Tafuta

Siku kuu ya Kristo Mtakatifu  de La Grita nchini Venezuela Siku kuu ya Kristo Mtakatifu de La Grita nchini Venezuela 

Venezuela,katekista awe na moyo wa kisinodi kusikiliza,kuamua&kushirikisha

Kuanzia tarehe 18 hadi 25 ni Juma la Kitaifa la Katekesi ambalo limeandaliwa na Kitengo cha Katekesi cha Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Venezuela.Katika taarifa kuhusu tukio hilo wanabainisha kuwa kifungu cha Kibiblia ni kutoka Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi(2,2b)kisemacho:“Basi kamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, upendo mmoja na kuwa wamoja katika roho na hisia moja”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika muktadha wa maadhimisho ya Juma la Kitaifa la Katekesi, ambalo litaanza tarehe 18-25 Septemba 2022 nchini Venezuela, Kitengo cha Katekesi cha Baraza la Maaskofu wameandaa mwongozo wa mada: “Katekista na moyo wa kisinodi” ambayo watajikita nayo kwa Juma zima. Katika uwakilishi wamesisitiza kwamba moyo ni kitovu cha uhai wa kuwa binadamu na kama ilivyo kwa  Katekista, na  mwongozo umeandaliwa kwa sababu Juma liweze kuwa fursa kwa ajili ya kutafakari, kusali na kuadhimisha jinsi ya myo wa katekisita unavyotakiwa kuwa: moyo wa kisinodi ulio tayari kusikiliza, moyo wa kuzungumza, moyo wa kufanya mang’amuzi na moyo wa ushirikishwaji.

Kamilisheni furaha yangu na na nia mona na upendo mmoja

Wakinuu kifungu cha Kibiblia ni kutoka katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi (2,2b) kisemacho: “Basi kamilisheni furaha yangu kuwa na nia moja, upendo mmoja na kuwa wamoja katika roho na hisia moja” na kwamba,  Moyo ni nyumba ya moto wa Roho Mtakatifu ambao unatoa kila ubaridi wowote ule ili kutembea na mwingine na kuishi udugu. Kwa kutoka hapo ndipo kiini cha maisha ya Katekista kinaanza kutoka nje bila woga wa kutoa huruma; wa kusindikiza, wa kujikita katika michakato mzima kwa uvumilivu hata kwa kiasi gani cha hali ngumu ili kushuhuda, na anajua kupelekea matunda, na kusheherekea ufalme wa Mungu.

Moyo ukiugua na ubinafasi hawezi kuwa wa kisinodi

Kwa mujibu wa maelezo hayo wamebainisha kwamba Moyo unapokuwa umeugua na ubinafsi, ukatili, ugumu, roho ya kiulimwengu, vita kati yao, unaondoa uwezekano ambao katekesita angekuwa shuhuda, muwasilishaji, msindikizaji, wa kiroho na kisinodi. Ili kuweza kujikita na tafakari kwa kina na mada iliyochaguliwa kwa ajili ya Juma la Katekesi Kitaifa, wameweka hata zana ambazo kupitia shughuli ambayo inaweza kufanyika kupitia makundi ya makatekista na mwendelezo kwa ajili ya tafakari binafsi na kijumuiya.

Juma la Katekesi litafunguliwa kwa misa 18  na kufungwa kwa misa Septemba 25

Dominika tarehe 18 Septemba 2022, inatarajiwa kutolewa ujumbe kwa ajili ya makatekista kutoka Kitengo cha Katekesi cha Baraza la maaskofu nchini Venezuela, wakati siku ya kufungwa rasmi Dominika tarehe 25 Septemba itaaadhimiswa misa kwa ajili ya Siku ya Katekista na kuwatuma makatekista wamisionari.

Juma la Katekesi nchini Venezuela
13 September 2022, 15:11