Tovuti mpya ya Uisg,katika huduma ya utunzaji wa watoto maskini
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Mpango kikatoliki wa Kimataifa la Kulinda Watoto(CCCI) unaohamasishwa na Umoja wa Kimatifa wa Mama Wakuu wa Mashirika{UISG} umezindua tovuti yake, ambayo inaonesha dhamira ya kina ya watawa wa Kikatoliki duniani kote ili kuleta mapinduzi katika mfumo wa ulinzi wa mtoto. Dhamira hii inajikita katika lengo kuu la Kiinjili la kuwatunza wale ambao ni wadhaifu zaidi, pamoja na mafundisho jamii katoliki yanayojikita zaidi katika kuthamanisha hadhi na utu wa mtu. Tovuti hiyo inatokana kwa dhati na utafiti za hivi karibuni katika nyanja ya sayansi jamii na inaambatana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto, zinazotambua haki ya kila mtoto kukua katika mazingira ya familia yenye kukaribisha.
Inahitajika ufahamu ulio wazi wa ulinzi wa watoto
Na Sr. Nadia Coppa, rais wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya kitawa [UISG] akitoa neno lake kuhusu Mpango huo mpya wa uzinduzi wa Tovuti kama chombo cha kimataifa katika masuala ya Ulinzi wa Watoto, alisema kwamba pamoja na shukrani kubwa, kwa niaba ya Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa anapongeza zaidi kwa mpango huo zaidi, unaohamasishwa na Kanisa Katoliki la Ulinzi wa Watoto, ili kuongeza ufahamu na kuweka wazi juu ya ukweli wa ulinzi wa mtoto. Amesisitiza hayo kutokana na kwamba suala hilo ni kama mzizi unaojikita katika sharti la kiinjili la kutunza walio wadhaifu zaidi, na vile vile katika mafundisho jamii ya Kanisa Kikatoliki ambayo yanazingatia hasa utu wa mtu.
Huduma ya Kimataifa katoliki kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto
Kwa kuzinduliwa nchini Uganda, Kenya na Zambia, Huduma Kikatoliki ya Ulinzi wa Watoto iliundwa rasmi mnamo mwaka 2020, chini ya usimamizi wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika[Uisg]. Dhamira yake ni kutoa msaada kwa harakati ya watawa wa Kikatoliki, ambao wanalenga kupunguza hitaji la kuwaweka watoto katika taasisi, na ili kuzuia kuvunjika kwa familia na kutoa suluhisho mbadala unayowezekana na kuwawezesha watoto kukua katika mazingira ya kifamilia yenye upendo. Hivi sasa,kwa maana hiyo huduma ya[Catholic Care for Children International] inafanya kazi ndani ya zaidi ya maeneo 200 na programu mbalimbali, ikijumuisha kupitia washirika wake, nchini Uganda, Kenya na Zambia, na inatazamia kupanua huduma yake katika nchi nyingine pia.
Kufanya mapinduzi katika mfumo wa ulinzi wa mtoto
Katika muktadha huo Sr, Niluka Perera, mratibu wa Uisg wa CCCI, amefafanua kwamba tovuti mpya ni suluhisho ambalo linawawezesha kuthibitisha hitaji kubwa la kuleta mapinduzi katika mfumo wa ulinzi wa watoto na kushiriki mikakati hiyo ya kuona mbali ambayo taasisi za kitawa zinafanya kwa ajili yao. Mamia elfu ya watoto duniani kote wanaishi katika taasisi kama vile vituo vya watoto yatima, lakini si kwa sababu hao hawana makazi. Hii ni kutokana na kwamba karibu asilimia 80% ya watoto, kiukweli, wana mzazi mmoja au jamaa wa karibu, lakini hawana rasilimali muhimu za kuwasaidia. Kwa maana hiyo Sista Perera alibainisha kwa maoni yake kwamba hakuna mtoto kiukweli anayepaswa kuishi katika taasisi kwa sababu familia ni maskini au imezidiwa na ugumu wa kupata huduma msingi wa afya, hifadhi ya jamii au elimu kwa mtoto wao.
Familia moja kwa kila mtoto
Umoja wa Watawa Kimataifa UISG, kwamaana hiyo, imejitolea kubadilisha hali kama hiyo kwa kuweza kutumia tovuti mpya ili kusaidia watawa na taasisi za kitawa mahali popote pale kushiriki kwa urahisi rasilimali na kila mmoja wao, na umma na mashirika mbali mbali yenye mapenzi mema yanayohusika katika harakati hizi kwa ujumla kuleta mabadiliko kwa watoto hao. Tovuti itaakisi juhudi zinazofanywa na watawa duniani kote, ikionesha kile kinachohitajika ili kutambua maono ya familia kwa kila mtoto. Zaidi ya hayo, alihitimisha Sr. Coppa, kuwa tovuti hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa kuhusu ukuaji wao Kama Umoja na kuwawezesha kujifahamisha kwa wengi uzoefu, mbinu na rasilimali zinazo hamasisha wazo hilo jipya la siku zijazo na vivyo hivyo, kuweza kuleta mabadiliko ya kijamii.
Tovuti kwa lugha mbali mbali
Uzinduzi wa tovuti ya Mpango kikatoliki wa Kimataifa la Kulinda Watoto {CCCI} unaashiria awamu ya kwanza ya kazi ambapo toleo la Tovuti itakuwa kwa lugha ya Kiingereza. Awamu nyingine itakayofuata italeta pamoja maendeleo ya toleo la tovuti kwa lugha ya Kihispania, Kiitaliano na Kifaransa; kwa kuongeza, Tovuti hiyo yenye washirika wa CCCI inaweza kuunganishwa na kila mmoja, kushirikiana na kushirikisha rasilimali za ziada. Zaidi CCCI ina chaneli zake za Facebook, Twitter, na YouTube.