CEI:Novemba 18 Siku ya Maombi kwa Waathirika wa nyanyaso:Ni uchungu na kufariji!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mfululizo wa mipango ya Makanisa mahalia nchini Italia, tarehe 18 Novemba 2022 itafanyika Siku II Kitaifa ya maombikwa ajili ya wahanga na walionusurika katika unyanyasaji, kwa ajili ya ulinzi wa watoto wadogo na watu wanaoishi katika mazingira magumu. Siku hiyo ilianzishwa na Baraza la Maaskofu wa Italia sambamba na Siku ya Ulaya ya Ulinzi wa Watoto dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia na Unyanyasaji wa kingono unahusisha jumuiya nzima ya Kikristo katika sala, ili kuomba msamaha kwa dhambi zilizofanywa na katika kukuza ufahamu wa suala la uchungu kweli.
Mungu aliyeumba ulimwengu anautunza
Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu Italia wanafafanua kwamba Mada inayoongoza Siku hii kwa mwaka 2022 imetolewa katika kifungu cha Zaburi “Bwana huwaponya waliopondeka moyo na kuwafunga jeraha zao” (Zab 147,3) na kwamba inaadhimisha Bwana ambaye aliumba ulimwengu na anautunza, akiiweka hai na, wakati huo huo, kamwe hawaacha watu wake katika machafuko ya maumivu, ambayo hukasirisha maisha ya kila siku na wakati mwingine huwafanya watu kupoteza maisha yao njiani na utambulisho. Picha ya kuponya majeraha ya moyo inaonesha uwezo wa Mungu wa kuwajua watu wake kwa kina; na kuna majeraha ambayo hayaonekani kwa nje, lakini yamekita ndani. Mungu anajua jinsi ya kufikia kina ya moyo ili kutuliza maumivu na kuanzisha uponyaji wa kina. Hii ndiyo faraja inayowangojea wale waliofungwa kwa Bwana: maumivu hayajatengwa, lakini hakuna maumivu ya uhakika. Na kwa hivyo sifa ambayo inaunda Zaburi inazaliwa kwamba Bwana hakuwaacha watu wake wakati wa mateso, wala hakuwangojea wapone wenyewe. Badala yake, alimfikia ili kumrudisha nyumbani, ili kumruhusu kurudi kuwa yeye mwenyewe: watu wa waliookoka. Baraza la maaskofu wamefafanua.
Faraja ni muhimu kwa Wakristo
Mada ya Siku ya Pili ya Kitaifa ya Maombi kwa Wahathirika na Wanusurika wa Unyanyasaji inatokana na tafakari hizi. Faraja, si tendo rasmi bali ni la lazima kwa jumuiya ya Kikristo, inakuwa ukaribu, usindikizaji, ulinzi, utunzaji, uzuiaji na malezi. Mtu hawezi kutazama mbali na majeraha yanayosababishwa na aina zote za unyanyasaji, wala hawezi kuwa na uponyaji bila kuchukua jukumu la maumivu ya wengine. Tukitumaini faraja ya Bwana katika kila maumivu, kila mmoja anaitwa kuunga mkono ufahamu huu mpya unaokomaa na kukua katika Makanisa yetu. Kwa maendelezo zaidi kuhusu siku hii inaweza kutazama kwenye Tovuti hii: https://tutelaminori.chiesacattolica.it/.