Ulaya/Ccee:Septemba 14 katika sala ya kuabudu kwa ajili ya kuombea Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Upyaisho wa Roho Mtakatifu unapendekeza kusali kwa kauli mbiu inayowaongoza “Ukuta wa moto” kwa masaa 12 ambapo makundi ya waamini na katika majimbo mbali mbali ya Italia watakuwa na zamu za kusali mbele ya Ekaristi. Katika tukio lililoanzisha na Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu Barani Ulaya (CCEE) kama ilivyotangazwa na Rais wake, Askofu Mkuu Gintaras Grušas, wa Jimbo Kuu katoliki la Vilnius, kwamba katika Siku kuu ya Kutuka kwa Msalaba, iadhimishwe siku ya sala kwa ajili ya Amani nchini Ukraine. Kama mtindo wa pamoja wa kuweza kukutana katika anzisho hilo wamechagaua kuabudu ekaristi takatifu.
Wachungaji na waamini wawe mbele ya sakramenti takatifu 14 Septemba
Mabaraza yote ya maaskofu barani Ulaya yamendaa mwongozo wa kiliturujia na sala na tafakari. Kwa maana hiyo wanaalika wachungaji na waamini kujiweka mbele ya Sakramenti Takatifu ili kumwomba Mungu zawadi ya amani kwa kufanya uwe wao wito ambao Papa Francisko aliutoa mnamo Jumatano iliyopita wakati wa Katekesi yake, akiomba kila mmoja awe mjenzi wa amani na kusali ili ulimwengu uweze kuwa na mawazo na mipango ya maridhiano na mapatano.
Maaskofu Ulaya kuungana na sauti moja na Papa
Maaskofu wa Ulaya, mara kadhaa, wameungana moja kwa moja na sauti yao na ile ya Papa ya kutaka kusitisha silaha na kukomesha mara moja vita vya Ukraine na kufanya kazi kwa ajili ya amani. Na pia wametoa wito mwingi kwa viongozi wa mataifa na jumuiya ya kimataifa kufanya kila wawezalo kumaliza mzozo huo unaoangamiza maisha ya watu na kusababisha mateso mengi. Wakati wa Kwaresima mpango wa sala mbele ya Ekaristi, ulinzishwa kama ishara ya ukaribu wa Kanisa kwa wahanga wa UVIKO-19 na familia zao, mwaka huu ukawa fursa ya kuwaombea wahanga wa vita na kuomba amani katika nchi ya Ulaya Mashariki.
Ukuta wa Moto kwa masaa 12
Baraza la Maaskofu Wakatoliki wa Ukraine walitangaza mwaka 2022, kwa kile ambacho nchi yao inapitia, kuwa Mwaka wa Msalaba Mtakatifu utakaomalizika kwa Ibada takatifu na Njia ya Msalaba tarehe 14 Septemba 2022 katika Madhabahu ya Mateso ya Bwana, huko Sharhorod, hasa katika Siku ya Ulaya kwa ajili ya kuombea nchi ya Ukraine. Baraza la Maaskofu katoliki Italia kwa kukubali mwaliko wa CCEE, linapendekeza, mchana tarehe 14 Septemba wawe na wakati wa kuabudu Ekaristi. Harakati ya Upyaisho katika Roho Mtakatifu pia wataungana na mpango huo kauili mbiu ‘Ukuta wa Moto’, wa masaa 12 bila kukatiza waliota kama Kichaka Kinachochomwa ili Kuabudu Ekaristi kwa kuongozwa na uhuishaji na kwa nia za Papa Francisko na maaskofu wa Ulaya. Kila saa ya kuabudu itahusishwa na majimbo ya Kaskazini, Kati na Kusini mwa Italia.
Yesu alionekana dhaifu Msalabani lakini akawa na ushindi wa upendo
Bwana Salvatore Martinez, rais wa Harakati ya Upyaisho katika Roho Mtakatifu,(CHARIS) amehamasisha kwamba, sala mbele ya Msalaba, ambapo Yesu alionekana dhaifu na asiye na nguvu, inafundisha kwamba, ushindi wa upendo, amani na maelewano yanawezekana; kwa sababu kuomba kunaondoa silaha, kufariji, kuponya na kuokoa. Na kuhusu ushiriki wa Papa Francisko katika Kongamano la Viongozi wa Dini za Dunia na Dini za Jadi huko Kazakhstan, siku hiyo ambayo watu wanaomba amani nchini Ukraine, Bwana Martinez ana hakika kwamba atatoa fursa mpya chanya za kuheshimiana, ya kukua kati yao na urafiki wa watu.