Congo DRC-Maaskofu wameitisha maandamano ya amani Desemba 4
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati dunia ikiendelea kutazam vita vya Ukraine, lakini bado kuna vita vingine vingi duniani vilizyosahulika vinavyozidi kuwatesa wasio na ulinzi na kujitetea. Ni katika muktadha wa Congo ambako watu wamechoshwa na makundi ya msituni yanaoendelea kutaabisha watu na mauaji. Jumla ya watu 2,639 wamevuka Mto Kongo kuanzia mwisho wa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa Septemba mwaka huu kukimbilia katika kitongoji kidogo cha Ngabe, katikati-mashariki mwa Jamhuri ya Congo. Caritas Congo inasema kinachotia wasiwasi ni hali duni ya usafi ambapo wakimbizi wanalazimika kuishi, huku kukiwa na hatari ya kuenea kwa magonjwa ya mlipuko, na uhaba wa chakula, unaochochewa na kupanda kwa bei ya vyakula kutoka mji mkuu, Brazzaville. Na haiwezekania kuondoa hata wimbi la wakimbizi wanaotoka DRC mahali ambapo hali inabaki kuwa tete sana.
Takriban watu 20 waliuawa hivi karibuni katika shambulizi katika kijiji cha Boku, eneo la Kwamouth, jimbo la Mai-Ndombe. Mapigano kati ya Teke na Yaka, ambayo yalizuka mwezi mwezi Juni, yalisababisha vifo vya takriban watu 180 kwa mujibu wa mamlaka ya Kinshasa na kuwalazimu makumi kadhaa ya maelfu ya watu kukimbilia maeneo mengine nchini DRC au karibu na Kongo Brazzaville (Jamhuri ya Kongo). Mapigano ambayo yalianza Mai-Ndombe mnamo Juni kisha kuenea hadi mkoa jirani wa Kwilu, ambapo shambulio katika kijiji cha Misia mnamo tarehe 2 Novemba 2022 lilisababisha vifo vya watu 16, kulingana na mamlaka ya mkoa.
Baraza la Maaskofu wa Kitaifa wa Kongo (CENCO) DRC limehitisha maandamano ya amani Dominika tarehe 4 Desemba 2022 ili kuomba usalama wa DRC. Maaskofu wamasema kwamba, Hali ni mbaya. Nchi yetu iko hatarini! Tusiibebe Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kutoka kaskazini hadi kusini, mashariki hadi magharibi, na vile vile huko ughaibuni, sote tusimame kulinda uadilifu wa eneo la nchi yetu. Kwa ajili hiyo, tunawaalika Wakristo na watu wenye mapenzi mema kufunga, kusali, kufanya ishara za mshikamano na waliohamishwa. Ni mwaliko uliotolewa na kuchapishwa mwishoni mwa Mkutano maalum wa Mjadala uliofanyika Kinshasa, kuanzia tarehe 7 hadi 9 Novemba 2022. Maaskofu hao wakielezea zaidi mashariki mwa nchi, ambako vikundi mbalimbali vya wapiganaji wa msituni vinavamia, watu na maeneo na hivyo wanakumbusha kuwa hali ya usalama inatia wasiwasi ambayo inaendelea katika maeneo ya Kwamouth (Maï-Ndombe) na Bagata (Kwilu).