Bukoba,Tanzania:waseminari 87 wamepokea vazi la uklero
Na Patrick Tibanga; - Radio Mbiu, Bukoba Tanzania.
Vazi liitwalo talar ni vazi la kikanisa kwa makasisi kwa baadhi ya madhehebu ya Kikristo. Neno talar linatokana na neno la Kilatino talus, au kisigino. Kwa sababu kiukweli ni kwamba neno hilo au kasoki, linatokana na vazi la makuhani wa Kiyahudi ambalo lilifika hadi kisigino. Vazi hilo basi likawa mfano kwa makasisi wa kikristo kuanzia karne ya IV au V (BK). Katika Kanisa Katoliki kasoki limekuwa vazi la kawaida la kikanisa linalovaliwa wakati wa shughuli za kidini, ambapo wakati mwingine hufunikwa na mavazi matakatifu wakati wa maadhimisho ya misa. Lakini pia hata kuvaliwa katika kazi za nje za kidini kama vazi la makasisi au wale ambao wako kwenye mchakato wa kuelekea ukuhani na watawa wa mashirika mbali mbali. Kulinganana hali ambayo huvaliwa, vifaa vingine vinaweza kuongezwa ili kukamilisha mavazi hayo kulingana muktadha wa tukio mfano (mavazi ya piano, au mavazi ya kwaya).
Kasoki au kanzu si lazima daima kuunganishwa na Sashi ambayo huvaliwa kiunoni, yenye rangi sambamba na cheo cha mtu mhusika. Kwa upande wa Maaskofu, makadinali na Papa basi huweka juu yake kiitwacho pilgrim, yaani mhujaji sawa na mozzetta yaani (kifuniko kama kofia ambacho ufungwa kwenye kifua kwa kifungo: na zaidi utakuta Papa anayo nyeupe na makardinali - nyekundu), ya maaskofu (violet) na baadhi ya vyeo fulani vya kikanisa, ambayo vinajulikana kwa kuwa ni wazi mbele, badala ya kufungwa na vifungo). Kasoki au kanzu nyeusi au nyeupe mara nyingi kwenye utume huvaliwa ulimwenguni na watu wengine wa kawaida, katika kutekeleza majukumu maalum ya huduma altareni, kama vile waseminari, wasomaji wa neno la Mungu na wahudumu wa altareni kwa ujumla.
Katika muktadha wa ufafanuzi mfupi, basi Jumamosi tarehe 26 Novemba 2022 katika Kikanisa cha Seminari Kuu ya Ntungamo ya Mtakatifu Antoni wa Padua, Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Almachius Rweyongeza wa Jimbo Katoliki la Kanyanga, Tanzania aliadhimisha misa Takatifu, katika fursa ya kubariki makanzu na sashi, kwa ajili ya waseminari 87 wa mwaka wa kwanza wa Falsafa. Wakati wa mahubiri yake, Askofu alisema kwamba vazi la Uklero ni ishara ya cheo cha mtumishi wa Mungu anayetumwa katika altare ya Bwana, hivyo msemimari anatakiwa kuitunza na kuifikisha safi katika uzima wa milele. Vazi wanalovaa watawa na Wakleri, lina maana yake kubwa ikiwa ni katika kulitumia katika maisha yote na kwamba nguo nyeupe ni ishara ya kuwa kiumbe kipya cha kumvaa Kristo, kwa njia hiyo vazi la Uklero ni vazi rasmi ambalo anayelivaa anatakiwa kufanya utume wake bila kutazama nyuma wala kando na kumtumikia Mungu katika wito alioufuata.
Askofu Rweyongeza aidha alisema kuwa kujifunga sashi na kuvaa kanzu la Uklero kuelekea upadre ni wito usio na malipo yoyote na kuwapa onyo kwa wazo lolote ambalo wanaweza kuunda vichwani mwao akitoa mifano kadhaa, hivyo kama waseminari wanatakiwa kujituma na kulitumikia Kanisa kwa upendo bila kutazama kandoni wala nyuma na aliwasihi mafrateli hao wasipenda hutafutaji wa kupata fedha za haraka kwani hicho ndicho chanzo cha maovu yote. Zaidi ya hayo unaweza kusikiliza sehemu ya mahubiri yake.
Yafuatayo ni sehemu ya mahubiri ya askofu Almachisu Rweyongeza kwa kufafanua maana ya Kanzu la Uklero: