Tafuta

2022.12.17  Papa Francisko amefikisha miaka 86 ya Kuzaliwa. 2022.12.17 Papa Francisko amefikisha miaka 86 ya Kuzaliwa. 

Celam,Miaka 86 ya Papa:zawadi na kisima cha tumaini kwa Kanisa na ubinadamu!

Katika siku ambayo Papa Francisko ameadhimisha miaka 86 ujumbe wa shukrani kwa watu ambao wanatoa maisha yao kwa ajili ya watu maskini kati ya maskini.Baraza la Maaskofu Amerika Kusini na Visiwa vyake wamemtakia matashi mema Papa.Baraza la Maaskofu Italia wanahaidi kuendelea kumwombea.

Na Angella Rwezaula-Vatican.

Ilikuwa mnamo tarehe 17 Desemba 1936 ambapo George Mario Belgorglio yaani Papa Francisko alizaliwa huko Buenos Aires, Argentina na familia moja ambayo ilihamia huko kutoka katika mkoa wa Piemonte nchini Italia. Kutokana na kumbukizi hilo, tarehe 17 Desemba 2022 akiwa anafikisha miaka 86 ya kuzaliwa Papa Francisko, Ujumbe mbali mbali umetolewa kwa kumtakia matashi mema. “Katika Siku ya kuzaliwa kwao tuna sababu nyingi za kusherehekea na kushukuru kwa ajili ya maisha yako, mafundisho na ushuhuda usiofutika, zawadi ya kweli na chemchemi ya matumaini kwa Kanisa na kwa wanadamu. Kutoka  katika Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini na visiwa vya Carribien tunaelezea upendo wetu na matashi mema ya  dhati. Tunainua maombi yetu kwa Mungu wa uzima kwa nia yako, na tunakushukuru kwa huduma yako ya Upapa yenye matunda ambayo imetoa maisha kwa njia nyingi za kukutana, kusikiliza, utambuzi, ushirika na udugu wa ulimwengu wote, kwa usikivu maalum kwa  pembezoni zetu za umbali kijiografia na maisha”.

Papa amefikisha miaka 86 ya kuzaliwa
Papa amefikisha miaka 86 ya kuzaliwa

Rais huyo kwa niaba ya Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (CELAM) ameandika hayo katika ujumbe huo ili kumpongeza kwa siku kuu yake ya kuzaliwa. Maaskofu hao wanatoa shukrani wakisema: “Asante, Baba Mtakatifu, kwa msaada wako na mwongozo wako wa kiroho kwa Kanisa letu la Amerika ya Kusini na Caribbien, kwa ukaribu wako na mwongozo wakati huu tunapoelekea Kanisa la Sinodi linalotakiwa kutoka nje. Unaendelea kutegemea kujitolea kwetu kichungaji na kuinjilisha pamoja na Watu wa Mungu.”

Cei Miaka 86 ya Papa:mkumbatia wa nguvu na wa kweli wa Makanisa ya Italia

Na wakati huo huo, ujumbe wa matashi mema kutoka kwa Rais  Baraza la Maaskofu nchini Italia (CEI) kwa niaba ya maaskofu wote anaandika kuwa “Kukumbatia kwa nguvu na dhati kwa Makanisa nchini Italia. Bado machoni mwetu tunayo ile picha ya uso wako ukiwa unatokwa machozi, ulipokuwa ukisali kwa  Bikira Maria, wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili, katika kutimiza tendo la kimapokeo katika Uwanja wa Hispania, Roma. Kwa sauti yako, iliyovunjwa na mhemko, na katika kichwa chako kilichoinama, tuliona uchungu na uchungu kwa tamasha vita ambavyo vimefunika Ukraine na giza lake. Siku chache kabla ya Noeli, furaha katika uso wa maisha ambayo huzaliwa Bwana inatishia kugeuka kuwa mateso kwa  walio wengi na  vifo vingi sana. Baba Mtakatifu, tunalia pamoja nawe, tukiwa na hakika kwamba Bwana ajaye atawafariji watu wake na kuwafunga jeraha zao.” Urais wa CEI kwa maana hiyo wanamuhakikishia kuwakabidhi wote chini ya  ulinzi wa Mama Yetu Bikira Maria  “Jumuiya zetu, wazee na watoto, familia, vijana, wagonjwa na masikini, waliopoteza kazi zao, walio peke yao, walioangukia katika hali tete, na  wale wanaopata ujasiri wa kutumaini. Pamoja Papa , ambaye unatuongoza kwa hekima na subira, tunatembea katika barabara za ulimwengu ili kukutana na dada na kaka zetu, ili kuweka alama za  njia za upendo na umoja”.

Heri ya Miaka 86 ya Kuzaliwa kwa Papa Francisko
17 December 2022, 15:53