Caritas Italia:Hatua za kupambana na umaskini na kuwasindikiza watu!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mkurugenzi wa Caritas Italia, Padre Marco Pagniello, akifafana juu ya mada ya mapato msingi, wakati wa kufunga semina kuhusu hatua za kupambana na umaskini iliyoongozwa na kaulimbiu: ”Endana na mada na mahitaji: sera dhidi ya umaskini nchini Italia, iliyofanyika tarehe 1 Desemba 2022, huko Roma, alisema kwamba: “ili kuwa makini na kuepuka kutangaza kauli mbiu tu, tunaendelea kuchunguza mada, kusikiliza hali halisi tofauti za ndani na kuendeleza uzoefu ambao tumekusanya. Ukweli kwamba Serikali yenyewe imejipa mwaka mmoja ili kufanya mageuzi ya Mapato ya Uraia inayo tuwezesha kuendelea na majadiliano na mchakato ulioanza kwa matumaini ya kuweza kuendeleza na kutoa mapendekezo madhubuti na ya kufikirika pamoja na vyombo vingine vya Kanisa la Italia vinavyohusika nasi kuhusu masuala ya kazi na kijamii na kiafya”. Baada ya yote, Mapato ya Uraia, alisema Padre Pagniello, “sio zana pekee tuliyo nayo kwa vita dhidi ya umaskini. Na hatupaswi kamwe kusahau kwamba mtu anayetugeukia sio tu mtoaji wa shida, lakini juu ya haki na rasilimali zote. Kazi ya Caritas na Jumuiya ya Kikristo kwa ujumla ni kusindikizana na watu, ili asiwepo yeyote atakayebaki nyuma na kila mtu aweze kuwa mhusika mkuu wa mabadiliko kuelekea jumuiya zinazoendelea kuwashirikisha na kusaidia watu”.
Wakati wa semina hiyo, Caritas Italia pia iliwasilisha matokeo ya kwanza ya uchambuzi wake wa vipengele vinavyopaswa kuzingatiwa katika kuingilia kati kwa mkakati wa kupambana na umaskini ambao unaendana na sifa zinazochukuliwa na hali hiyo katika nchi yao, kwa kuzingatia utekelezaji wa hatua za kukabiliana na umaskini ambao unawakabili. Na kwa maana hiyo hivi karibuni Italia wamekuwa na mtazamo kulinganisha katika ngazi ya Ulaya kikundi kazi ili kufafanua kile kilichoibuka, na kukielezea katika mapendekezo madhubuti. Hata hivyo hatua ya kwanza asubuhi iliona hotuba za Massimo Baldini kutoka (Chuo Kikuu cha Modena) kuhusu ‘Wapokeaji wa hatua ya kukabiliana na umaskini’, na Daniele Pacifico (OECD) kuhusu ‘Muundo wa kipimo: umaskini na/au kazi? Uzoefu wa nchi zingine barani Ulaya’, na mratibu wa mradi wa Caritas Italiana, Nunzia De Capite, alijikitia juu ya ‘Ustawi wa ndani kwa ushirikishwaji wa kijamii: vikwazo vya sasa na jinsi ya kuvishinda’, na Giulio Bertoluzza (mshiriki wa Caritas Italia) juu ya: “Njia za mageuzi: vikwazo na fursa” na Cristiano Gori (Chuo Kikuu cha Trento na mkurugenzi wa kisayansi wa mpango) juu ya “Muhtasari wa majibu ya sasa”.
Kutokana na kulinganisha mada hizo uliibuka uthibitisho kwamba Mapato ya Uraia yanawasilisha mfululizo wa masuala muhimu ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi. Kuna “watu maskini” wengi ambao hawapati mapato na kinyume chake. Lengo linahitaji kufafanuliwa kwa upya. Na mtu anaweza, lazima pia wafikirie kwa utulivu juu ya tofauti katika kiwango cha eneo. Ni muhimu kwamba hatua dhidi ya umaskini ni matokeo ya majadiliano yenye sauti nyingi, ya mchakato ulioelezwa. Ni suala la kutenga muda wa kutosha kwa awamu ya kubuni ya mageuzi, kubuni maelezo ya mchakato wa utekelezaji tangu mwanzo, kutumia ujuzi uliopo wa msingi wa mageuzi, kusikiliza watendaji mbalimbali wa taasisi na kijamii, mafunzo kwa ajili ya mchakato wa mageuzi yanashirikishwa na kutilia maanani yaliyo mema na kuchukua hatua kwa uthabiti katika vigezo vichache vya kimsingi.