Kard.Montenegro,Rais wa Caritas Italia:Umaskini hausubiri mikono iliyoonyoshwa!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Kila ifikapo tarehe 16 Oktoba ya kila mwaka uhadhimishwa Siku ya Umaskini Duniani, iliyotangazwa miaka 25 iliyopita na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na azimio 47/196 la 22 Desemba 1992. Mwaka huu pia ni kumbukumbu ya miaka 30 ya wito wa tarehe 17 Oktoba 1987 wa Padre Joseph Wresinski, mwanzilishi wa Harakati ya Atd-Fourth World, yaani ‘Htd Ulimwengu wa Nne’, Wakati watu laki moja walipoitikia kwa kukusanyika katika ukumbi wa Uhuru na haki za binadamu wa Trocadero jijini Paris nchini Ufaransa ili kuwaheshimu waathirika wa njaa, vurugu na ujinga na kutangaza kukataa kwao taabu.
Baada ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa FAO, katika fursa ya Siku ya Chakula Duniani, aliouelekeza kwa Bwana Qu Dongyu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) la vyakula na Kilimo, alisema kuwa haiwezekani kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu ikiwa hufanyi kazi na kutembea pamoja; ni lazima kutazama wengine kama kaka na dada zetu, ambamo mateso na mahitaji yanatugusa wote. Kwqa maana hiyo katika mahojiano na Gazeti la Baraza la Maaskofu Italia la Avvenire, Kardinali Francesco Montenegro, Rais wa Caritas Italiana, amekumbuka jinsi gani “umaskini hausubiri, mikono iliyonyooshwani mikono inayoparamia. Kwao huwezi kusema: siku moja itakuwa zamu yako pia. Ni muhimu kuingilia kati mara moja. Lazima tuwajibu maskini wote Tunahitaji ujasiri, hakuna wakati tena.”
Kwa upande wa Kardinali na rais wa Caritas amebainisha kwamba kiwa ni sehemu tu ya wale wanaohitaji wanaweza kupokea faida, ni wazi kwamba sisi sote tutahitaji kufungua mioyo yetu zaidi kidogo. Akitazama ujumbe wa Papa, Kardinali amesema kwamba Papa Francisko anatuambia kwamba ni lazima tutende kwa upendo na kwa upendo. Upendo ni kujibu mahitaji ya mwingine. Narudia kusema: sio sadaka, ni kutafuta haki. Na Papa Mstaafu Benedikto XVI pia alisisitiza umuhimu wa upendo katika kujenga uchumi wa haki zaidi. Upendo hutusukuma kujiangalia zaidi ya sisi wenyewe na hutualika kuwa na ujasiri katika kufanya chaguzi tofauti.
Wiki ijayo, kuanzia Alhamisi ijayo Caritas Italia itachapisha mtandaoni Ripoti yake yakila mwaka kuhusu Sera za Umaskini nchini Italia, na kisha katika mwezi Novemba, 17 ijayo itawasilisha Ripoti yake ya Umaskini ya 2017, tangu kuanzishwa kwa Siku ya Kwanza ya Maskini Duniani kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko mwishoni mwa Jubilei ya Huruma 2016, ambayo iliweza kuona na kuonja ladha ya huruma na upendo wa Mwenyezi Mungu kwa wale wote ambao wanamkibilia kwa imani.