Kinshasa,amejindikisha kupiga kura katika kituo cha kuajiandikia cha Mtakatifu  Raphaël de Limété - Kinshasa,Jumanne 27 Desemba 2022. 2022.12.28 Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Kinshasa,amejindikisha kupiga kura katika kituo cha kuajiandikia cha Mtakatifu Raphaël de Limété - Kinshasa,Jumanne 27 Desemba 2022. 

Congo DRC:Kard.Ambongo anawaalika wazalendo kujiandikisha kupiga kura 2023!

Kujiandikisha kupiga kura ni jukumu muhimu la kizalendo na kitendo kikubwa cha uwajibikaji.Ndio mwaliko uliozinduliwa kwa washirika wake na Askofu Mkuu wa Kinshasa,naakiwa mstari wa mbele amejiandikisha kama wananchi wengine.Pia amezungumzia juu ya kuwasili kwa Papa nchini kwao:"uwepo wake utatusaidia kurejesha imani katika siku zijazo"

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Askofu mkuu wa Kinshasa, Kardinali Fridolin Ambongo, Jumanne tarehe 27 Desemba 2022 amekwenda na  kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mnamo mwaka 2023. Kardinali alikwenda katika kituo cha CENI ambacho ni cha tume huru ya taifa ya uchaguzi, kilichoko ndani ya shule katoliki ya Mtakatifu Raphaël, na jina lake lilijumuishwa katika orodha za wapiga kura.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kishansa Kardinali Ambongo akijiandikisha kupiga kura ya uchaguzi 2023
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kishansa Kardinali Ambongo akijiandikisha kupiga kura ya uchaguzi 2023

Kwa upande wa Kardinali Ambongo amebainisha kuwa “chaguzi daima zimekuwa chanzo cha matumaini kwa wakazi wa Congo kwa kiwango kikubwa cha ubora katika usimamizi wa nchi. Ikiwa Kanisa la Congo daima limeshiriki katika elimu ya kiraia na uchaguzi, hasa kupitia mafunzo ya waangalizi wa uchaguzi ni kwa sababu inaamini kuwa uchaguzi mzuri unaweza kufungua matarajio mapya kwa nchi, na kwa wakazi. Kwa hiyo kujiandikisha “ni ishara ndogo, lakini yenye kuwa na matokeo, alisema Kardinali Ambongo, huku akiwatumia watu ujumbe wa uhamasishaji, na mwaliko wa kujiandikisha kwa wingi. Kwa hiyo amesema kuwa “ni fursa kwa kila raia kutumia haki yake ya kuchagua mtawala wake wakati wa uchaguzi”.

Matumaini ya wagombea kuwa waaminifu na mipango yao

Kwa upande wa wagombea, Askofu mkuu wa Kinshasa anayo matumaini kwamba watakuwa waaminifu, wabebaji wa mipango mizuri ya kijamii kwa nchi na idadi ya watu ambayo imekuwa ikiteseka kwa zaidi ya miongo mitatu.  Kufanya siasa, alisisitiza, ni mpango wa kimaadili. Kwa upande wa Kardinali Ambongo, pia akizungumzia juu ya ziara ya Papa Francisko kwa mwezi ujao 2023, amebainisha kwamba ni kichocheo na faraja kwa idadi ya watu na zaidi ya kukiri kidini, wakazi wote wa Congo wanamngoja na uwepo wake utasaidia kurudisha imani katika siku zijazo. Kwa 2023 Askofu mkuu wa Kinshasa amewatumia  ujumbe wa matumaini kwamba kile ambacho wanapitia Wakongo ni hali ya ugumu wa kupindukia, huku kukiwa na mateso, njaa, mauaji, hasa mashariki mwa nchi hiyo ambapo watu hutupwa mitaani, wakifukuzwa makwao, kazini na maisha yenyewe na watu ambao wamepoteza upendo wa kaka na dada zao.

Mivutano na matatizo katika mikoa ya Magharibi wa nchi

Hali kadhalika Kardinali Ambongo, alisisitiza, kwamba kuna mivutano na matatizo pia katika maeneo ya mikoa ya magharibi, katika eneo la Kwamouth na mazingira yake. Licha ya hali hiyo ya matatizo, Kardinali amewaalika watu wasipoteze matumaini na waandae maisha yao ya baadaye kwa uwajibikaji, kwa sababu anaamini kwamba zaidi ya haya machafuko yanayotokea kwa mwanadamu, Mungu yuko hatimaye mwisho wa njia na ataingilia kati kwa siku zake. Kardinali Ambongo pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu tabia ya kupora ardhi ya Jimbo na kwa mashirika ya kitawa, ardhi zilizonunuliwa kabla ya uhuru. Kwa hiyo amesema Kanisa ni mwathirika wa kunyang'anywa ardhi kwa misingi ya vyeti vya uongo na hii, hutokea pia kwa watu wa kawaida ambao hawana njia ya kujitetea. Kwa mujibu wa Mkataba wa Mfumo kati ya Vatican  na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jimbo kuu ya Kinshasa limeshauriana na mamlaka, ambao wametoa maagizo ya kutatua tatizo hilo.

Chaguzi daima ni chanzo cha matumaini

Kwa upande wa Kardinali Ambongo amebainisha kuwa “chaguzi daima zimekuwa chanzo cha matumaini kwa wakazi wa Congo kwa kiwango kikubwa cha ubora katika usimamizi wa nchi. Ikiwa Kanisa la Congo daima limeshiriki katika elimu ya kiraia na uchaguzi, hasa kupitia mafunzo ya waangalizi wa uchaguzi ni kwa sababu inaamini kuwa uchaguzi mzuri unaweza kufungua matarajio mapya kwa nchi, na kwa wakazi. Kwa hiyo kujiandikisha “ni ishara ndogo, lakini yenye kuwa na matokeo, alisema Kardinali Ambongo, huku akituma watu ujumbe wa uhamasishaji, na mwaliko wa kujiandikisha kwa wingi. Kwa hiyo amesema kuwa “ni fursa kwa kila raia kutumia haki yake ya kuchagua mtawala wake wakati wa uchaguzi”.

 

28 December 2022, 15:57