Tafuta

2022.09.07 Sr. Maria De Coppi, Mkomboni aliuawa nchini Msumbiji  kati ya tarehe 6 na 7 Septemba 2022 2022.09.07 Sr. Maria De Coppi, Mkomboni aliuawa nchini Msumbiji kati ya tarehe 6 na 7 Septemba 2022 

Msumbiji:Sr Maria De Coppi shuhuda wa upendo kwa watu

Waasi walichoma nyuma ya kimisionari huko Chipene,mpakani mwa wilaya ya Cabo Delgado nchini Msumbiji.Mapadre wawili wa fidei donum na watawa wawili waliweza kukimbia,wakati Sr. Maria De Coppi hakuweza kujiokoa.Rais wa CEI alisema "tunalia kwa mara nyingine kwa dada ambaye kwa urahisi wake, shauku na ukimya alitoa maisha kwa ajili ya Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya Wakomboni huko Chipene nchini Msumbiji Kaskazini, ilishambuliwa katika usiku kati ya tarehe 6 na 7 Septemba 2022  na kikundi chenye silaha ambacho hakikutambuliwa. Sr  Maria De Coppi, mwenye umri wa miaka 84 asili ya Venezia Italia ambaye amekuwa nchini humo tangu 1963 ameuawa kwa mtutu wa bunduki, labda alipokuwa akitoka katika eneo la malazi ya kike ya Parokia. Waliookoka ni mapadre waili wa fidei donum wa Jimbo la Concordia-Pordenone. Hawa ni Padre  Loris Vignandel, 45 anni, asili ya Corva e na aliwahi kuwa Paroki wa  Chions (Pordenone) na Padre Lorenzo Barro, ambaye aliwahi kuwa gambera wa seminari ndogo ya Jimbo katika mji wa Destra Tagliamento, wote kutoka Italia. Wao waliweza kukimbia pamoja na watawa wengine wawili ambao baadaye walifikiwa na Askofu wa Nacala, Askofu Alberto Vera Arèjula.

Watu wengi wamekimbilia msituni

Kundi hilo lililojihami tayari lilikuwa limekaribia kituo hicho mapema kabisa, kwa siku nzima japokuwa lilikuwa halijavuka Mto Lurio, mpaka wa asili na jimbo la Cabo Delgado, eneo la ghasia zilizofanywa na makundi ya waasi kwa miezi kadhaa. Usiku, hata hivyo, uvamizi huo, pamoja na miundo mingi ya majengo ya kituo cha kimisionari kilichochomwa, ikiwa ni pamoja na kazi za parokia, mabweni na chumba cha kompyuta kilichozinduliwa hivi karibuni, huku vyumba walimokuwa walikimbilia mahali walipokuwa wamisionari ili kuepuka moto. Watu wote wanakimbia. Hali inasikitisha sana, watu wengi wanabaki kulala msituni". Yalikuwa  ni hayo baadhi ya maneno yaliyosikika katika ujumbe wa sauti, uliochapishwa kwenye tovuti ya watawa wamisionari wa Comboni uliotuma saa 2.17 mnamo usiku  tarehe 6 Septemba 2022 na Sr Maria De Coppi kwa mpwa wake Sr.  Gabriella Bottani.  “Bwana awalinde watu hawa”, alithibitisha Maria mwishoni mwa ujumbe wake.

Kituo cha kimisionari kimechomwa

Katika kuwasiliana kwa simu na mapadre, katika saa hizo za kutisha, kulikuwa na Alex Zappalà, Mkurugenzi wa kituo cha kimisionari huko Pordenone, ambapo manusura wawili wanatoka, ambaye alielezea  kwenye maikrofoni  za Vatican News kwa kile kilichotokea. Kutoka  kengele ya kwanza saa 3 usiku hadi kwa hofu ya Padre  Loris saa chache baadaye. “Tutaonana mbinguni,” alikuwa ameandika huku akisikiliza milio ya kwanza. Kisha saa 9 za asubuhi moto uliwaka katika kituo cha kimisionari, na makuhani wawili wakakimbilia katika vyumba viwili ambavyo vilivkuwa  havijaguswa na washambuliaji na moto. Kwa upande wa Katibu wa  Shirika la Kimisionari la Wakomboni Sr  Enza Carini, katika Ujumbe wake alisema, “Tusali kwa ajili ya dadfa yetu.Kwa uhakikaka ataombea watu wa Msumbisi na kwa ajili ya amani ya nchi hiyo aliyoipenda sana”

