Nigeria:Utekaji nyara kwa padre mwingine nchini Nigeria
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Aliyekuwa Paroko wa Mtakatifu Yosefu, Abata Nsugbe, Padre Joseph Igweagu, alitekwa nyara wakati alikuwa anarudi nyumbani kwake, baada ya kuadhimisha misa ya mazishi huko Umunnachi, Serikali ya Anambra, siku ya Jumatano tarehe 12 Oktoba 2022. Ni taarifa zilizotolewa na Jimbo Kuu katoliki la Onitsha tarehe 16 Oktoba 2022 kwa mujibu wa Shirika la habari za Kimisionari Fides zilizowafikia.
Kufuatia na tukio hilo, waamini wote wanaombwa kusali ili Padre huyo aweze kuachiliwa huru bila shurutisho lolote, na Jimbo kuu linafanya kila liwezalo ili aweze kuachiwa huru. Wakati wanaendelea kusali kwa ajili ya uongofu wa watekaji nyara, vile vile wametoa ombi kubwa kwa Mama Maria anayefungua mafundo yote ili kwa maombezi yake mama Padre aweze kuachilia haraka. Ndiyo ujumbe ulivyoelezwa na Shirika la habari za kimisionari Fides.
Serikali ya Anambra inapatikana Kusini Mashariki mwa Nigeria na ni moja ya maeneo yaliyokumbwa na matukio kama hayo ya utekaji nyara kwa lengo la kulipa fidia na wahalifu ambao wamekuwa adui wakubwa katika maeneo ya Nigeria.