ITALIA:harakati za Caritas Italia kusaidia watu waliokumbwa na maparomoko,kisiwa cha Ischia
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Caritas Italia inaendelea kufuatilia kwa umakini hali halisi ya Casamicciola, katika kisiwa cha Isichia nchini Italia kilicho kumbwa na maparomoko mabaya ambayo yalisababisha vifo, majeruhi na mrundikano wa watu wengi kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni, mnamo Jumamosi tarehe 26 Novemba 2022, Rais na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI), Kardinali Matteo Zuppi na Askofu Giuseppe Baturi, walimpigia simu Askofu Gennaro Pascarella kueleza masikitiko yake na mshikamano wa Baraza la maaskofu wa Italia kwa Jumuiya nzima iliyokumbwa na mkasa huo mbaya.
Kutokana na tukio hilo, Ijumaa tarehe 2 Desemba 2022, Mkurugenzi wa Caritas Italia, Padre Marco Pagniello, atakwenda katika kisiwa hicho ili kushuhudia na kuwa na ukaribu kwa watu huku kwa kufanya tathmini nzima na kanisa mahalia kuhusiana na uingiliaji kati wa kutoa msaada. Kwa kuungana kwa sala kwa ajili ya waathirika na kwa ajili ya familia zao, Caritas Italia inabaki na mawasiliano na kutuma uwakilishi wa kikanda na Caritas Jimbo ili kutathimini mahitaji ya lazima na ili waandae vema msaada huo. Hata hivyo kwa haraka mara baada ya tukio hilo kutokea walianza mapema kutoa msaada wa hali na mali hasa kiadili na kisaikolojia kwa familia zilizorundikana kwa namna ya pekee watoto na wadhaifu.
Wakati wakisubiri utekelezaji wa mpango wa Ulinzi wa Raia, ambacho kimefanya kazi usiku na mchana kutafuta ambao bado wamepotea, kituo cha Yohane Paul II ambacho kwa sasa ndicho kituo cha kwanza cha marejeo ya kupokea watu waliohamishwa na kuelekezwa kwenye hoteli ambazo zimetoa nafasi, ambapo baadhi yao majiko hayafanyi kazi, kwa muda Caritas pia inaendelea kutoa chakula kwa watu hao, ameeleza Mkurugenzi wa Caritas Italia.
"Dharura hii mpya inaathiri eneo na idadi ya watu ambayo, kama walivyo kuwa wameshutumu mwezi uliopita, kwa bahati mbaya bado inakabiliwa na ucheleweshaji wa ujenzi baada ya tetemeko la ardhi ambalo mnamo tarehe 21 Agosti 2017 lilisababisha vifo vya watu 2 na watu 42 kujeruhiwa, pamoja na watu 3,000 ambao baadhi yao bado leo hii wanaishi katika nyumba za muda", Padre Marco Pagniello amefafanua. Na zaidi aliongeza kusema kwamba hawawezi kuendelea kuzungumza kuhusu kinga na matibabu tu wakati kuna dharura. Ni wakati wa uwajibikaji na ufahamu, kwani vitendo thabiti na vya mara kwa mara vya mafunzo, ulinzi na utunzaji wa eneo vinaweza kuzuia au kwa hali yoyote kupunguza hatari kwa watu walio hatarini zaidi.