Tafuta

Maaskofu nchini Ghana wamehitisha mkutano wao mkuu kwa wito kwa serikali ya kujikita kutatua matatizo ya wananchi wao ambao wamekasirika na kukata tamaa. Maaskofu nchini Ghana wamehitisha mkutano wao mkuu kwa wito kwa serikali ya kujikita kutatua matatizo ya wananchi wao ambao wamekasirika na kukata tamaa. 

Ghana-Watu nchini Ghana wamekasirika na kukata tamaa kutokana na ufisadi

Mwisho wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Ghana wameandika ujumbe wao wakielezea hali halisi ngumu ya kijamii na matatizo yao.Kwa mujibu wa Maaskofu wamebainisha kuwa hasira na kufadhaika inachochewa na ufisadi wa viongozi wa umma.Wanatoa wito hasa kuhusu suala hili linaliionekana kutoleta matokeo chanya.Ufisadi ni katika kila nyanja ya maisha nchini Ghana.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ufisadi, mzozo wa kiuchumi, majanga ya mazingira yanayohusishwa na shughuli haramu za uchimbaji madini na hatari zinazoweza kutokea za upanuzi wa shughuli za wanajihadi kutoka nchi jirani yamekuwa matatizo yanayoikabili Ghana yaliyosisitizwa na Maaskofu wa nchi hiyo katika taarifa yao iliyochapishwa mwishoni mwa Mkutano wao wa Baraza Kuu uliofanyika huko Donkokrom. Nchini Ghana, inayofikiriwa kuwa miongoni mwa nchi zilizo imara zaidi katika Afrika Magharibi, kwa mujibu wa Maaskofu wamebainisha kwamba,  kwa sasa inakumbwa na gharama kubwa ya maisha, kupanda kwa mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira kwa vijana, rushwa, ongezeko la uhalifu, uchimbaji haramu wa madini (galamsey), taasisi za serikali dhaifu na zisizo na ufanisi, miradi ya serikali iliyoachwa na kutokamilika, utamaduni wa kutoadhibiwa, usafirishaji haramu wa binadamu na utekaji nyara. Kwa sababu ya matatizo makubwa ya kiuchumi, Watu wa Ghana wanazidi kukasirika, kukatishwa tamaa na kwa maana hiyo Maaskofu wa nchi hiyo wanaoomba hatua za haraka zifanyike ili kuzima hasira na kufadhaika kwa idadi ya watu.

Zirejeshwe fedha zilizoibiwa na wafisadi

Hata hivyo kwa mujibu wa Maaskofu nchini Ghana wamebainisha kwamba hasira na kufadhaika pia kunachochewa na ufisadi wa viongozi wa umma. Kutona na hilo wanatoa wito wao hasa kuhusu suala hili linaloonekana kutoleta matokeo chanya. Wamesisitiza kwamba ufisadi katika kila nyanja ya maisha  nchini  Ghana si kwamba inaonekana tu, bali  pia imeenea sana, kwa njia hiyo  wanaoomba juhudi kubwa zaidi kuwabaini wafisadi na kurejesha fedha zilizoibiwa. Kuhusu suala la  galamsey hivi karibuni limeshutumiwa na madhehebu mbalimbali ya Kikristo. Katika ujumbe wao, Maaskofu wamesisitiza kuwalenga wale wanaofadhili shughuli za uchimbaji haramu wa madini kwamba wanaviomba vyombo vyenye uwezo vinavyohusika na ulinzi na uhifadhi wa maliasili zao kuwafungulia mashitaka wafadhili wa shughuli zinazosababisha uharibifu mkubwa kwa nchi kama vile uchimbaji haramu wa madini hayo ya Galamsey.

Mzozo uliosahuliwa katika eneo la Mashariki ya Juu mpakani na Burkina Faso

Hatimaye, Maaskofu nchini Gahana katika hati yao mara baada ya Mkutano wao Mkuu  wamekumbuka mzozo uliosahaulika katika eneo la Mashariki ya Juu, kwenye mpaka na nchi ya Burkina Faso kwamba  inaonekana migogoro hiyo  na ukosefu wa usalama huko Bawku  na unatoweka polepole kutoka katika rada ya serikali. Jiji limekuwa kivuli cha ubinafsi wake wa zamani kwani sekta za elimu, afya na kijamii zimeathiriwa vibaya na kuhama kwa walimu, wauguzi na wafanyabiashara kutoka eneo hilo. Katika Mkoa huo kwenye  sehemu ya kaskazini-mashariki mwa Ghana, kwenye mpaka na Togo upande wa mashariki na Burkina Faso upande wa kaskazini, wakazi wa Mamprusi na Kusasi wamekuwa wakikabiliana kwa miaka mingi kuhusu masuala ya umiliki wa ardhi. Kwa maana hiyo wamebainisha kwamba ni lazima kuzingatia kwa umakini hali ngumu ya wakaazi waliosalia katika jiji hilo, kwa kuhakikisha kuwa suluhisho la kudumu linapatikana kwa mzozo huo ili kuzuia Bawku na mazingira yake kuwa chachu ya vikundi vya kigaidi vinavyofanya kazi katika nchi jirani, wamehimisha maaskofu hao.

Maaskofu nchini Ghana wakemea ufisadi wa kukithiri

 

18 November 2022, 10:43