Harakati la Shirika la Kipapa kwa ajili ya Msaada wa kanisa Hitaji Harakati la Shirika la Kipapa kwa ajili ya Msaada wa kanisa Hitaji  

ACS:Kifurushi cha msaada kwa ajili ya kudhibiti mgogoro wa nishati Ukraine

Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji(ACS)limeidhinisha kifurushi cha msaada kusaidia wananchi wa Ukraine ili kukabiliana na tatizo la nishati.Mashambulizi ya makombora ya Urussi na kuwasili kwa msimu wa baridi katika mikoa isiyo na miundombinu ya joto itasababisha idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani kuteseka kwa baridi hasa watoto,wanawake na wazee.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Huko Nchini Ukraine itakuwa vigumu sana kuishi kipindi cha  baridi bila nishati na kwa joto ambalo linaweza kushuka hadi -20°. Kwa sababu hiyo, shirika la kipapa la Misaada kwa Kanisa linalohitaji(ACS) limeidhinisha kifurushi cha msaada ili kukabiliana na tatizo la nishati. Mashambulizi ya makombora ya Urussi na kuwasili kwa msimu wa baridi katika mikoa isiyo na miundombinu ya joto itasababisha idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani kuteseka kwa baridi, wale ambao watakaolipa gharama zaidi ya yote watakuwa watoto na wanawake ambao waume zao wanahusika moja kwa moja  au wahanga wa mzozo unaoendelea. Amesema hayo Bwana Alessandro Monteduro, mkurugenzi wa  Shirika la Kipapa la Msaada wa Kanisa Hitaji (ACS) Italia. Kulingana na serikali ya Ukraine, asilimia 50% ya mitambo ya nishati imeharibiwa. Mashambulizi ya hivi karibuni ya ndege zisizo na rubani za Urussi hayalengi malengo ya kimkakati ya kijeshi, badala yake yana lengo la kufanya maisha ya kila siku ya Waukraine kuwa magumu zaidi alifafanua Monteduro na kwa sababu hiyo mfuko umeidhinisha mfululizo wa mipango ili jiko la usambazaji na jeneretor, kutia ndani jeneretor ndogo 40 kwa ajili ya Donetsk, eneo ambalo wamekamatwa mapadre wawili na askari wa Urussi.

Mpango wa kubadilisha mfumo jito katika parokia tatu huko Kharkiv

Pia kuna mipango ya kubadilisha mifumo ya joto katika parokia tatu, nyumba mbili za watawa, makazi ya askofu, nyumba ya parokia na seminari ya Ternopil. “Tutanunua majiko ya kuni hasa kwa Jimbo la Kharkiv-Zaporizhia, mashariki mwa Ukraine, kilomita 30 tu kutoka mpaka wa Urussi, ambapo majira ya baridi ni baridi sana”. Wasiwasi juu ya baridi kali ilimfanya Askofu wa Jimbo la Kilatini la Kharkiv-Zaporizhia kuomba msaada kutoka kwa Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji ACS, ili kuepusha matokeo makubwa, yanayoonekana baridi iko karibu. “Itakuwa changamoto kubwa kwa joto la nyumba na kupika chakula, kwa sababu si kila mtu hana upatikanaji wa umeme au gesi. Watu wengi wamekuja kwetu wakiomba msaada”, askofu  Pavlo Honcharuk aliliambia  shirika hiliACS.

Ombi la Msaada hata katika Seminari ya Ternopil

Mbele ya kukabiliwa na  uhaba wa umeme na gesi, wengi wanatafuta kubadili mifumo tofauti ya joto. Mkuu wa seminari ya Ternopil, Padre Ivan Rymar, ni mmoja wa watu wengi ambao wameomba msaada katika kubadili kutoka kwa gesi asilia hadi aina ya vikuni vinavyoweza kuwaka, vilivyotengenezwa kwa vipande vidogo vidogo vya mbao zilizobanwa.  Seminari  ayari inazalisha  zana hizo, shukrani kwa msaada unaotolewa na Chombo hiki cha Msaada (ACS) utaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kupasha joto seminari hiyo. Akiwageukia wafadhili wa ACN, Askofu Honcharuk alihitimisha kusema kwamba: “Tunapitia kipindi kigumu sana nchini Ukraine. Tena, tunashukuru sana kwa msaada wenu. Pia tunashukuru kwa maombi na usaidizi tuliopokea kutoka kwa watu wengi wakati wa vita.”

ACS kutoa msaada nchini Ukraine
03 December 2022, 11:34