Tafuta

Wamisionari wanakwenda kila eneo Wamisionari wanakwenda kila eneo 

Siku ya Kimisionari duniani 2022:kuzuia wahamiaji ni kuzuia ndugu katika imani!

Katika kuelekea siku ya Kimisionari duniani Dominika tarehe 23 Oktoba,Rais wa Mfuko wa Baraza la Maaskofu wa Italia katika kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi amethibitisha:kuzuia wahamiaji ina maana ya kuzuia kaka na dada katika imani.Katika ujumbe wa Papa wa Siku hii anafafanu zaidi juu ya kwamba ni mashuhuda wa imani katika nchi wanazokaribishwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Kimisionari duniani, itakayofanyika Dominika tarehe 23 Oktoba 2022, kwa kuadhimishwa na maparokia yote duniani, Askofu Mkuu Gian Carlo Perego, wa Jimbo Kuu katoliki la Ferrara Italia na Rais wa Mfuko wa Wahamiaji (Migrantes) wa Baraza la Maaskofu Italia amethibitisha kuwa: “Kuzuia kukaribisha wahamiaji maana yake ni kuzuia kaka na dada zetu hata katika imani”.  Hata hivyo katika ujumbe wa tukio la Siku hiyo kwa mwaka 2022, Askofu Mkuu Perego amesisitiza kwamba Baba Mtakatifu Francisko alielezea kwa dhati juu ya nafasi ya wahamiaji kwa namna ya pekee  kwamba  wakimbizi ni kama mashuhuda wa imani na umuhimu wa kukaribishwa kwa nchi  wanapofikia.

SIKU YA KIMISIONARI MWAKA 2022 NI DOMINIKA 23 OKTOBA
SIKU YA KIMISIONARI MWAKA 2022 NI DOMINIKA 23 OKTOBA

Katika maelezo ya kifungu hicho  kwa sababu ya mateso ya kidini, na hali za vita, vurugu, alisema wakristo wengi wanalazimika kukimbia katika ardhi zao kuelekea nchi nyingine. Kwa maana hiyo kuna furaha kubwa ya kaka na dada hao ambao hawajifungii katika mateso, bali wanashuhudia Kristo na upendo wa Mungu kwa Nchi ambazo zinawakarimu. Kwa ufafanuzi alisema katika hilo alikuwa anashauri Mtakatifu Paulo VI kwa kuwafikiria  uwajibikaji ambao unasubiri wahamiaji katika Nchi ambazo zinawapokea (Evangelii nuntiandi, 21). Kiukweli, kwa kufanya uzoefu kama uwepo wa waamini wa mataifa mengi yanatajirisha sura za parokia na kuzifanya kuwa za ulimwengu na zaidi kuwa katoliki. Matokeo yake, utunzaji wa kichungaji wa wahamiaji ni shughuli za kimisionari ambazo hazitakiwi kudharauliwa na ambazo zinaweza kusaidia hata waamini mahalia wanapofikia kugundua furaha ya imani ya kikristo  waliyoipokea.

SIKU YA KIMISIONARI MWAKA 2022 NI DOMINIKA 23 OKTOBA
SIKU YA KIMISIONARI MWAKA 2022 NI DOMINIKA 23 OKTOBA

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Perego amesema hata nchini Italia, wahamiaji wanatoka karibu  nchi 190 na wakimbizi kutoka karibu nchi 60. Kupitia  historia zao  maisha yao ambayo yanazungumza, na kwa kutumia tena maneno ya Baba Mtakatifu, alisema, wanatambuliwa hata shida na mateso kwa ajili ya imani yao zaidi ya vita, mabadiliko ya tabianchi, na umaskini. Kwa maana hiyo wahamiaji na wakimbizi ni sura na historia za matumaini ambazo zinamwilisha hata maisha ya kikristo ya jumuiya zao, ambapo karibu ni wakatoliki wahamiaji 900.000 nchini Italia, kwa kuongezea idadi ya Wakristo mwaka huu na ambao kiukweli wanasaidia kugunda furaha ya imani na kutoa msukumo na mwamko wa kutembea pamoja.

Siku ya Kimisionari duniani 23 Oktoba
21 October 2022, 14:01