Tafuta

Mgogoro wa kivita unaendelea kati ya Ukraine na Urussi Mgogoro wa kivita unaendelea kati ya Ukraine na Urussi 

Comece:Wito wa pamoja wa Maaskofu kutaka amani nchini Ukraine na Ulaya yote!

Katika tamko la Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu Barani Ulaya (COMECE) kwa ajili ya amani nchini Ukraine na Ulaya kwa ujumla wanamuomba Bwana “awaangazie wasimamao katika giza na uvuli wa mauti na kuziongoza hatua zao zote katika njia ya amani”.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu Barani Ulaya COMECE kwa pamoja tarehe 14 Oktoba  2022 walitoa wito  kwa ajili ya Amani nchini Ukraine na Ulaya yote ambao unaongozwa na kauli mbiu: “kuongoza  hatua zao juu ya njia ya amani” (Lk 1,79). Katika tamko lao, maaskofu wanabainisha kuwa wakati wameunganika pamoja katika mkutano wa majira ya vuli, wamehisi kuwa na huzuni wa kina kwa sababu ya mateso yasiyo elezeka ya kibindamu kwa kaka na dada zao wa Ukraine kutokana na kuvamiwa na kuuawa vibaya na mamlaka ya kisiasa ya Urussi. Maaskofu wanawakumbuka waathirika kwa sala na kuelezea ukaribu wao wa dhati kwa familia zao zote zinazopata mateso sasa.

Papa akiwa na wajumbe wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya
Papa akiwa na wajumbe wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya

Maaskofu aidha sawa na hilo wanahisi ukaribu na mamilioni ya wakimbizi hasa  wanawake na watoto ambao wamelazimika kuacha nyumba zao na kama ilivyo kwa wote ambao wanateseka huko Ukraine na katika nchi za karibu kwa sabababu ya uwenda wazimu wa vita hivyo. Maaskofu wa Shirikisho la Umoja wa Ulaya wanahisi kuwa na wasiwasi kuhusu matendo ambayo yanazidi kuwa tishio na hasara kubwa kutokana na matokeo mambaya kwa binadamu. Vita nchini Ukraine vinawatazama moja kwa moja wote hata kwa wazalendo wa Umoja wa nchi za Ulaya. Mawazo yao kwa maana hiyo yamewaendea wale wote walio katika matatizo kijamii na kiuchumi  ambayo yanazidi kuwa makubwa, kutokana na dharura ya nishati, kupanda kwa mfumko wa bei na kuongezeka kwa gharama ya maisha.

MKUTANO WA TUME YA SHIRIKISHO LA MABARAZA YA MAASKOFU ULAYA
MKUTANO WA TUME YA SHIRIKISHO LA MABARAZA YA MAASKOFU ULAYA

Mara nyingi ndani wakati wa mgogoro kama huu, maaskofu wamebainisha jinsi ambavyo  wanatambua  kwamba Muungano wa Ulaya ni ukweli wa thamani, kulingana na msukumo wake wa asili. Maaskofu  kwa maana hiyo wanashukuru juhudi zisizochoka za watunga sera wa Ulaya  katika kuonesha mshikamano na Ukraine na katika kupunguza matokeo ya vita kwa raia wa Ulaya na wanahimiza kwa dhati viongozi kudumisha umoja wao na azimio lao kwa mpango wa Ulaya. Kwa ushirikiano kamili na maombi mengi yaliyozinduliwa na Papa Francisko na Vatican kwa ujumla maaskofu nao wanatoa wito kwa waliohusika na uchokozi, ili kusimamisha uhasama mara moja, na kwa pande zote ili wafungue mfululizo mapendekezo ya amani ya haki, kwa nia ya suluhisho endelevu la mzozo katika heshima kamili kwa sheria ya kimataifa na uadilifu wa eneo la Ukraine na kwa maombezi ya Bikira Maria, Malkia wa Amani.

WITO WA SHIRIKISHO LA MABARAZA YA MAASKOFU ULAYA (COMECE)
22 October 2022, 13:25