Kardinali Zuppi sadaka yake ipande mbegu ya matumaini

Salamu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Sr Maria zimeelezwa hata na Kardinali Matteo Zupi, Rais wa baraz ala Maaskofu nchini Italia (CEI) na askofu Mkuu wa Jimbi Katoliki la Bologna. Kwa mujibu wake alisema , “ Baada ya Sr Luisa Dell’Orto, wa Shirika la Dada wadodo wa Injili wa Charles de Foucauld, aliyefariki mnamo tarehe 25 Juni huko Haiti, , tunalia kwa mara nyingine tena kwa dada ambaye kwa urahisi wake, shauku yake na ukimya alitoa maisha kwa ajili ya upendo wa Injili”. Kwa maana hiyo Kardinalia amewaalikwa kusali kwa ajjili ya mtawa huyo ambaye kwa miaka sitini hivi alihudumia nchi ya Msumbiji na nchi kugeuka kama ya kwake, huku akiwa na matumaini kwamba sadaka ya  Sr. Maria iweze kuwa mbegu ya amani na mapatan katika nchi ambayo baada ya miaka ya msimamo, kwa upya iemkumbwa na janga la vurugu zitokananazo na makundi ya kiasi ambayo kwa baadhi ya miaka wamekuwa wakipanda hofu kubwa na vifo katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi. Kwa hiyo Kardinali  Zuppi alihimiza kila mtu awaombee wamisionari waliosalia katika nchi nyingi ili watoe ushuhuda wa upendo na matumaini na kuwa na mshikamano nao kwa sababu wanatembea na wote na kusaidia kufikia sehemu za mbali  ambapo wote wanaweza kujielewa kuwa wao akina nani na kuchagua jinsi ya kuwa wanafunzi wa Yesu.

Nchini Msumbiji Sr Maria alikuwa karibu na watu

Sr. Maria, Mkomboni, alizaliwa mwaka 1939, huko Santa Lucia di Piave katika Wilaya ya Treviso, Italia na baadaye kuhamia na familia yake hadi Ramera katika eneo la Veneto Italia. Mnamo mwaka 1963 alifika nchini Msumbiji kwa mara ya kwanza, nchi ikiwa bado chini ya ukoloni wa Ureno. Baada ya kuchukua uraia, Sr. Maria alikuwa sasa sehemu ya ardhi hiyo na watu hao mwenye huduma ya mara kwa mara iliyofanywa katika tume mbalimbali katika jimbo la Nampula. Kama ilivyoripotiwa na gazeti la kila wiki ‘veneto L'Azione.it’, ambalo lilimhoji nchini Italia mnamo 2021, miaka miwili iliyopita nchini Msumbiji alieleza jinsi ilikuwa ngumu sana kutokana na vita vya Kaskazini kwa rasilimali za dunia, basi pia kutokana na kupitia kwa  kimbunga na tena, kna wa ukame wa muda mrefu katika miaka iliyopita.Mtawa huyo alizungumzia umaskini uliokithiri na familia zilizokimbia. "Ninajaribu kukaa karibu na watu, zaidi ya yote kwa kusikiliza kile wanachoniambia. Licha ya umaskini wa mali, kuwasikiliza wengine bado ni zawadi kubwa, ni kutambua hadhi yao", alikuwa amesema. Masisita wenzake  Sr. Maria walisafiri kwenda  Chipene na kuchukua mwili wake ili kuuzika katika sehemu nyingine ya utume wao wa kimisionari.

Askofu Mkuu wa Nampula amesema ni janga baya sana 

 
Naye Askofu Mkuu Inacio Saure, wa Nampula, ambalo ni Jimbo kuu mahali ilipo nyumba ya kimisionari huko  Chipene, na Nacala, ikiwa ni mshirika alizungumza na Shirika la Habari za Kimisionari Fides. Na kuhusu utambulisho wa wale waliofanya shambulio hilo, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Suare alithibitisha kwamba "hatuna uhakika kama ni magaidi wa Kiislamu, hata kama kuna uwezekano mkubwa kwamba wao ndio walioshambulia kituo cha kimisionari”. Mwitikio wa watu hapa kama huko Capo Delgado, ni kukimbia tu. Hatujui ni watu wangapi wametafuta hifadhi msituni. Ni jambo la kutisha na bado ni vigumu kuhesabu."
Kifo cha Sr Maria Mkomboni nchini Msumbiji ambaye aliuawa na waasi wa kujiami kwa silaha
14 Septemba 2022, 14:27