Ikiwa milioni moja ya watoto wanaosali Rozari,ulimwengu unaweza kubadilika!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Shirika la Kipapa la Mfuko wa Kanisa Hitaji (ACS) linatoa mwaliko kwa mara nyingine tena kwa parokia, shule za awali, za msingi, sekondari na familia ili kushiriki katika mpango wa Kampeni ya kila mwaka uitwao: “Milioni moja ya watoto wanasali Rosari”, itakayofanyika mnamo tarehe 18 Oktoba ijayo. Dhumuni ya kampeni ya sala ni kuzidi kuomba kwa ajili ya amani na umoja kwa ulimwengu wote, kuwatia moyo watoto na vijana ili kuwa na imani kwa Mungu wakati wa shida, kwa mujibu wa Rais wa Kimataifa wa Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji (ACS), Kardinali Mauro Piacenza.
Katika Bango la Kampeni ya mwaka huu, inawakilisha mikono miwili iliyofunguliwa na kukumbatia ulimwengu na kuwasaidiwa na watoto pamoja wa kila bara la ulimwengu. Mikono hiyo inaamanisha Baba Muumba ambaye aliumba ulimwengu kwa upendo na ambaye anatamani kuwaokoa watu wote na kuwapeleka kwake wakiwa salama na waliokombolewa. Kwa kutazama hali halisi inayozungukia ulimwengu kama vile vita, ubaya, mateso, magonjwa na hovu ambazo zinatetemesha ulimwengu wetu, watu wanaweza kujiuliza: “Je Mungu kweli ni mdhibiti? Kwa mujibu wa Kardinali Piacenza anauliza katika uwakilishi wa mpango huo, lakini pia na kujiibu kwamba ndiyo anafanya hivyo lakini tunapaswa hata sisi kuonesha mikono yetu na kumkumbatia Yeye.
“Mungu alitukaribua sisi sote kwa njia ya Maria. Kwa maana hiyo tumuombe ikiwa tutasali Rosari kwa imani, pamoja kwa Mama Mtakatifu wa Mungu atatufikisha wote kama familia kubwa katika mikono yake ya upendo kwa Baba wa Mbinguni”. Kwa kuhangaishwa na hali ya vita, vurugu na umaskini mkubwa unaoendelea kuzikumba nchi kama vile Ukraine, Nigeria, Myanmar, Pakistan, au maeneo kama Mashariki ya Kati na Sahel barani Afrika, Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji (AC) unapenda kuyakabidhi maeneo hayo yote ambayo watu hawa hawana mahali na wanaweza kuishi kwa amani katika mikono yenye nguvu na upendo ya Baba wa Mungu, kwa maombezi ya Mama wa Mungu. Mfuko wa kipapa unaamini kuwa ushiriki wa nchi kadhaa katika kampeni zilizopita umekuwa mzuri sana. Tayari mnamo 2020, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu alikuwa amehimiza kujiunga na mpango huo.
“Baadhi ya hisia chanya ambazo tumekuwa nazo zimetoka katika maeneo ambayo amani inahitajika zaidi. Inatia moyo sana kujua kwamba kuna watoto nchini Iraq, Siria, Belarus au Myanmar wanaosali pamoja na wale wanaokusanyika huko Fatima, Ureno, Canada au Marekani. Inatufanya tuwe na matumaini kwamba upendo unaotokana na imani unaweza kushinda vurugu”, alisema, Padre Martin M. Barta, Msimamizi wa Kikanisa wa Kimataifa wa Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji (ACS).
Ukurasa wa wavuti wa Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji ACS unatoa nyenzo za bure kwa wale wanaosali katika parokia, shule, vikundi vya watoto na familia. Kifurushi cha habari kisicholipishwa kina maagizo ya jinsi ya kusali Rozari, tafakari fupi za watoto kuhusu Mafumbo ya Rozari na nyenzo nyinginezo, zote zinapatikana mtandaoni, pamoja na picha za kupaka rangi, kwa watoto katika lugha 26 tofauti. Kwa nyenzo katika Kiitaliano inawezekana kutembelea tovuti:https://acs-italia.org/rosariobambini,wakati kwa lugha nyingine tovuti ni: https://acninternational.org/millionchildrenpraying/material/.
Ikumbukwe chimbuko la mpango wa “Watoto Milioni Moja kusali Rozari” ulianza mnamo mwaka wa 2005, wakati kikundi cha watoto kilionekana wakisali Rozari kwenye kaburi katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas, na baadhi ya watu wazima walioshuhudia tukio hilo walikumbuka maneno ya Mtakatifu Pio wa Pietrelcina kwamba “Watoto milioni moja watakaposali Rozari, ulimwengu utabadilika”. Tangu wakati huo, kampeni imeenea kwa kasi na imekuwa jambo la ulimwengu wote.